Nimeumizwa sana na Hili la TAMISEMI:

Mungu yupo walimu wenzangu,atafanya tu.Wapuuzeni haya majitu yanayoleta mizaha kwenye mambo ya msingi kama haya.
 
Kama mpaka sasa Leaving certificates za form 4 2013 bado hawajatoa unadhani hawa ni watu makini? Ngoja ukosee mdogo tena jambo dogo tu uone kitakacho fuata watakugombania kama mpira wa kona mpaka ujute kuzaliwa hivi huu si uzembe ulio pitiliza? Mwanafunzi toka amalize shule octoba 2013 mpaka sasa bado hajapewa cheti bado TAMISEMI idara ya Elimu wanakenua meno na kuimba wimbo wa BRN wakati wao wanachapa usingizi
 
Tamisemi sikieni kilio chetu,moro tc tupo takriban watu 50 ambao tuna cfa na hatujapangiwa vituo vya kazi...why lakini??
 
sasa 2ngefanyj?inabidi 2subirie walicho2ahidi,maana walituambia 2andike majina ye2 na 2mefanya hvo sasa cjajua kama walikuwa wanafanya sensa ama vipi hawa tamisemi

Kwa style hii ya uandishi...wanafunzi wanna kazi
 
UALIMU NI KAZI YA LAANA,HATA YESU ALIKUWA MWALIMU HAWAKUMSHUKURU WAYAHUDI KWA UKOMBOZI BALI WALIMSULUBISHA,KUMDHIHAKI,KUMVIKA TAJI LA MIIBA NA HATIMAYE KUMSULUBU MSALABANI!!

Leo TAMISEMI wanakusulubu km WAYAHUDI walinvyomsulubu YESU,wanakudhihaki,hawakupangii ajira na wakikupangangia watakupeleka kijijini,na hata ukipata hiyo ajira kwa taabu km ulivyojisomesha kwa mkopo toka loan bord then ukapewa asilimia ndogo HAUTAPANDA DARAJA KWA MDA STAHIKI,HAUTALIPWA HELA YA LIKIZO,HAUTALIPWA MALIMBIKIZO YAKO,HUTAKUTA MAABARA,MDARASA MABOVU,OFFICE MBOVU NK THEN UTALIPWA MSHAHARA KIDUCHU!!!HIYO NDIYO C.C.M!!!
 
leo mnalalamika ikifika uchaguzi ndio mnakua wa kwanza kukichagua chama cha kijani sasa mnaona hadha hiyo elimu yako inakudhalilisha mtaani,
 
Hata cjui wana lengo gani na sisi kwani Dakawa siko pekee angu , kuna wenzangu ambao hawajapangiwa pia,

Ivi inamaanisha awa tamisemi awana msemaji kuhusu jambo hili coz ukienda pale ofici zao za dar maswali magumuu wanakujibu majibu mepesi
 

St.john's yalitoka majina manne tuu ya wahitimu waliopangiwa shule,hivyo ilibidi waende dodoma chuoni wakafuatilia kwa umoja wao majina yakapelekwa tena na kufuatiliwa na uongozi wa chuo na wanafunzi hadi wakafanikiwa.pole sana endelea kufuatilia na kuwa na subira huenda wanamalizia kukamilisha
 
kiukweli nijambo baya sana mtu usome kwanguvu ilimradi upate pasi lakini chaajabu unakosa ajira,kiukweli inauma sana unaelimu tena ya ualimu alafu unanyanyasika mtaani pale chuo cha ualimu korogwe tupo stashahada 195 tulio kosa ajira mpaka sasa hawa tamisemi wamekaa kimya tuseme wizara kubwa kama hii hawana msemaji!!!???.
 
inawezekana wanachukulia poa tu,wakati sisi tumehangaika miaka yote leo hii unapewa adhabu ya kukaa mtaani bila sababu.
 
hivi kweli hawa jamaa,haya malalamiko yetu wanayaona kweli au tunajisumbua tu,maana na shangaa leo wametoa majina ya walio badilishwa vituo tar 7/4 sisi ndo tumesahaulika kabisaaaaaaaa??!!mh!!.
 
hivi kweli hawa jamaa,haya malalamiko yetu wanayaona kweli au tunajisumbua tu,maana na shangaa leo wametoa majina ya walio badilishwa vituo tar 7/4 sisi ndo tumesahaulika kabisaaaaaaaa??!!mh!!.

Ata mimi nimeona ayo mabadiliko waliyoweka kwenye website yao mi naona ni dharau na dhihaka kwa nini wasiweke na katangazo kuhusu wale waliokosa ajira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…