Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,156
- 10,974
Habari wakuu,
Hapa nilipo nimejaa kitete siyo poa. Yaani hata sielewi, ingawa maamuzi niliyoyachukua nilishauriana na moyo wangu nikaridhika, lakini still nafsi inanisuta.
Nimeuza kiwanja changu cha urithi nilichopewa kwenye mgao wa familia, tena kiwanja kilicho barabarani kabisa. Nilitakiwa kukiuza kwa Tsh. Mil 18 (atleast), lakini nimejikuta nakiuza kwa milioni tano ili ninunue simu ya ndoto yangu kabla haijatoka kwenye chati.[emoji24][emoji24]
Tayari nishafanya yangu. Nimenunua kitu cha Samsung Galaxy Z Fold 4 kwa Mil. 4 na laki 9. Hapa mfukoni nimebaki na laki tu. [emoji24][emoji24] Kiwanja kimeenda. Naombeni mnipe moyo ili nisiugue presha mwenzenu, nafsi inatapatapa maskini[emoji24][emoji24], bora hata ningefungua biashara.
Nilivutiwa na hii simu kwa sababu imekaa kama kitabu, nikiifungua inaungana vioo viwili inakuwa kama ka TV kadogo, kamera safi na hadhi ya kimataifa.
Moyo umejaa kitete, nifanyeje? [emoji24][emoji24]