Nimeuza kiwanja na kununua simu ya ndoto yangu

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,156
Reaction score
10,974
Habari wakuu,

Hapa nilipo nimejaa kitete siyo poa. Yaani hata sielewi, ingawa maamuzi niliyoyachukua nilishauriana na moyo wangu nikaridhika, lakini still nafsi inanisuta.

Nimeuza kiwanja changu cha urithi nilichopewa kwenye mgao wa familia, tena kiwanja kilicho barabarani kabisa. Nilitakiwa kukiuza kwa Tsh. Mil 18 (atleast), lakini nimejikuta nakiuza kwa milioni tano ili ninunue simu ya ndoto yangu kabla haijatoka kwenye chati.[emoji24][emoji24]

Tayari nishafanya yangu. Nimenunua kitu cha Samsung Galaxy Z Fold 4 kwa Mil. 4 na laki 9. Hapa mfukoni nimebaki na laki tu. [emoji24][emoji24] Kiwanja kimeenda. Naombeni mnipe moyo ili nisiugue presha mwenzenu, nafsi inatapatapa maskini[emoji24][emoji24], bora hata ningefungua biashara.

Nilivutiwa na hii simu kwa sababu imekaa kama kitabu, nikiifungua inaungana vioo viwili inakuwa kama ka TV kadogo, kamera safi na hadhi ya kimataifa.

Moyo umejaa kitete, nifanyeje? [emoji24][emoji24]
 
Hivi mnavyo amuaga kutunga story za hovyo huwa mnataka nini!
Je, kuangalia majibu yetu juu ya kukosa kazi kwenu
Je, kutafuta umaarufu JF kwa upumbavu wenu
Je, kuthibitisha tatizo la ajira Tanzania linasababisha ulemavu wa akili
Ama mna maanishaga nn!!??
 
Uza na kingine ununue na tv curve yake Samsung, utanishukuru baadaye ukipenda.
 
Chakurithi si chako, tafuta chako.
 
 

Attachments

  • Screenshot_20221127-141738_Google.jpg
    77.7 KB · Views: 9
Sasa tafuta wa kumuuzia usikie bei utakayoambiwa.
Hapo ndipo utajua kuwa hujui
Sema fresh huko china wenzio wanauza hadi figo kununua iPhone
 
Kuna mtu mmoja humu, watu kama nyie yeye huwaita

"vijana wa hovyo"
Mkuu, nishauri nifanyeje? Ndo kwanza ina siku moja. Kwani nikiirudisha hawawezi kunikubalia? Japo wanikate 50k kama faini? [emoji24][emoji24] Nataka nitejeshe kiwanja mkuu
 
GENTAMYCIME huwaita mapopoma watu kama hawa [emoji23][emoji23]

Samsung zilivyo mbovu ikizingua kidogo tu hela yake imeenda na akimkumbuka marehem aliemwachia kiwanja cha urithi basi roho itamuuma zaidi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu, sema walau neno moja la kunifariji. Yaani nahisi kufa kufa mkuu
 
Aya nenda sasa kwa hao mademu uliodhani ukiwa na simu ya kufunga na kufungua kama kitabu utatomb*
 
Hapana mkuu, sijatunga. Hapa nilipo nishang'ata kucha mpaka vidole vinauma. Kila nikivuta picha namna nikavyowasilisha ujumbe huu kwa wanaukoo nahisi dunia imeniacha gizani

Sijui nitawajibu nini. Sijui niseme kimeibiwa? [emoji24][emoji24]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…