Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Makosa si ya mwanaume pekee, hata mdada ana makosa. Mahusiano ni ya watu wawili!!!
 
Wakataja kiasi cha mahari kuwa wanataka mil. 4.5, hapo tukashtuka kweli, kabla hatujakaa sawa wakataja mkaja wa mama sh. laki saba, jumla wanataka 5.2 Milioni!
Hukupaswa kushituka,

Jukumu lako ilikuwa kusikiliza, kisha unaondoa ile sifuri ya mwishoni, hapo itasoma 520,000 unamkabidhi mshenga jukumu la kuweka sawa mambo, unachukua mke, NAni kakwambia mahali huwa inalipwa yote?
 
Aisee, hapa tatizo tayari. (naendelea kusomma)
 
Ulipata mshenga makini sana.
 
Wewe ndo mwenye shida mkuu.. jishushe tu... milioni 4 kitu gani? tafuta upeleke.. mke wako unasema hana shida,ila kumbuka huyo ndo baba yake
 
Aisee pole kwa hii changamoto uliyokutana nayo.
 
Very sad kutegemea mtoto akiwa tajiri aje akusaidie, ufinyu mkubwa wa kufikiria huu, nadhani kila mtu anatakiwa kujiandaa kwa uzee, n'a hata mtoto akiwa bilionea kiasi gani ni za kwake n'a kamwe siwezi kulia lia eti hanipi hela, never!
 
Tulienda na gari tuaiacha mjini, kutoka mjini kwenda huko Kijijini tulikodi boda boda kwani njia ni mbaya mno!
Bodaboda saa 8?? Afu unafika unaambiwa milioni mezani?? Mmmmmae mimi ningekua mshenga wako ningekushauri tuwaage kama tunafata hela benki ndo ingekua mazima
 
Dah!pole sana mkuu.....ila umeingia nyumba sio....maisha gani ya kuishi unaogopa kurogwa
 
pole sana mkuu kuna mila na tamaduni za ovyo sana baadhi ya sehemu
 
Pole sana, wazee wanatafuta mitaji ya biashara kupitia mahari aibu tupu.
 
Muwe mnauliza mambo yote kabla ya kupeana mimba.
Mwanamke wa watu anaenda kiwa single mother bila kupenda.Mtoto anaenda kulelewa na mzazi mmoja bila kupenda.
 
Very sad kutegemea mtoto akiwa tajiri aje akusaidie, ufinyu mkubwa wa kufikiria huu, nadhani kila mtu anatakiwa kujiandaa kwa uzee, n'a hata mtoto akiwa bilionea kiasi gani ni za kwake n'a kamwe siwezi kulia lia eti hanipi hela, never!
acha kiburi cha kijinga je unaamini maisha uliyo nayo utakuwa hivyo milele? acha kuongea pumba wakati huijui kesho yako.hebu tufanye kama unabeba hicho kiatu cha huyo mzee unamsomesha mtoto kwa shida anafika mpaka chuo unasubili kupata matunda kwa mtoto wako gafla anatokea mjinga mmoja ana mzini mwanao afu baada ya kumpa ujauzito anamwambia nenda kajifungulie kwenu, mtoto amejifungua tayali ndo aje kujifanya anatoa mahali utajisikiaje? waha sio cheap kama mnavyofikiri
 
utasikia ngonjera nyingi sana.....ila tambua kitu kimoja tu..mahali hua aimalizwi...mtia em moja mzee afu kausha.
NB;ukijifanya unatoa zote tu umerogwa man.
SHTUKA MTEGO HUO
 
Ningekuwa Mimi ningewavimbia hapo hapo, niliwahi kuwatolea makavu hawa wahehe wa kwangu siku naenda kulipa mahali ili nimuoe binti yao.

,Tangu namuoa binti yao hawanichukulii Kama mtu wa kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…