Nimevumilia sana ila leo imebidi niulize, hivi mtu anakupaje msaada wa Trilioni 1.5 wakati nchini kwake kuna watu wanalala nje na kufa njaa?

Nimevumilia sana ila leo imebidi niulize, hivi mtu anakupaje msaada wa Trilioni 1.5 wakati nchini kwake kuna watu wanalala nje na kufa njaa?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Nimekuwa najiuliza sana hili swali bila majibu ya uhakika, hivi haya mataifa yanayojiita donor countries, huwa wanatupa hii misaada kwa misingi na madhumuni yapi hasa?

Na kwanini wanapotupa misaada huwa tunasainishana mikataba ya msaada? hivi huo ni msaada au tunawauzia kitu hadi tusainishane? Whats happening?
 
Unapewa hela ya kuinua sekta ya elimu, kwa mfano, hivyo lazima mkubaliane huo msaada utakuwa na manufaa gani kwenye elimu na jinsi utakavyowafikia walengwa.
 
Kwanini wasiwasaidie kwanza watu wanaolala nje na kufa njaa nchini mwao?, na kwanini wasitufutie madeni badala ya kutupa misaada? makes more sense?
Kutoa msaada kwa mwingine haimaanishi wewe hauna uhitaji wa huo msaada.
 
Kumsaidia au kutoa msaada kwa mdogo apate mtaji wa kufanya biashara baimaanishi wewe huna haja na pesa hizo wala matumizi ya pesa hizo au hauna shida na pesa hizo.

Alafu pia nchi zinazotoa msaada kwa nchi zingine zinajitosheleza sema kuna watu ni madrug addict Tabia mbaya walevi hata ukiwasaidia wanarudia makosa yale yale anaona hata ukitoa pande zingine zinaweza kusaidia vizuri sana kweli kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HAKUNA MISAADA HAPO,

YOTE NI MIKOPO,

NDIYO MAANA DENI LINAPAA KWA KASI YA JET SIYO BOMBARDIER.
 
Urudishe na faida, siyo kile nikichokupa tu.
Haswa. Unapobanwa na shida na ukaenda kumlilia jirani akukopeshe kile kitendo tu cha yeye kukubali kukukopesha bila kujali kama utarudisha na riba juu au bila riba tayari ni msaada kwako. Kwa hiyo wewe mkopaji unaweza kujidai kuwatangazia wanafamilia yako kwamba jirani yako fulani kakupatia "msaada" na ukaepuka kutumia neno "mkopo" ili wanafamilia wasihoji zaidi kuhusu masharti ya mkopo huo na wamwone huyo jirani kwamba ndiye rafiki wa kweli.
 
Mara nyingi misaada yao hua haina tofauti na ile tunayo wasaidia kina Mwajuma kwa kuwanunulia chipsi kuku au nyama choma pamoja na fanta baridi.

Sent from my DUB-LX1 using Tapatalk
 
Kutoa msaada kwa mwingine haimaanishi wewe hauna uhitaji wa huo msaada.
Sasa ipi mantiki ya kumpa mtu msaada wa shs. 100/= huku unambana akulipe deni lako la shs. 5,000/=? badala ya kumpa msaada si umfutie / umpunguzie deni?
 
Mara nyingi misaada yao hua haina tofauti na ile tunayo wasaidia kina Mwajuma kwa kuwanunulia chipsi kuku au nyama choma pamoja na fanta baridi.

Sent from my DUB-LX1 using Tapatalk
Haha, hii mifano ni hai kabisa. Unamlisha Mwajei chips kuku na pepsi ya baridiii, kumbe home wanashindia ugali tembele. Huyo Mwajei lazima kuna malipo atakupa, atake asitake. Huenda Dona kantriz nao wapo kama sisi.
 
Unaweza kumlisha mchepuko chips kuku huku wanao na mkeo wanalala njaa/kula ugali chumvi..kuna kitu utakuwa umekilenga kwa mchepuko na sio kwamba unampa fervor pekee[emoji125][emoji125]

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo sisi Tz ni kama mchepuko anaelishwa burger na pizza huku nyumbani kwao wanashindia ugali tembele, ila baadae mchepuko kuna cha moto anakipata.., sivyo?
 
Back
Top Bottom