Nimeumia sana na jinsi hali ya kisiasa inavyoendelea hapa nchini

Nimeumia sana na jinsi hali ya kisiasa inavyoendelea hapa nchini

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
1,403
Reaction score
2,546
Nimeumia sana na jinsi hali ya kisiasa inavyoendelea hapa nchini. Nimeumia zaidi kuona viongozi wa dini wanavyosifia serikali hii iliyojaa kila aina ya dhambi na kuacha kukemea mauaji, ukabila na uchama unaoshamili nchini.

Nimeumia sana kuona wasomi wenye elimu ya juu ambao wamesomeshwa kwa kodi za wauza uji na wauza karanga Tsh. 20,000 kwa mwaka na kodi mbalimbali wakisimama kutetea matumbo yao na kuacha haki ikiminywa.

Inaniuma sana kuona katiba ya jamhuri ikikanyangwa na wachache walioshika madaraka ya nchi hii kwa kuiba kura.

Naumia sana kuona jinsi gani nchi hii imekua ni nchi ya kufahamiana yaani kama hujulikani hauli matunda ya nchi yako.

Naumia sana kuona mapato ya serikali yanatumika vibaya kwa miradi isiyokuwa na tija kwa taifa iliyojaa dhuluma na upigaji wa hali ya juu.

WITO: Vijana tuna nguvu hii nchi ni yetu wote. Tupiganie nchi yetu tuliyopewa na Mungu.

Tuachane na hizi dini za kipuuzi zinazoshabikia uvunjifu wa haki. Tusiwape hela zetu kwa kisingizio cha sadaka. Ukitaka kutoa sadaka nenda kwa yatima na wajane ambao wametapakaa kila mahali.
 
Mbona haukuumizwa na wale waliotafuna michango ya wabunge waliochangishwa kwa muda wa miaka 5, pia haukuumizwa na hao hao waliotafuna michango ya wabunge kuchangisha wananchi maskini ktk mikutano yao ya kampeni na kuitafuna mazima, hapo sijazungumzia ruzuku na misaada mingine kutoka kwa wafadhili wao mbali mbali(hapa namaanisha mabeberu)
 
Naumia sana jinsi ninyi wafuasi wa vyama vya upinzaini mnapohamisha maovu ya viongozi wenu kwa viongozi wa Serikali na vyombo vyake.

Hamwoni aibu kutokemea maovu ya viongozi wenu. Ndiyo maana mwaitwa NYUMBU
 
Wewe umechukua hatua gani?
Kama hujachukua hatua nani aanze?
Unafikiri nani atabeba majukumu ya wengine kama sio wewe?

Tusilaumu wengine haliyakuwa tunajificha humu na tu vpn.

Ford, microsoft, amazon n.k zilianzishwa na mtu mmoja.

Sisi humu ni keyboard warriors tu.
 
Ni bora izo ela zinatolewa kwa hiari na utashi wa mtu kwan kama hautaki unawanyima tu,.........ela inayouma sana ni ile tunayoshurutishwa kuilipa km kodi na mwisho wake inakuja kutumika kununua madiwani na wabunge wa upinzani.
Mbona haukuumizwa na wale waliotafuna michango ya wabunge waliochangishwa kwa muda wa miaka 5, pia haukuumizwa na hao hao waliotafuna michango ya wabunge kuchangisha wananchi maskini ktk mikutano yao ya kampeni na kuitafuna mazima, hapo sijazungumzia ruzuku na misaada mingine kutoka kwa wafadhili wao mbali mbali(hapa namaanisha mabeberu)
 
Mbona haukuumizwa na wale waliotafuna michango ya wabunge waliochangishwa kwa muda wa miaka 5, pia haukuumizwa na hao hao waliotafuna michango ya wabunge kuchangisha wananchi maskini ktk mikutano yao ya kampeni na kuitafuna mazima, hapo sijazungumzia ruzuku na misaada mingine kutoka kwa wafadhili wao mbali mbali(hapa namaanisha mabeberu)
Mzalendo wa kweli huumia nchi yake inapoumia na si Chama cha siasa. Majizi na mafisadi hushangilia nchi inapoumia.
 
Hii nchi inatakuwa iwe crushed na vikwazo vikali na mbinyo wa kimataifa tuumie wote hadi tuelewane ile tupate ukombozi wa kweli.
 
Ukombozi wa nchi hii utakuja automatic baada ya wananchi kuchoka hadi kuchakaa!
Waliobaki kusaidia hili ni mabeberu tu
 
Vunga wewe umeumia kwa vingap hata siasa ije kuwa ya pili?

Haya ni mapito wanayajua wenyewe wanasiasa na yatapita tu itakuja zama nyingine kwanza ushawahi kufurahishwa na zama zipi za siasa hapa nchini? Za nyerere au mkapa? Au unafurahishwaga na siasa za nchi za nje tu?

Hebu tulia ulipo usitushike mkono huku subiri zamu yako
 
Mbona haukuumizwa na wale waliotafuna michango ya wabunge waliochangishwa kwa muda wa miaka 5, pia haukuumizwa na hao hao waliotafuna michango ya wabunge kuchangisha wananchi maskini ktk mikutano yao ya kampeni na kuitafuna mazima, hapo sijazungumzia ruzuku na misaada mingine kutoka kwa wafadhili wao mbali mbali(hapa namaanisha mabeberu)
Si muliisha peleka TAKUKURU, vipi tena?
 
UKIPATA sehemu ya kuiba we iba Sana nenepesha familia yako tu
 
Hii nchi inatakuwa iwe crushed na vikwazo vikali na mbinyo wa kimataifa tuumie wote hadi tuelewane ile tupate ukombozi wa kweli.
Havitatokea International community inajitambua siyo nyie leo mnawaita binadamu wenzenu covid19 hamjajitambua bado na mna safari ndefu

Sasa mmechoka kusubiri kesi yenu kule ICC mnataka vikwazo.Nyumbu wa chadema sheeda
 
Naumia sana jinsi ninyi wafuasi wa vyama vya upinzaini mnapohamisha maovu ya viongozi wenu kwa viongozi wa Serikali na vyombo vyake.

Hamwoni aibu kutokemea maovu ya viongozi wenu. Ndiyo maana mwaitwa NYUMBU
Nimecheka kwa nguvu, kilaza katika ubora wako.
 
Back
Top Bottom