Nimetofautiana na jirani yangu, naombeni ushauri

Jenga ukuta matawi yatakayo vuka ukuta utafyekelea mbali huku ukiwa ndani kwako akija kungonga getini muulize wakati unagonga geti si unajua ni kwa mtu bas huyo mtu kafanya maamzi nyumbani kwake kuhusu mazingira
 
Mkuu Nahuja, inaonekana kuwa jirani yako hataki ujirani, hafikirii kuwa na uhusiano mwema, hivyo mueleze waziwazi kuhusu nia yako ya kupeleka mgogoro ngazi ya kisheria halafu umsikie.

Vv
 
Nina uchungu mkuu stickvibration ila sasa ndio hivyo tena, nashindwa chakufanya ndio nimewaomba ushauri, nashukuru mnanishauri vizuri
 
Mkuu Nahuja, inaonekana kuwa jirani yako hataki ujirani, hafikirii kuwa na uhusiano mwema, hivyo mueleze waziwazi kuhusu nia yako ya kupeleka mgogoro ngazi ya kisheria halafu umsikie.

Vv
Anauza hiyo sehemu, pia anaringa kwa kuwa ni polisi!!!
 
Hiyo ya kukata miti siwezi ni mirefu sana inatakiwa kukatwa kwa ufundi ili isiangukie nyumba. Kuhusu kumtandika makofi sina nguvu za kumpiga ni mwanamme. hahahahah mimi ni mwanamke. Kumlaza selo ni ngumu ni POLISI
Ondoa woga, tena kama ni polisi ndiyo rahisi zaidi, mpeleke kwa mkuu wake wa kazi, kama ni IGP piga hodi kwa Katibu Mkuu wa Wizara , Meja Jenerali Rwegasira.

Vv
 
Huwa hakuna mkate mgumu kwenye chai, wewe umeshasema ni mwanamke na yeye ni mwanume tena mkurya, huwa hakuna mwanaume mjanja mbele ya mwanamke, andaa chakula cha jioni maridadi kabisa, ikiwezekana tafuta na kichuri, mtumie mtu ambae ana ukaribu nae au anaemmudu umkaribishe kwako kwa anuani ya kuja kuzungumzia biashara ya kuuziana hicho kiwanja (hawezi kukataa). Akifika nyumbani kwako jishushe, kuwa mkarimu mpaka mwisho (wakurya wa Dar hawana tabu kabisa), zungumza nae kwa vituo na kwa kujiamini, ukiona anaelekea kutoelewa mpapase shingoni kidogo, ikiwezekana pitisha vidole masikioni mwake huku unamtazama machoni kwa jicho la nusu mwezi, akirembua tu unaingiza vigezo na masharti kuzingatiwa, hapo mgogoro unakuwa umekwisha, unamwambia kuwa akate miti ili uje umpe zawadi ya ushindi, ataikata hata kwa kisu cha nyanya! Case closed!
 
Ahsante sana
 
Du! weee Kisusi Mohammed jamani loooh!
 
Ondoa woga, tena kama ni polisi ndiyo rahisi zaidi, mpeleke kwa mkuu wake wa kazi, kama ni IGP piga hodi kwa Katibu Mkuu wa Wizara , Meja Jenerali Rwegasira.

Vv
Koplo
 
Anzia kwa mjumbe pata ushauri wake kwanza
 
Ngumu sana! Ahsante sana popoma03
Mkuu utafanyaje hayo mambo ya kisheria ni mapana sana na hata kama ukilipwa fidia it doesn't matter nakushauri tafuta watu wa kazi usiku mnene tena huko mwanza siku hizi mvua zinanyesha wamalize miti yote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…