Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
NIMEULIZWA KUHUSU HISTORIA YA BABA WA TAIFA NA UVUTAJI SIGARA, KUSUDIO NINI?
Mtoto...
Nimekutana na picha za vitu vya zamani hapa mtandaoni vitu ambavyo vimenikumbusha historia niijuayo katika vitu hivyo.
Ndipo nikaamua kuwa nitaandika historia hizo kwa nia ya kuweka kumbukumbu na nikaanza na Mwalimu Nyerere na sigara Clipper.
Katika picha hizo kuna picha ya Aspro.
Niliamua baada ya Sigara Clipper niandike makala kuhusu Aspro na historia yake ambayo inawahusu watu watatu muhimu sana katika Afrika ya Mashariki na Kati katika miaka ya 1950 hadi 1960 - Peter Colmore, Mwenda Jean Bosco na Eduardo Massengo.
Katika hawa watu watatu Peter Colmore nikimfahamu vizuri kwanza nikiwa mtoto Dar es Salaam na kisha mtu mzima Nairobi na ndiye aliyenieleza haya ya Aspro.
Hiyo picha ni ya Peter Colmore.
Colmore ndiye aliyemjenga Massengo akawa mwanamuziki mkubwa sana na kupitia kwa Massengo Colmore akamleta Mwenda Jean Bosco Kenya kuja kuitangaza Aspro Afrika ya Mashariki.
"Aspro ni Dawa ya Kweli," lilikuwa tangazo maarufu katika radio zote Afrika ya Mashariki.
Bosco alikuwa pia mwanamuziki mkubwa Congo lakini alikuwa hajafika Afrika ya Mashariki.
Hii ndiyo ilikuwa nia na azma yangu kwa bandiko lile la Baba wa Taifa na Sigara Clipper na nihitimishe na historia ya siku mwaka wa 1961 Ally Sykes alipowachukua Peter Colmore na Eduardo Massengo kuwapeleka nyumbani kwa Nyerere Magomeni kuwatambulisha.
Siku ile ikasadifu kuwa ndiyo siku Patrice Lumumba aliuliwa.
Ziko picha za Mwalimu na Massengo.
Sent using Jamii Forums mobile app