Nimeumia sana na jinsi hali ya kisiasa inavyoendelea hapa nchini


The Gang of Three wamehodhi madaraka yote ya kuendesha nchi hii kiasi ambacho katiba haipewi umuhimu tena. Wanachotamka wao ndio katiba na sheria. Sijui Watanzania wote zaidi ya milioni sitini tumepatwa na nini mpaka watu watatu tu wanatupeleka puta!
 
Kama nchi hii laiti ingebahatika kuwapata viongozi wazuri, viongozi wapenda haki, viongozi wenye upendo na utu, viongozi wanaomjua Mungu wa kweli, kila mwanadamu angependa kuishi Tanzania.

Leo Watanzania wanahangaika na kutafuta kwenda mataifa mengine ambayo Mungu hakuyajalie hata 10% ya kilichopo Tanzania. Wema wa Mungu kwa Watanzania umefutwa na watawala wenye roho ya shetani.
 
Kaumizwa na taifa linavyorejeshwa nyuma kula pesa za mbunge ni issue binafsi sisi twaumizwa na jinsi ya utamaduni wa kusigina katiba unakua ndio MTINDO wa wanasiasa wetu tuliowaamini
 
Ahsante !
 
Havitatokea International community inajitambua siyo nyie leo mnawaita binadamu wenzenu covid19 hamjajitambua bado na mna safari ndefu

Sasa mmechoka kusubiri kesi yenu kule ICC mnataka vikwazo.Nyumbu wa chadema sheeda
Mkuu polepole aliwaita wapinzani sawa na Corona, umesahau?
 
Papaa wangu huu ndy ukweli
 
Nimecheka kwa nguvu, kilaza katika ubora wako.
Bora uwe kilaza kuliko kulamba miguu ya kiongozi ambaye kwa kila hali hajiheshimu wala haheshimu binadamu wenzake

Huwa najiuliza sipati jibu, hivi ujasiri mnao uonesha humu JF, nyuma ya "keyboard" kulaumu Serikali, unakwenda wapi dhidi ya genge la wanasiasa uchwara? Ila wananchi wametambua hilo na kuliadhibu hilo genge kwenye sanduku la kura. Ukweli utabaki hivyo na hata ikiwekwa Tume ya Uchaguzi, yenye wajumbe wote watakaoteuliwa na hilo genge, bado wapiga kura wataliadhibu.

Hivi huwa hujiulizi kwa nini viongozi wanakihama chama badala ya kupokea? Lowassa, Sumaye na kundi lao walihamia huko na wote wakatoka. Ni Nyarandu tu ndiye kabaki huko mguu ndani mguu nje. Sasa hilo genge linawafukuza wanawake 19 hodari, kisa tu mahawara wao hawamo kwenye hiyo orodha ya Wagombea wa Viti Maalumu. AIBU
 

Nasema hivi, kilaza katika ubora wako. Na kama ni uchaguzi ule haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi katika box la kura. Kuhusu viongozi kuhama hasa hao uliowataja, ni salama zaidi wao kurudi ccm kwasababu ya mali walizochuma ni za utata mtupu. Kwenye nchi za madictator, ukitaka kubaki salama ni kuwafuata na kuwasujudia, maana hata wahamaji hawasemi wanafuata itikadi, bali iitwayo kasi ya mtu.
 
Mkuu tatizo ni wale waganga 900 Wa ccm kutoka geita,nchi imetulia kama hakuna kilichotokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…