Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
WOSIA WA MAMA KWA MWANAYE KUHUSU NDOA
1. Mwanangu, ukiona unatumia pesa kwa mwanamke na hajawahi kukuuliza kama unaweka akiba au kuwekeza, na anaendelea kufurahia tu, usimuoe huyo mwanamke.
2. Mwanangu, mwanamke anaweza kuwa mke mzuri kwako, wengine wanaweza kuwa mama mzuri kwa watoto wako, lakini ukipata mwanamke ambaye ni kama mama kwako, watoto wako na familia yako, tafadhali usimuache.
3. Mwanangu, nikikuambia wewe ni kichwa cha familia, usiangalie mfukoni mwako; angalia kama utaona tabasamu usoni mwa mke wako.
4. Mwanangu, kamwe usimpige mwanamke wako, maumivu ya mwili wake si kitu ukilinganisha na jeraha la moyoni mwake, na hiyo inamaanisha unaweza kuwa katika hatari kuishi na mwanamke aliyejeruhiwa.
5. Mwanangu, enzi zetu tulikuwa wake wengi na watoto wengi kwa sababu ya mashamba makubwa na mavuno mengi, lakini sasa hakuna ardhi tena ya kulima, kwa hiyo mkumbatie kwa karibu mke wako.
6. Mwanangu, usipoteze akili yako unapopata pesa zaidi, badala ya kutumia kwa miguu midogo isiyojua ugumu wa kazi yako, zitumie kwa mwanamke aliyesimama na wewe muda wote.
7. Mwanangu, nilipotupa mawe madogo au kupiga filimbi kwenye dirisha la nyumba ya baba yake mama yako, haikuwa kwa ajili ya ngono, ilikuwa kwa sababu nilimkumbuka sana.
8. Mwanangu, mama yako, Asake, alipanda baiskeli nami kabla sijanunua gari lile la kobe nje pale, mwanamke ambaye hatavumilia nawe mwanzoni mwa safari yako hafai kufurahia utajiri wako.
9. Mwanangu, kuna kitu mnaita feminismi, sawa, kama mwanamke anadai haki sawa na wewe nyumbani, gawanya bili zote mara mbili, chukua nusu na mwambie aanze kulipa nusu nyingine.
10. Mwanangu, baba yako alinikuta bikra, alitumia siku mbili kunitoa bikra, kitanda kilivunjika zaidi ya mara tatu, nilichukua viazi zaidi kwa baba yake, kama humkuti mke wako bikira, usimlaumu, kile ambacho sikukueleza ni kuwa wanawake wetu walikuwa na heshima.
11. Mwanangu, sikupeleka dada zako shule kwa sababu nilikuwa mjinga kama wengi waliofikiria mtoto wa kike hawezi kuendeleza jina la familia, tafadhali usifanye kosa hilo, mafanikio ya wanawake wa siku hizi yamefanya jinsia ya kiume kuwa tu alama ya kawaida.
12. Mwanangu, mama yako aliwahi kunifungia nguo niliyokuwa nimevaa na karibu aichane kwa sababu alikuwa na hasira, sikuwahi kuinua mkono kumpiga kwa ajili ya siku kama hii, ili niweze kujivunia kukwambia kuwa sikuwahi kumpiga mama yako hata siku moja.
13. Mwanangu, enzi zetu, wanawake wetu walikuwa na uzuri wa asili zaidi, ingawa sitakudanganya, wengine walikuwa na michoro midogo ya wino mikononi mwao, walipaka hina, ambayo mnaita tattoo siku hizi, lakini usisahau kwamba hawakuwa wanavaa nguo fupi zinazoonyesha sehemu za miili yao kama wanawake wa sasa.Mwanaume ikitokea akiona paja la mwanamke enzi zetu basi "lazma apate mfadhaiko, "mjomba asimame" na lazma huyo mwanaume aote alichokiona.
14. Mwanangu, mimi na mama yako hatutaki kuingilia mambo yanayotokea kwenye ndoa yako, jaribu kushughulikia matatizo bila kutuambia kila mara unadhalilisha heshima ya ndoa yako na mwenza wako,usifungue mdomo wako bali tibu hilo tatizo. Kuna mengi huyajui tuliyo yapitia kwenye mahusiano yetu hakuna lazima wewe kuyajua.
15. Mwanangu, kumbuka nilimnunulia mama yako mashine yake ya kwanza ya kushona, msaidie mke wako kutimiza ndoto zake kama unavyoendelea kutimiza zako. Usije kusahau jambo hili mwanangu.
16. Mwanangu, usiache kututunza mimi Maliyawatu na mama yako, ni siri ya kuishi muda mrefu na kupata watoto watakaokutunza pia. Apandacho mtu ndicho huvuna mwanangu.Mimi Maliyawatu ninafanya hivyo Mwanangu
17. Mwanangu, omba na familia yako, kuna kesho usiyoijua, zungumza na Mungu anayejua kila kitu, kila siku.