Nimetengwa baada ya baba yangu kufariki

Nimetengwa baada ya baba yangu kufariki

Mdeke_Pileme

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2013
Posts
1,596
Reaction score
2,226

Baada ya baba yangu kutoweka duniani nimekataliwa kuwa sio mmoja wa familia.Nimekulia kijijini baba yangu alikuwa anaishi mjini.

Kutokana na kutokunitambulisha kwa ndugu na kuwatambulisha dada zangu pamoja na kaka zangu, baba wadogo na shangazi wanadai mbona wao hawakutambuliswa!

Kwa msaada wenu mnafikiri nini nifanye ili nami nipate haki yangu?
 
Hao ndugu zako ni baba na mama mmoja au baba mmoja mama tofauti?
 
Baada ya baba yangu kutoweka duninia nimekataliwa kuwa sio mmoja wa familia
nimekulia kijijini baba yangu alikuwa anaishi mjini ,kutokana na kuto kunitambulisha kwa ndugu na kuwatambulisha dada zangu pamoja na kaka zangu, baba wadogo na zangazi wadai mbona wao hawakutambuliswa!
Kwa msaada wenu mnafikiri nini nifanye ili nami nipate haki yangu?

Pole sana ila ushauri Wangu ni hivi you just move on hauko peke yako hata mimi ni mmoja wao so muombe mungu sana akupe nguvu na uendelee na maisha yako pole sana!
 
Kikubwa zaidi, ichukulie umri umefika wa kuoa, mke mtarajiwa anasema nami natamani kuja kwenu kwa wazazi wako, kwa mtazamo wako unafikiri nitampeleka wapi akidai twende kwa baba mzawa! Just help,
 
Lukas4 sidhani kama issue ya mtarajiwa wako kukutaka umpeleke kwa baba ni issue nzito ki hivyo otherwise kama unataka kupata share katika mali alizo acha mzee...huyo mwanamke mwambie ukweli kuhusu hali ya wewe na nduguzo basi!sidhani kama atalazimisha kwenda sehemu ambayo wewe hutambuliki...
 
Last edited by a moderator:
Wamekukataa kwa vigezo gani? Kutotambulishwa si kosa lako. Wanapaswa kukutambua sasa. je una kitu chochote kinachothibitisha wewe ni mtoto wa marehemu? kama picha, vyeti, watu wa kwenu n.k. Nia yako hasa ni nini? Urithi au kutambuliwa tu. Tafuta vithibitisho.
 
Pambana mkuu uhakikishe haki yako imepatikana. Hao wanao kuambia achana uachane na familia yako ambayo kimsingi ni muhimu kuijua
Hata kama haitakusaidia kitu.

KomAa nao kisheria.
 
vithibitisho vipo kama picha za utotoni ambazo nilipiga naye, furthermore baada ya kumaliza kidato cha nne baba yangu alikuja kunichukua na kunipeleka kwake kwa mama mkubwa na kumtambulisha pamoja pamoja na watoto zake. Pingamizi kubwa ni kwa baba mdogo na shangazi zangu, inafika mwaafaka ninakosa hadi amani kwamba mimi ninani kakika jamii!
 
Lukas4 sidhani kama issue ya mtarajiwa wako kukutaka umpeleke kwa baba ni issue nzito ki hivyo otherwise kama unataka kupata share katika mali alizo acha mzee...huyo mwanamke mwambie ukweli kuhusu hali ya wewe na nduguzo basi!sidhani kama atalazimisha kwenda sehemu ambayo wewe hutambuliki...

Asante, kwa hyo wazo lako mkuu mimi nijitenge?
 
Last edited by a moderator:
Kama mama yu hai, anaweza kuwa msaada mkubwa kukupatia vithibitisho.Pia uwezekano ni mkubwa akawa anafahamiana na baadhi ya ndugu wa baba
 
Katika kizazi chetu mambo ya ndugu, mali na misaada kimepungua sana ... na kwa mijini, tunaishi na ndugu wengi lakini kuonana ni mara chache sana na kuusu misaada, amini usiamini, kwa wengi wetu marafiki wamekuwa muhimu zaidi kuliko ndugu.

Kama umeshakuwa mtu mzima ... ondoa huo ukakasi wa ndugu, mali na haki yako kichwani kisha shikamana na ndugu wa mama unio nao kwani kosa kubwa la kutotambulisha limeshatokea kisha pambana kivyako, binafsi huwa naamini hii dunia haina mwenyewe i.e Ni yetu sote hivyo basi kila mtu anayo nafasi ya kufanikiwa.

Kazi kwako.

(Ni mtazamo binafsi)
 
Kama mama yu hai, anaweza kuwa msaada mkubwa kukupatia vithibitisho.Pia uwezekano ni mkubwa akawa anafahamiana na baadhi ya ndugu wa baba

kufahamiana kwao na mama ni kwamba kulikuwa kuna kaka wa kwanza alikufa mbaye alikuwa mkubwa kwangu ndiyo huyo wao ndio wanadai kuwa angekuwa yule wa kwanza wangekubaliana nae ila sio mimi,tatizo ndio hlo.
 
vithibitisho vipo kama picha za utotoni ambazo nilipiga naye, furthermore baada ya kumaliza kidato cha nne baba yangu alikuja kunichukua na kunipeleka kwake kwa mama mkubwa na kumtambulisha pamoja pamoja na watoto zake. Pingamizi kubwa ni kwa baba mdogo na shangazi zangu, inafika mwaafaka ninakosa hadi amani kwamba mimi ninani kakika jamii!

Kuna mali mnayopigania?
 
Sawa kabisa. Sasa nambie ni nini kusudio lako; kudai urithi? au?
 
Pambana mkuu uhakikishe haki yako imepatikana. Hao wanao kuambia achana uachane na familia yako ambayo kimsingi ni muhimu kuijua
Hata kama haitakusaidia kitu.

KomAa nao kisheria.

Haki gan mnayotaka apiganie?akipigania mali ataonekana kumbe shida yake sio undugu bali mali.

Kuonyesha anajali undugu basi kama kuna swala la mali ajitoe kabisa, asihangaike na hiyo mali kama ipo.
 
Kuna mali mnayopigania?

nyumba tatu town Guesthouse inavyumba 13, na nyumba mbili za kupangisha kwa nyumba mbili za kupangisha zinavyumba 20, gari moja, na shamba hekari 26.
 
munisijo;
Ushauri wa busara.

Kwa kuongeza tu, ata ndugu wa kwa Baba hawawezi kuwa na pingamizi na yeye kama TU SHIDA YAKE SIO MALI, hakuna mtu atakataa au kumchukia kwa kuwa Baba alizaa nje na ana vithibitisho ila watamchukia na kumkataa kama wanamuona ni oppotunist tu au ni mzigo tu anataka abebwe mgongoni.

Hivyo ni muhimu sana kuwa clear hapo kuwa hutaki msaada wa mali yoyote na kama kuna mgawo awaambie yeye wasimuweke.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom