Nimetumia Dawa zote nilizopewa Kuku wangu wa Layers bado wanamafua makali

Nimetumia Dawa zote nilizopewa Kuku wangu wa Layers bado wanamafua makali

KIKUMI

Member
Joined
Jan 19, 2012
Posts
7
Reaction score
2
Habari wana Jamii, Kwa kifupi nimeanza kufuga Kuku wa Mayai (Layers) ni mgeni kabisa katika suala la ufugaji kuku wangu kwa sasa wana wiki 10 ila kuna Kuku kama 20 kati ya 300 wanatoa machozi hatari, watalaam wanasema ni mafua nimetumia dawa zoote nazopewa na wataalam hakuna chochote.
Kwa kifupi nafuga kwenye cages hivyo uchafu kwao sio rahisi kabisa. Banda lina hewa la kutosha ila bado napata taabu na Mafua.
Wadau kama kuna mtu anaemfahamu mtalaam naomba nipatiwe i will pay consultations kwa sababu najiona naenda kupata hasara. Au wenye uzoefu naombeni ushauri wenu wadau.
 
Ili nikupe ushauri wenye tija.. Embu elezea dawa ulizotumia mpaka sasa na ulizitumia kwa namna gani... Maana katika kutibu hasa mafua yana kanuni zake na namna ambayo mtiririko wa dawa unapaswa kutumika ili kuleta matokeo chanya
 
Hii ndio Shida, Mtu anaweka post, haina Taarifa zozote kwa ukamilifu, kama unajua huwezi kuwepo mtandaoni mda mwingi..weka taarifa kwa ukamilifu ili watu wasikuhoji maswali...
 
Back
Top Bottom