Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Na
Nanyori mambo!
 
Pole sana. Ila huyo mwanamke usimuache, huyo ndie chaguo lako. Narudia tena usimuache, huyo ni mke mwema kabisa kwako. Mambo ya baba mkwe achana nayo, hayo yanatokea tu kila sehemu. Mshukuru MUNGU sana huyo mwanamke anakupenda na anaupendo wa kweli.

Iliwahi tokea Kwa mdogo wangu alikuwa anaowa Mwanza, siku ya Mahali tulikutana na kizingiti kikubwa sana, ila mjomba wake na Binti alisawazisha mambo na kuwaambia maisha yanaendelea na yanaendelea l, hivyo Mahali aliyonayo atoe, tukatoa 1.4 million badalaa ya 4 million. Na mchakato ulikuwa mgumu sana na tulitoka mbali (Iringa).

NEEMA YA BWANA WETU YESU KRISTO NA UPENDO WA MUNGU BABA NA USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU ZIWASHUKIE NA KUKAA NANYI DAIMA.
 
Waende wazee kutoka Dar mpaka Kigoma halafu ndo niende mimi tena?why???
Karma haijawahi kumuacha mtu salama mkuu...!

Kumuacha mke kwa makosa ya mzazi wake...na kumsababishia maumivu...hiyo karma itakuandama popote uendako....

kwa maumivu utayokuwa umemsababishia.....

If you truly love her...... embrace her...

Pesa zinatafutwa chief.....Lakini kutafuta na kumpata mtu mnaependana kwa dhati.....!
Hilo ni jambo jingine kabisaa!....

Pia....Kwa ninavyofahamu.....Mahari inaweza kulipwa kwa awamu.

Hata marehemu baba enzi za uhai wake....aliwahi niambia kuwa bado ana deni la mahali kwa mama yangu....

Kikubwa ni malipo ya awali tu...maana vingine umeshatekeleza.

The Choice is Yours....!Akili kumkichwa
 
Hzo faini lengo lake ni nn hasa...👣
 
Siku moja nilienda shambani kwangu nikakuta kijana wangu wa shamba mkewe hayupo, nikamuuliza vipi mbona uko pekeyako? Akanijibu we acha tu…. Akasema wajomba wa mkewe wamekuja kundi la watu kumfuata mtoto wao (huyo mkewe)

Nikamuuliza kwahiyo wamesemaje? Akajibu wameniambia niende nikalipie utamu la sivyo mke harudi. 😂

Enzi hizo mimi naishi bila ndoa natoa tu utamu bure bure, nikajisemea kumbe I’m selling myself short. 🤣 anyways masuala ya mahari huko vijijini ni very big deal.
 
Ngoja niweke busara za kupaka rangi maneno na kuyelemba kando. Nikupe busara za kiutawala na ubabe.

Hapo hakuna ishu ya mzee kuwa na hasira wala nini, hapo ni Game ya Utawala. Mzee karusha kete zake, ukiingia huo mtego wake, atakubulizaa hasaaa. Busara zake zero, mtu kaonyesha unyenyekevu kutoka alipo unaishia kufoka na kusema hakuna mjadala [emoji848].

Wewe huna majukumu ya ku solve matatizo yake, kiuchumi, au kijamiii, inafanywa kwa upendo na ushirikiano, sio jukumu lako ku show up ktk majanga yao, wewe yako wanaweza kuyashiriki?.

Msaada wowote ukweni ,sio jukumu lako, ni yeye na kete zake za ujanani hadi uzeen au watoto wake wafanye hayo, ishu sijui hujaenda kutoa pole sijui nn, hoja za kitoto.

Hawezi kukutreat kama muharifu, hukubaka mwanae, ni maelewano na alikuja kwa ridhaa yake yeye. Hakuna jeuri uliyofanya. Je, alitaka before kukaa na mwanae au kulala naye ungetuma barua ya maridhiano,?.

Ukiangukia ktk huu mtego,jiandae kuja kubuluzwa ktk maamuzi hata familia yako. Utapewa majukumu ya ukoo au mashemej, utasikia tu, shemej yako anakuja mpokeen hiyo ni final.

Chekecha akili, simika dominance yako hapo, yeye kasusa, hajasusa ni ego tu ya hao watu viburi tu,wabishi sanaaa. Vungaaa cheza na akili yake like u don't care.

Harafu usitishwe na sijui uchawi na nini, angekuwa na uwezo na kila kitu , asingekuwa bush huko,asingekuwa na mawenge aliyo nayo. Usitukuze uchawi wala kuhusudu ishu zao. Ogopa MUNGU pekeeeee, weee kaa vizuri na MUNGU, hakuna boya wa kuchukua uhai wa familia yako.

Damu nzito kuliko maji, unaambiw tu ,et kama mama mkwe yuko poa sijuii nini, oyaaa huyo ni mumewe hawez kumsaliti over you, kuhusu binti sijuii wewe wamjua vyemaa.

Tafuta ushauri wa kiroho ,uone ktk lipi utakuwa safe zaidiiii, wanawake wapoo tu, kama vipi anza life lako, watakuja wenyeweee. La msingi timiza jukumu lako lea mtoto wako, tuma matumizi, then mengin waachie wao. Ukiulizwa waambie sina Milion 4, niliyo nayo nimewapa yote. Kuna maisha nje ya ndoa na mapenzi.
 
Sio wote wanakuwa single mother kwa scenario Kama hiyo
 
Kwa hiyo baada ya kuzaa nilitakiwa kutokomea siyo?
ukitokomea ni hasara yako mwenyewe,maana ukimtelekeza toto linakuwa tajili la kutisha afu baba mtu unakuwa na maisha ya digidigi una baki kulia lia kwenye media eti mwanao hakujali, mi ni muha .ki kwetu nikosa kumzalisha mwanamke kabla ya kumuoa kwani ina hesabika ni dharau kwa familia ile
 
Kwa hiyo kwa mtazamo wako sisi kutoka Dar mpaka Kigoma kwenda kuyajenga tulikuwa wapumbavu?
Ilikuwa busara kuona dhamira yetu na kuwa muungwana, ila kwa réaction aliyoonyesha atabaki n'a mtoto wake tu, siwezi kuwa n'a baba mkwe wa aina yake

Unasemaje atabaki na mtoto wake ilhali uliondoka naye na upo naye.!

Kama una akili timamu ungeshajua kuwa imeisha hiyo, mzee hataki tu kukuchekea ila mkeo hapo hatoki…. ulishindwa kumwacha kwao siku hiyo huwezi kumtimua.
 
Kweli mkuu jamaa walimfanyia makusudi kama kumkomoa kwa kuchelewa kujitambulisha ukweni na kama angeweza kuwa nao karibu kipindi cha nyuma hyo mahari isingefika gharama hzo tatizo lililokuwepo yeye kutojitambulisha mapema na kuzalisha mtoto wao pasipo yeye kufahamika ukweni wamefanya kwa kumkomesha tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…