Mkuu ogopa sana jamii zenye asiri ya machafuko. The only way used to protect themselves was through witchcraft. So baada ya kupata sehemu iliyosettle hayo mambo hawakuyaacha na sasa wamegeuza malengo ya zamani😌Hivi ni Kabila au ni hulka za watu tu?
Naamini kuna waha swaaafi kabisa n'a kuna wasio kuwa waha n'a ni washirikina mbayaaaa..
Kama nimekuelewa vileeeMkuu ogopa sana jamii zenye asiri ya machafuko. The only way used to protect themselves was through witchcraft. So baada ya kupata sehemu iliyosettle hayo mambo hawakuyaacha na sasa wamegeuza malengo ya zamani[emoji18]
Asante kwa kunielewa, nimetumia fasihi zaidi ili nisivamiwe na wenye makabira yao 😆😆Kama nimekuelewa vileee
Dogo, kama yamekukuta kweli, ni stori ya mwezio au umetunga! Kama kweli ni wewe basi una safari ndefu sana ya maisha. Unachikulia poa masuala serious, unaona ni kitu kidogo tu, unajiona uko sawa, huonekani kujutia wala kukubali kuwa una makosa na kuwa hayo waliyokufanyia walikuonea!Umeandika kwa mihemko sanaaa, nani amesema alitaka kupokelewa kwa maturumbeta?
Kipi bora, kwenda kuyajenga n'a kuweka sawa? Au kupotelea mitini mazima wabaki na mtoto na mjukuu wao?
Halafu ukisema hawakutaka pesa, unathibitisha kwamba walitaja pesa nyingi ili nishindwe kulipa wabaki na mtoto wao?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Asante kwa kunielewa, nimetumia fasihi zaidi ili nisivamiwe na wenye makabira yao [emoji38][emoji38]
Mlienda na gari yenu private? Kwanini usingewabeba wazee wa heshima (akiwemo baba yako?) Angalau baba mkwe wako asingekuwa na hasira na wewe, mlienda wepesi mno ndo maana, wazee huwa wanaongeza uzito wa ugeni. Bro wako tu asingetoshaTulienda na gari tukaiacha mjini, kutoka mjini kwenda huko Kijijini tulikodi boda boda kwani njia ni mbaya mno!
Unatokea pande gani za nchi ambazo hawana mambo haya? Haya mambo yanapungua kadiri jamii zinazovyochangamana na jamii ngeni na zinavyozidi kuendelea na kuelimika.Waha hawajambo kwenye hayo mambo mkuu [emoji1787][emoji1787]
Nasikitika kwamba unanihukumu kwa hisia zako tu, ukisema nilitakiwa kwenda kwa "unyenyekevu mkubwa" una maanisha nini? Kwamba nilienda pasipokuwa mnyenyekevu?Dogo, kama yamekukuta kweli, ni stori ya mwezio au umetunga! Kama kweli ni wewe basi una safari ndefu sana ya maisha. Unachikulia poa masuala serious, unaona ni kitu kidogo tu, unajiona uko sawa, huonekani kujutia wala kukubali kuwa una makosa na kuwa hayo waliyokufanyia walikuonea!
Ulitakiwa uende kwa hofu na unyenyekevu mkubwa ili mambo yasiwe makubwa. Kumbuka wewe nawe ni mzazi, unapaswa kujifunza na kujiandaa kwa ajili ya nyakati zijazo. Uyafanyayo sasa huenda utakutana nayo baadaye, jifunze kitu, jifunze ku-handle haya mambo kwa hofu na unyenyekevu, huenda hayo uliyofanya na kuyafanya dhidi ya mkweo, naye ujanani alikuwa na akili kama zako na sasa wewe unatumika kumkumbusha aliyomfanyia mwenzake.
Vv
Nakubaliana na wewe.Unatokea pande gani za nchi ambazo hawana mambo haya? Haya mambo yanapungua kadiri jamii zinazovyochangamana na jamii ngeni na zinavyozidi kuendelea na kuelimika.
Vv
Huyu kaka yangu ana zaidi ya miaka 50, lakini ndiye baba yetu kwani baba mzazi alishafariki miaka mingi tu!Mlienda na gari yenu private? Kwanini usingewabeba wazee wa heshima (akiwemo baba yako?) Angalau baba mkwe wako asingekuwa na hasira na wewe, mlienda wepesi mno ndo maana, wazee huwa wanaongeza uzito wa ugeni. Bro wako tu asingetosha
Pole sana mwamba. Emu jipe muda kila kitu kitakuwa sawa tu hakuna mzazi asiyependa binti yake aolewe.Huyu kaka yangu ana zaidi ya miaka 50, lakini ndiye baba yetu kwani baba mzazi alishafariki miaka mingi tu!
That is why,nilinunua zawadi za yule mzee kichwani nikiamini atakuwa baba yetu (Mimi na mke wangu) lakini alinivunja moyo sanaaa!
Ninaweza kuendelea na maisha na mke wangu, lakini yule mzee sijui kama nitampa value niliyokuwa nampa awali, na kwa vyovyote vile mke wangu hawezi kukubali baba yake asithaminiwe na mimi mumewe, inaweza kuwa shida baadaye, that is why nafikiria kumuacha tu, nihesabu kwamba nimekataliwa kwao n'a mimi siwezi kulazimisha!Pole sana mwamba. Emu jipe muda kila kitu kitakuwa sawa tu hakuna mzazi asiyependa binti yake aolewe.
Ahsante japo ndiyo maisha yenyewe, tunajifunza kila sikuPole sana Mkuu
Mkuu si Kila anayeishi na mke anayempenda anamahusiano mazuri na wazazi hapana wewe jikite kuwasamehe hujui makuzi ya Mzee hivyo inahitaji utulivu wa Hali ya juu na endelea kuwa na mawasiliano na mshenga kujua kama utulivu mmemrejea mzeeNa hapa ndipo penye mkwamo, nakosa namna yoyote ya kufanya isipokuwa kumuacha kabisa mtoto wao, japo ni kweli nampenda ila sina namna!
Sidhani kama unampenda kweli unampenda huyo dada, upendo una gharama, kama kweli unampenda gharama haziwezi kuzuia nia yako ya kufunga naye ndoa, mtu ni raslimali nambari moja. Au huyo dada yeye hachangii kwente uchumi wako? Kama hana mchango, mnapanga iwe hivyo maisha yenu? Yakobo [kama unasoma Biblia], kwa upendo wake kwa Raheli, alikuwa tayari kumtumikia mkewe kwa miaka 7 zaidi.Nasikitika kwamba unanihukumu kwa hisia zako tu, ukisema nilitakiwa kwenda kwa "unyenyekevu mkubwa" una maanisha nini? Kwamba nilienda pasipokuwa mnyenyekevu?
Brother kwa akili ya kawaida tu, unawezaje kwenda ukweni, tena kwa mara ya kwanza na usiwe mnyenyekevu? Au unyenyekevu unaomaanisha ni wa aina gani?
Halafu ni mtu katili pekee anayeweza kufikiria kuwa safari ya Dar mpaka Kigoma, nikiambatana na kaka yangu mkubwa (mbadala wa baba yangu kwani mzee alishafariki) ni mzaha, lakini kwa yeyote aliye timamu kabisa alipaswa kuiona hiyo dhamira yetu,na angalau kutupokea kama binadamu (hata kama kuna makosa tuliyowahi kuyafanya, mimi n'a mtoto wake)
Lakini kutu-harass na kutufedhehesha mbele za watu,na kutaja pesa anazojua kabisa kuwa hatuwezi kuzilipa ni ukatili mno!
It is just to share the experience,wala sio kutafuta kuungwa mkono na yeyote!Mtoa mada anatafutwa uungwaji mkono tu.
Humble yourself, elewa watu wanachokuambia, funika kombe mwanaharamu apite.
Sijawapa tena fedha na baada ya kukabidhiwa Binti na Mimba nikapachika biashara ya Mahari ikaishia hapo.Kwa hiyo ulilipa pungufu ya asilimia 10 ya mahari?
Ajabu sisi tumeenda na Milioni moja mzee anakataa na kudai anataka 4 Milioni,hakika sitampelekea hiyo pesa hata kwa fimbo
Pole sana Mzee wangu,hapo Kuna mambo yakujifunza,pia jitahid uwe makini haswa kwenye swala la kimaamuzi maana Kuna mitego wamekupa bila wewe kujua" umeondoka na mwanamke ni ishara ya utayari wako kutoa mahali ambayo wametaka, pia kitendo Cha mwanamke kukulilia na kukushika miguu huyo Kuna jambo la hatari ambalo alishapewa kama onyo na huyo Mzee, pia jitahid sana kutoa mahali japo taratibu ingawaje wamefanya kama kukuadhibu kurudisha garama zao za masomo na kuwadharaulisha Hilo inategemea na Mila zao, pili usipotoa mahali ukiacha mambo ya kishirikina na ikatokea bahati mbaya mwanamke amepatwa na tatizo kubwa (kifo) huyo Mzee anaweza akakuzilia/ kususa na akagomesha wasizike mpaka alipwe mahali! Sasa binafsi naona ni mtego ndiomana walikuwa radhi kuacha uondokenae hvyo kwenye maamuzi jitahid ushirikishe wazee wako na wenyeji wa kiha ili iwe salama kwako!Nimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke kutoka Kigoma tangu 2020, tulikutana chuo, na penzi likakolea haswaa!
Kipindi cha Covid penzi lilinoga zaidi kwani "Working from home" ilifanya muda wote tuwe pamoja, ilikuwa mwendo wa kwenda sokoni kununua mazaga zaga pamoja, tinaweka ndani then kila baada ya mlo ni mnyanduano tu, hatimaye binti akashika mimba!
Baada ya mimba kufikisha miezi minne bibie akaniambia ni bora aende kwao kwanza kwani kubaki tukiwa wawili hatuwezijua complications za mimba, nilikubaliana nae, nikajipiga kwa kadri ya uwezo wangu nikamkatia tiketi na vizawadi kidogo vya wazee akaenda kwao!
Akiwa kwao mawasiliano yetu yalikuwa vizuri kabisa mpaka akajifungua salama salmin, na mimi niliwajibika haswa mpaka dk. ya mwisho, hatimaye tukapata mtoto wa kiume.
Bibie baada ya mtoto kufikisha miezi 6 bila mimi kwenda kujitambulisha akatoa wazo la kurudi kwangu kwani alikuwa amechoka kuishi nyumbani kwao, nikamkaribisha tukaendelea na maisha ya sogea tuishi.
Mwaka jana December, ilitokea msiba kwao akalazimika kwenda msibani, nikamfanyia maandalizi vizuri kabisa, akaondoka.
Amekaa huko tangu December, mpaka juzi nilipoamua kufuata taratibu za kwenda kwao ili tusiendelee kuishi kimya kimya (tufanye kuwa official), nikajiandaa kwa mambo kadhaa kama nilivyokuwa nimeng'atwa sikio na mpenzi wangu.
Nimeanza safari kutoka Dar kwenda Kigoma (kwao), nikiwa nimeambatana na brother wangu wa damu, aisee kwao ni mbali, maana tulitembea siku 2 njiani, tulipofika mjini, safari ya kwenda kwao ikachukua masaa mengine 8, vumbi kali hatari, tulipofika Kijijini kwao tukaambiwa Burundi ni mwendo wa kutembea nusu saa tu.
Brother akaniuliza, "Hivi dogo hukuona wanawake mikoa yote tuliyopita mpaka kuja huku?" Nikamwambia mapenzi yana nguvu bro, sikuwahi kufikiria kama kuna siku ningesafiri umbali namna hii kufuata mwanamke tu. Tulipofika mjini tulitafuta mzee mwenyeji, anayejua mila na desturi za Kiha ili mambo yasiwe magumu.
Basi bwana, tumefika pale tumepokelewa vizuri wakaandaa utaratibu wa mjadala, mshenga akatambulisha na kuanza mazungumzo rasmi, hapo nilikuwa na zawadi ya baba mkwe na mama mkwe, nilinunua tangu Dar kwa upendo kabisa.
Wakataja kiasi cha mahari kuwa wanataka mil. 4.5, hapo tukashtuka kweli, kabla hatujakaa sawa wakataja mkaja wa mama sh. laki saba, jumla wanataka 5.2 Milioni!
Yule mzee tuliyeenda naye akaomba twende nje kwa mazungumzo, akatuuliza kama tulipewa mwongozo na tuliyekwenda kumuoa, nikamjibu ndiyo (alisema mahari kwao haizidi Milioni moja) na mkaja wa mama huwa ina-range kuanzia 100k - 200k, na mimi niliandaa 200k kama mkaja wa mama! Mzee akasema hapa kuna tatizo, huku haijawahi kutokea mahari kubwa kiasi hiki, akasema tutasimamia kwenye hiyo 1M na mkaja wa mama 200k, tukarudi ndani!
Mzee (mshenga) akaanza kuzungumza, kuwa sisi tuna mahari 800k na mkaja wa mama 100k, lakini pia tuna zawadi kwa ajili ya baba na mama, ambazo si sehemu ya mahari, ni zawadi tu ya kijana wetu kwenu, mzee akatoa zile zawadi akaweka mezani.
Mshenga wao akashukuru na kuanza kuzungumzia mahari yetu kuwa angalau tufanye mahari mil.4 mkaja wa mama 500k.
Kabla hajamaliza akasimama baba mkwe, akionyesha kukasirika akasema "Sitaki mjadala wa kitoto hapa, mimi ndiye baba wa x, mkaja wa mama laki 5, mahari yangu nataka Milioni 4, Sitaki mjadala wala kusikia kupunguziana, kwanza unabeba zawadi kutuletea nani amekutuma utununulie, tumekuomba sisi utuletee zawadi zako?"
"Kwanza huyu kijana anadharau sana, tangu mtoto azaliwe hajawahi kufika hapa nyumbani, anaishia kumtumia mwenzake pesa tu, sisi hajawahi kututumia pesa hata mara moja, tumepata msiba hajawahi kuja kutupa pole zaidi ya kupiga visimu vyake tu, sasa mimi nimeshasema mkaja wa mama laki tano, mahari Milioni 4, sitaki mjadala!"
Aisee nilijikuta nimejaa hasira mpaka basi, mshenga wetu akatutaka twende nje, akasema "huyu mzee inaonekana ana lake jambo, tusiingie kwenye mtego wake, iweni wapole, tuondoke salama, watu wa huku ni hatari sana, tukiwa na hasira tunaweza tusirudi salama, hii si dalili nzuri."
Tukajadili tuvyojiandaa pale, mzee akasema muhimu tuanze na mkaja wa mama, tuwawekee hiyo 500k then tutawapa faini za mbuzi mbuzi, na vingine vidogo vidogo, baada ya hapo mahari tuwaambie kuwa tunaenda kuitafuta then mtaangalia wenyewe baada ya kufika nyumbani!
Tuliporudi ndani tukakuta mzee anaonyesha kuwa na hasira hasira tu, kiasi kwamba mshenga wao akawa ameduwaa tu, basi mshenga wetu akaanza kujitetea pale, akaweka mezani Tsh. 500k mkaja wa mama, akawaambia mbuzi watatu wa uchafuzi 300k, sijui koti la mjomba, mara blanketi ya wazee na vikolo kolo vingine kwa Kadri ya taratibu zao, ile pesa tuliyoenda nayo ikawa imekata!
Muda huo wote nina hasira vibaya mno, ila najitahidi kuificha japo mpenzi wangu aligundua kabisa kuwa nimechukia. Tukawaambia hiyo mil. 4 tunaenda kuitafuta, mzee akasema "Mkaitafute muilete hapa, au mutanitumia kwenye simu," tukawaambia sawa.
Muda wa kutoka nikakuta mpenzi wangu ameshabeba mabegi anataka tuondoke wote, nikamwambia hapana unapaswa kubaki nitakuja kuwachukua nikimalizia mahari. Akagoma, akawa analia wakati wote akiwa amenikumbatia, anaomba radhi kwa kilichotokea ila anaomba tuondoke wote, yeye hawezi kubaki kijijini tena. Nikamwambia hapana, unapaswa kubaki mpaka tumalizane na mzee, akagoma kata kata, akawa amepiga magoti huku amekumbatia miguu yangu, machozi yanamtoka tu!
Mzee wake alipotoka akaona mwanaye analia akasema "Kama mnaondoka wote nendeni tu!" Mara mama mkwe akaja na dogo (mtoto wangu), akamshusha nilipokuwa, nikambeba mtoto nikamwambia mama mtoto asimame, bro na mshenga wetu wakaniita pembeni, mshenga akasema tuondoke nao, tukimuacha na wakahisi kuwa kuna dalili za sisi kutorudi, watamuua huyu mtoto.
Basi kishingo upande, tukawakubalia kuondoka nao, mama mkwe akaleta maharage na jogoo akataka tuondoke navyo, nikakataa kuchukua, nikamwambia tutabeba wakati mwingine, akagundua bado nina hasira. Akamuita mtoto wake, akamwambia "Mwambie mumeo amsamehe bure baba yako, amekosea sana, na mimi mama naomba atusamehe tu."
Tukaondoka zetu, kichwani nikiwa nimejaa mawazo mengi mno, kiasi kwamba sikuweza kujua niamue nini. Tumefika Dar lakini moyoni nimejikuta sina tena interest ya kutengeneza undugu na familia ya mpenzi wangu, japo yeye binafsi hana shida, lakini kwa namna tulivyopokelewa na tulivyoondoka, nilijisemea moyoni kwamba sitokaa nirudi Kigoma, wala sitokaa nipeleke hiyo mahari waliyosema.
Nasubiri mwanangu akuekue kidogo nimwambie mama mtoto kwamba hakuna namna naweza kuunganisha undugu na familia yake, japo namhurumia ila ndiyo hivyo tena.
Kweli tembea uone, all the way from Dar to Kigoma, naenda kukutana na aibu tu, anyways.