Nimevunjika Moyo

Nafikiri umesoma vibaya embu soma upya ili uchangie unazidi kunitia majonzi

kwani siunaweza kurudia kuvitaja vigezo vyenyewe ili kama kuna ulichosahau ukiongeze hapo?
 
Usijali hayo ndo mapenzi,lazima kukubali matokeo,kuacha na kuachika ni njia ya kufungua ukurasa mwingine mpya ambao sometimes unakupeleka kusahau yote yaliyotokea na kufurahia maisha zaidi ya mwanzo.Hisia za mapenzi zinaundwa jinsi unavyounda hisia ndo zitakavyokugharimu,na hisia pia unaweza ukaunda kwa mwingine na kumsahau uliyekuwa naye.
Anapokuacha ndo amekuruhusu uweze kujua ulimwengu mwingine wenye mapenzi matamu,Cha msingi kama we ndo unamakosa jirekebishe na upate funzo.
Enjoy ur day.....usiwaze sana
 


kuambiwa hakuna connection mbona dogo ndugu yangu kuliko yule anayekuambia mna connetion ila siku hizi hakufeel kabisa, hata kupiga simu anasema hawezi.

Tujifunze kukubali na kuipokea hali halisi. Maisha lazima yaende.
 
pole sana mpendwa, usiumie sana, nipm pamoja na picha yako full, we will find some missing connection, tutamuonesha kuwa "jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pepembeni" do it ASAP, POLE SANA
 
Dinnah,

Pole sana!! Shukuru kwamba hamkwenda hatua ya mbali zaidi, shukuru mungu!

Did not you read the siigns on the wall?

mara nyingi sio abrupt!
 
Pole sana Dinnah ndio ukubwa huo.

mshukuru Mungu kwa yeye kuwa na uthubutu wa kukuambia. kubali ukweli na songa mbele yupo atakaekupenda kwa dhati.
 
Sasa huo ni ushauri au ni kuzidi kumvunja moyo?????????? Tuliza akili yako Dinar, mambo kama hayo lazima uyapitie maishani ndio kukua ati!!!!!!!!!! Muombe Mungu, mpe moyo wako atashughulikia swala lako fasta,bora tuu umuamini kuwa atafanya!!!!!!!!!Ubarikiwe!!!!!!!!
 
Pole sana mpendwa usijali hayo ni mapito tu isitoshe mungu analo kusudi lake endelea kumwomba mungu naye atakuongoze mshukuru mungu kwa hilo wala usijali pole sana
 
Mkuu kulikoni tena? yamekuwa hayo? usiombee yakukute tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…