Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Ben-adam

Kigoma sio sehemu ya kuoa usije kujaribu, kuthubutu au kumshauri yeyote yule.
Niliwahi kuwa na msichana mrembo sana mzawa wa huko, aliisumbua sana akili yangu kwa kuwa nilikuwa nampenda sana. Tulidumu kwa miaka takribani minne.
alikuwa Na gubu moja Pro Max, sijui kama kuna mwanamke anaweza kumpiku. Tuliachana baada ya kuona anataka alete itikadi za kunipelekesha kindezi kama vile ananimudu. Ilikuwa ni mwezi mtukufu, kwakuwa mi sikuwa muislamu ilitokea siku moja kaniletea habari sizo.

Tumeongea na simu usiku akaniambia natakiwa nimuamshe muda wa daku kwa kumpigia simu. Nikamwambia kwanini asiweke alarm tu maana naweza kupitiwa hadi muda huo nisiwe macho. Eti anakaza serious, ikabidi niingize vimjadala vingine kumtoa kwenye tension, naona hatoki eti kakaza tu nikasema basi sawa nitakupigia.
Bahati mbaya nilipitiwa, asubuhi naamka nampigia simu hapokei, piga sana hakuna tu, nikatuma sms ya kumsihi apokee simu tuongee lakini kimya. Hadi saa nane mchana nahangaika tu kumtafuta lakini wapi. Nikaona huu sasa ufala, ananipeleka vipi huyu, nikaandika sms moja waraka, ndefu kumtolea maneno makali kidogo, akajibu eti niendelee na maisha yangu.
Yaani kama angekuwa karibu ningeua, nilipatwa na hasira kali sana, nikijaribu kupima naona kabisa mbona sioni kosa hapo? Hata kama lipo ndio la kuniletea upumbavu ule? Nikawaeleza baadhi ya watu, ila bado waliona sina kosa.

Nikala kiapo cha DAMU, haitokaa itokee nirudi kwa huyo kima au hata watu wa jamii yake. Cases zilikuwa kibao ila hii ndio ilikuwa ya mwisho nikainua mguu moja kwa moja, nikafunga ukurasa na kitabu nikapiga moto.[/B]
 
Usije ukathubutu kumtamkia maneno hayo huyo mke wako.
Huo mtihani umeshaupita, ila mapito hayo usije ukayatumia kumchapia mwenza wako. Huyo mwenza wako ni stahiki yako, usimuumize.
Huyo mzee ana stress zake, huenda kuna mzee mwenzake waliahidiana kuunganisha familia kupitia watoto wao na huenda mzee tayari alikua akivutavuta vihela vya hapa na pale.
 
USIPELEKE POSA MWENYEWE VIJIJINI AMBAPO HAWAJUI MAMBO YA KISASA YA KUZALISHANA NA KUISHI BILA RIDHAA YA WAZAZI ESP PALE AMBAPO USHAISHI NA BINTI NA MIMBA UMEMPA. MILA NYINGI NA TAMADUNI HUCHUKULIA KAMA DHARAU KWA WAZAZI NA AIBU KWA JAMII YA PALE NA MZEE WA BOMA ANAKUWA NA HASIRA KWA AIBU ALIYOIPATA HAPO KIJIJINI.

TUMA MZEE AMBAYE ANAJUA TARATIBU ZA HUO UKOO IKIWEZEKANA NA KILUGHA ANAONGEA. KAMA HUJUI WEWE UNAWEZA KUDHANI KUWA UNAENDA KWENYE JAMBO LA HERI NA UNASUBIRIWA KWA FURAHA KUMBE WAZEE WANAKUSUBIRI WAKIJUA UNAKUJA KUOMBA RADHI KWA KUWAKOSEA. SASA UKIFIKA HAPO BILA KUJUA NINI CHA KUFANYA LAZIMA MAMBO YAVURUGIKE.
 
Kwahiyo gharama za kumsomesha zinalipwa na mahari...?, Angekua jobless baada ya chuo hizo gharama angezirudishaje..?

Nyie ndo mnaona watoto wenu ni mitaji ya kuwatoa kwenye umaskini wenu [emoji706][emoji706]
We uoni kama kampoteze muda binti wawatu miaka yote walivyoishi pamoja na kumzalisha na itakuwa miaka yote hiyo binti alikuwa hana shughuli yoyote ya kumuingiza kipayo, we fikiria binti aishi na mwanaume kinyumba bila ndoa wala familia kujua na azalishwe unaona ni sawa? Huyo binti angekuwa haja zalishwa wala hajishi kinyumba kwa sasa angekuwa anafanya kazi yoyote halali ya kumuingiza kipato na mpaka sasa angekuwa kiuchumi yupo mbali na angesaidia familia yake, sasa jamaa yeye anafanya kazi na anasaidia familia yake, Mwanamke yeye alikuwa yupo nyumbani tu sasa kwa mfumo huo si bora wazazi wake wange muozesha mapema.
 
Chukua mke tulia na familiar yako....

Mbona mimi niliambiwa ng'ombe wa 5 kwa kiasi cha laki 3 kwa kila ng'ombe mmoja ila nililipa laki Tano mpaka leo mwaka wa 6 huu napeta tu,!!.

Mahali aimalizwi bob , wakikuomba waambie huna (hali ngumu) wataacha tu hasa mtoto wao kama anakupenda ..!
 
Waende wazee kutoka Dar mpaka Kigoma halafu ndo niende mimi tena?why???
Wewe ulienda kufanya nn.? Unaleta dharau...kwani huna wazazi? We ungepeleka wazazi, wakawakiana pale weee, baadae wangeelewana....peleka wazazi acha dharau kwenye familia za watu
 
Huyo alikua kashaamua kukuacha kitambo na hapo alikua anatafuta kaupenyo. Sababu ya kitoto sana mtu kununa kisa hujamuamsha sasa alarm kwenye simu yake ipo kwa kazi gani? Ujinga tu.
 
Sheria kali kule ukimpa binti uja uzito lazima umuoe, na kule hakuna tabia ya kuishi tu na mwanamke bila ndoa na kuzaa watoto, kila jamii ina taratibu zake, mfano Wamasai uwezi kuishi tu na binti wa mtu ukamzalisha tu, jambo alilofanya huyo kijana ni laki uni tu, tunatakiwa tulikemee kwa nguvu zote ili kuepuka kuwa na watoto wa mitaani .
 
Madhaifu yetu ni makubwa kwenye maswala ya ndoa mfano huyu yeye kaishia na binti wawatu bila ruhusa na hajulikani upande wa familia ya mwanamke je binti ange pata matitizo, kuna jamii hivi vitendo hawa vikubali kabisa mfano hawezi kufanya kwa binti wa kimasai.
 
Kwani huyo mwanamke ni mtoto? Hajitambui yeye? Aliamua kuishi na jamaa yake akiwa na akili zake timamu sidhan kama alilazimishwa. Mimba kabeba kwa hiyari yake hakubakwa eti. Kama kukosea wamekosea wote muhimu jamaa arekebishe pale alipokosea basi
 
Hapo mkuu kamq unampenda huyo msichana tafuta wazee hata kama wa kule kule kigoma,au wajomba na akina baba mdogo wa binti ongea nao waongee na mzee. Hapo mzee kaona kama umedharau familia kwa kukaa mda mrefu pasipo kujitambulisha.
 
4mil amekua kiwanja??
 
Huyo alikua kashaamua kukuacha kitambo na hapo alikua anatafuta kaupenyo. Sababu ya kitoto sana mtu kununa kisa hujamuamsha sasa alarm kwenye simu yake ipo kwa kazi gani? Ujinga tu.
Akili zake alizijua mwenyewe tu. Huenda alitegemea ningejiliza kama ambavyo nilikuwa nikifanya kabla. Safari ile nili-decide moja kwa moja. Nilipata mfululizo wa kutafutwa kwa namba ngeni lakini I ignored them. Hope was her.
 
Akili zake alizijua mwenyewe tu. Huenda alitegemea ningejiliza kama ambavyo nilikuwa nikifanya kabla. Safari ile nili-decide moja kwa moja. Nilipata mfululizo wa kutafutwa kwa namba ngeni lakini I ignored them. Hope was her.
Alijua unampenda sana maringo kibao. Na hivi ndio inatakiwa unampenda mtu nyodo kama zote siku ukiamsha unaamsha kimoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…