Nimevunjika Moyo

Hata kama wewe ni Muislam, nakushauri msikilize huyu jamaa, japo tega tu sikio usikilize, utapata faraja. Click the following link [video]http://www.joelosteen.com/Broadcast/VideoStreaming/Pages/VideoStreaming.aspx[/video]
Mimi mkristo nimeingia nimefurahi sana ubarikiwe mpendwa
 
Unafikiri nimemchukia! nimefurahi kapata moyo wa ujasiri kuniambia mapema
 
Bishanga karibu senene, nimependa sana comment yako
 
Tatizo sie wanawake rahisi sana kupenda, hata kama mtu alikuwa anadanganya we unaweza anza mpenda ki ukweli hapo ndio inakuwa tabu, thanks post yako imenipa nguvu
 
Ahsante sana michelle kwa ushauri nina amini Mungu anaweza
 
Let it go my dear, wala usiumie sana kuna kitu mungu amekuepushia. Pole sana.
 
Shukuru Mungu jamaa ametamka mwenyewe haoni connection kuliko angeanza kukutenda kwanza kabla hajakutamkia. Inauma zaidi unapovumilia mateso halafu bado mnaishia kuachana. Sioni raha kuachwa lakini nachagua kuachwa kuliko kuacha. Akigundua baadaye kuwa alikokotoa vibaya hesabu zake utakuwa ktk ruling position ya uhusiano wenu na utafurahia zaidi endapo utaamua kuendelea naye.

Umewahi kuwaza; Bahati mbaya ujidhanie humtaki tena jamaa yako, halafu mwaka mmoja baada ya kumwacha ugundue ulifanya kosa kubwa la maisha na sasa unamhitaji kuliko 0xygen? Imagine wakati huo unamkuta jamaa katulia hana haraka na maisha. Unayajua maumivu ya kumwangukia mpenzi wako kumwomba msamaha ili akurejee? Usipate tabu Honey, kwa kuwa unampenda si wewe uliyepoteza mtu bali yeye (kwa ujinga na connection zake) ndo anapoteza mtu anayempenda na kumjali.

Uzuri wa hali yako ni kwamba hata kama mshikaji anao uzuri wa aina gani (kama hujamkosea) hutakaa ujute daima. Hofu yangu ipo kwake. Atakapogundua hicho alichodhania ni connection hakipatikani popote aendapo, atatamani kuwa panya auawe kwa sumu.

Tulia kwanza kabla ya kukimbilia wafuta machozi (rebounds). Baada ya muda wa utulivu utapata mtu utakayempenda na atakayepokea penzi lako kwa moyo wa shukrani. Watu wanasema "Kuwa na uhusiano mzuri si lazima kiwango chenu cha kupenda kilingane". Mmoja anaweza kupenda zaidi na mwenza akalijua hilo, akaliheshimu na kulipokea kwa shukrani. Ukiwakuta watu wa namna hii wanavyothaminiana huwezi kujua ni nani anamzimikia mwenzake zaidi.

 
Dinna pole na shukuru Mungu kwa yote,tulia muombe Mungu akupe mtu sahii.Cheers
 
nashukuru sana sana kwa ushauri mzuri the analyst, yaani umeelezea vizuri mpaka nahisi furaha, najua itaenda itaisha na nitajipa muda sana kwa kuwa najinua sio mtu wa kukurupuka, kwa sasa nitajipa nafasi niendelee na masomo litakalotokea mbele ni Mungu anajua
 

umevunja big time,safi mkuu!
 
pole sana,dinar. .pain come and go,ebu jipe nafasi ya kutafakari jinsi ilivyompendeza MUNGU kukupa uhai bado una nguvu,matatizo mengine ni changamoto tu,maisha ni kama hadithi iliyokwisha andikwa ktk kitabu,baadh ya mambo lazm yatokee kutimiza neno,sema bahati mby imekutokea wewe,jipe nafasi ya kuona kua dunia sio sehemu ya raha na pia yeye atapita na atakuja mwengine best kiasi pale utaona ulivykua unapoteza tym yk.
 
Kwa kuwa unasoma naomba nikuongezee ushauri mwingine. Unapovunjwa moyo ndiyo wakati mzuri zaidi wa kutengeneza GPA bomba. Yale machungu ya "....Poa tu....umeona sikufai siyo?...Mungu atanisaidia.....Nakwambia utanikumbuka...." Kwa maumivu uliyonayo naamini unanielewa vizuri. Basi kipindi hiki ndiyo usome kwa lengo la kulipa kisasi. Miaka ya nyuma yaliwahi kunikuta pia. Bahati mbaya kwa kiasi fulani nilikuwa mkosaji pia. Mdada akapata bwana. Roho iliniuma sana, muda wote tuliokuwa tunaspend naye awali sasa nikawa nautumia kupiga book bila kujali nammiss au la. Thank God ikaniinua kweli kwenye matokeo ya mwisho. Nilivuka salama na yeye na jamaa yake ndiyo wakasambaratika after 2 to 3 years na baadaye zaidi sijui nini kilifuata.

Currently I'm happy with my life doing my own stuff. Tena amini nakwambia ukianza kuchapa book kwa hasira na kuona unavyo-gain utagundua alikuwa nuksi tu akikupotezea muda bure. Usishangae baada ya muda si mrefu atatamani awe wako tena. Usikurupuke kabisa kusema ujaribu kumwoneshea eti una connection na jamaa wengine. Mapenzi ya kufuta machozi huwa hayako makini na mara nyingi yanaweza kuishia kukuumiza zaidi. Mashost kibao wameshauri ujipende mwenyewe na mimi nasisitiza hivyo. "Penzi la dhati kwako litatoka kwako mwenyewe" Mungu akubariki daima.

 
Shukuru Mungu kakuambia mapema kabla hamjafanya commitment zaid kwani ingekutafuna sana kuliko sasa...Amini kwamba huu sio mwisho wa maisha kwani wanaume wapo wengi na huwezi jua Mungu kakuepusha na nini.Piga moyo konde na ufungue moyo wako kwa mahusiano yatakayofuata.
Mungu akubariki na akupe haja ya moyo wako.
 
pole sana Dinnah endelea na maisha yako kama kawaida shukuru ungu hamkufika mbali ingawa hakuna cha afadhali kwenye mapenzi, angalia umeshauriwa vizuri sana huku juu shikilia hayo pia the analyst ameanalize fresh sana soma posts zake kwa makini kila la kheri dear
 
usijali yupo ataujenga moyo wako ulovunjika tena utakuwa moyo imara tu
 

First of all you must thank him for his honesty and decency.
Secondly, you should accept and let the reality sink in...pick up the pieces, then move on. Remember, there's always somebody for everyone. Utampata mwengine may be utampenda zadi ya huyo. Good luck!!
 
Jipende mpaka ukikutana nae aone alikosea, watu wa hivi wameshazoea kuacha, huwezi ukmwandikia mwenzako email kumwaambia huna connection, si kama angekuwa anayosema yanatoka moyoni angekutafuta uso kwa uso, nakusikitikia sana sababu najua unavojisikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…