Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Hizi blanket statements ni ujinga. Huwezi jumlisha watu wote wa mkoa au kabila fulani kwa ujinga wa mtu mmoja.

Kisa mchaga mmoja kaua mme wake. Haliwezi kuwa kosa la wachaga wote.

Mpare mmoja bahili sio wapare wote.

Msukuma mmoja mshamba sio wasukuma wote.

Mrangi mmoja malaya sio warangi wote.

Mhaya mmoja mjivuni sio wahaya wote.

Mtanzania mmoja mvivu sio watanzania wote.

Mtu yeyote anayetoa sweeping statements ni mjinga.
 
POLE SANA MWANANG. WE CHUKUA MKE WAKO ONDOKA NAYE AU M UACHE AKUFUATE HALAFU ULE PINI UONE WATAKAVYOHANGAIKA KUKUTAKA KUTOE CHOCHOTE YAISHE. HUWEZI KUMALIZIA UMASKINI WAKO KWA MWANAO. HUKU NDIKO HUITA KUKOSA UBUNIFU. UTAKUTA H UYO BABA ANAYEDAI MILIONI NNE HAKUTOA HATA MALI KWA MAMA. MKWE WAKO. KIMSINGI, HUO NI UTAPELI NA WIZI WA WAZI WAZI. UKIFIKA NYUMBANI MPIGIE SIMU BABA MKWE WAKO KUWA UMEPATA BINTI MWINGINE WA LAKI MBILI HIVYO, MWANAE ANAWEZA KUOZESHA MWENGINE NA MJUKUU AKITAKA ACHUKUE. MWAMBIE KWA HESHIMA KUWA BABA SINA UWEZO HATA WA NUSU YA HIYO FEDHA. HUO NDIYO USHAURI WANGU MWANANGU ILA NAWE UNGEFANYA RESEARCH KIDOGO BADALA YA KUKURUPUKA NA TAMAA ZA MWILI KUMBAFF KABISA
 
Ndio milioni tano? Bora nihasiwe, siwezi toa hiyo hela kuoa, tena mwanamke wa kiha. Labda mleta uzi
 
Mbaya zaidi ntalazimika kumuacha mtoto wao kwa makosa ya baba yake
Kama utaamua kukuacha mtoto wao ambaye unathibitisha kabisa kuwa anakupenda na hana shida kwa ajili ya matatizo ya Mzee wake basi hutakua na tofauti na huyo Mzee tena wewe ndio utakua kiande kabisa.
 
We jamaa una ego kali sana, hutaki ushauri wowote cha msingi fanya unachoona wewe ni sahihi.
 
Ushauri mzuri sema jamaa anaonekana ni mbishi sana km wakwe zake
 
haha ndio kigoma mimi nshaacha kabisa kijana wangu huko miaka 14 sasa....mama mkwe yule mwalimu wa kasulu dizain kama zako....kha....
 
Chekecha na Wajomba..
Washenga tupo hapa wenye cv kali na kuketi mezani pa bwana na Wazee wa namma hiyo.
 
Maamuzi mazuri mkuu...Achana na hao wapuuzi ila mwanamke usimuache kama hana shida na usikubali akaja kukuyumbisha na presha atakazokua akipewa huko kwao,watalegeza wenyewe tu wakiona miaka inaenda na haurudi.
 
Hapo kwa simulizi yako, mwenye shida ni baba mkwe wako, wengine sijaona ubaya wao, "usiwahukumu waha wote kwa ukorofi wa mkwe wako"

Ukorofi ni asili na hauna kabila.

Lea familia yako, usikimbie majukumu. Umemuoa mkeo na si mkweo!


Kama mkweo alikosea, je wewe kumpa mimba mtoto wao, kukaa nae bila taarifa ni sahihi kibinadamu na kidini? usione kibanzi cha mwenzio while una boriti kwa jicho lako...
 
Pole mkuu. Lakini hiyo mahari nadhani ni reasonable hasa ukizingatia ulimzalisha mtoto wao na ulichelewa kwenda kujitambulisha! Mimi sijamzalisha wa kwangu lakini nimepigwa mahari 3.8 M na wanyakyusa wa Simike wale!
 
Hiyo Ilinitokea miaka ya nyuma kiasi baada ya kuzaa na binti yake nikaenda Kujitambulisha. Yule mzee mwanajeshi kidogo aniue siku ile.lakini nashukuru familia na ukoo wote ulikuwa upande wangu.nimejaliwa watoto sita. Mpaka mda huu ninaye hapa nyumbani jumatatu nampeleka muhimbili kupima tezi dume
 
Ulokosea walipopata msiba ungetuma pole mshukuru mshenga wako ana busara sana, ila baba mkwe alizidi.
 
Huo undugu unavunja na nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…