Nimevutiwa na house girl

Kama kweli umempenda mpe msaada wa kusoma kwanza akiwa hapo hapo kwa rafiki yako na usifanye naye ngono. Ujue ma-housegirl wanatoka kwenye mazingira magumu, na lazima atakupa jibu la ndio. Kwa kifupi housegirls are vulnerable - wanahitaji msaada sana. Ukifanya naye ngono tu kwa sasa bila matunzo kama hao wa class yako unaweza usimtake tena.

Halafu kwanza uelewe maana ya ndoa, pili malengo yako kwenye ndoa. La sivyo utakuwa wa kutamani/ kupenda kila mwanamke hata baada ya kumuoa huyo.
 
Kwanza ukutakiwa kusema umevutiwa na 'housegirl' ilibidi useme umevutiwa na msichana halafu utupe qualities zake ikiwemo hiyo kazi yake. Kwa kuanza na kusema 'housegirl' hata ukimuoa naona kuna uwezekano wa kuendelea kumwita 'housegirl'! Hivi angekuwa ni Accountant, Nurse, Doctor, Lawyer, ungetuambia kuwa umevutiwa na lawyer?
 
...Ndugu yangu mapenzi hayana macho yangekuwa na macho nadhani kusinge-kuwepo na Diforce ...sasa nachokuambia lile wazo lako la kwanza lililokujia mawazoni mwako ndilo sahihi...Elimu ni mambo tuliyakuta tuu hapa duniani na tukazidi kuya-complicate tuu...Kumbuka ya kwamba Adam na Hawa hawakuwahi kwenda Shule au Ibrahimu alimpomdhalisha mjakazi wake haikupangwa hiyo hivyo. Cha msingi umempenda basi mpende kama alivyo (Yakhe ukipenda Boga penda na Maua yake eti) ..Kaa nae ongea nae akikubalia la kwanza hayo mengine yatakuwa matokeo. All the Best Brother and remember that no one has a power to create Love ...Love is the natural thing and its only created by God kwa watu wenye mapenzi ya kweli kama alivyo Bwana wetu Yesu Kristo kwa upendo wake mkuu na mapenzi yake makubwa kwa Binadamu hata akautoa uhai kwa ajili yetu ili mimi na wewe tupate Uzima wa MILELE. JINA LA BWANA LIBARIKIWE AMEN.
 

utamu wa pipi ni mate yako mwenyewe
 

Ndugu yangu Pochi ya Hela...

Hii ni karne ya 21. Na wewe una digrii. Kwa Elimu yako unapaswa kufahamu kuwa: Mapenzi hayana cha Elimu, Umri, Rangi, Dini wala kabila!. Yaani unampenda mtu kwa vigezo vyote halafu kimoja tu cha Elimu unampotezea? OMG....Suppose unampata huyo menye Elimu unayemtaka lakini akawa anagawa kama njugu itakuwaje? Awe hakujali na kukuheshimu, hajui na kwa makusudi hataki kutimiza wajibu wake kama mke. Grow up man!

Kwa mfano wa karibu na wa uhakika ni huu. Baba yangu ana shahada 2 na mama yangu ni mwalimu wa shule ya msingi, hajawahi kukanyaga kidato chochote lakini OMG..... sijawahi kuona ndoa imara kama hii. Mpaka nawaonea wivu hakyanane binti muhamale!

Oa hiyo kitu mazee uiridhishe nafsi na moyo wako...after all maisha ni mafupi sana!:A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up:
 

Kabisa, hata mimi nimemwambia, manake tangu mwanzo ana muona yuko chini asije tu kumnyanyasa kwa hilo huko mbele hata kama atamuendeleza!!
 
ukiona unaanza kujiuliza tu na kupata mtingo wa mawazo kuhusu kumpenda mtu ujue hakufai maana nachojua mimi penzi ni upofu mapungufu uwa hayaonekani na kama wewe umeshayaona na kuingia na wasiwasi ni bora kuachana nae maana utaishi na hilo jakamoyo maisha yako yote. Achana nae
 
Wakuu nimefikiri vya kutosha nikachanganya na mawazo yenu nikaona kuwa nizungumze nae kwanza then nitajua cha kufanya. So far nazungumzia upande wangu tu. Ila kwa dokezo binti ni yatima. Na anaoishi nao wanamchukulia zaidi kama mdogo wao

Kama una nia ya kumuoa basi muoe. Usimchezee na kumuacha kwenye mataa. Kumbuka huyo ni yatima kama unavyosema wee mwenyewe, Mwenyezimungu mtukufu amehusia tuwafanyie hisani mayatima. Kwa hiyo kama utamuoa Mola atakuzidishia baraka, kwani itakuwa kama unamlea. Kumbuka kumuendeleza kielimu. Haikatazwi kumuoa au kuolewa na mfanyakazi wa ndani (house boy/house girl).
Inawezekana huyo ndio mola alokupangia umuoe, huyo wa class yako unayemuongelea utamtafuta na usimpate, au utampata tayari akiwa ameshachakachuliwa saaaaaaaaana!!.
Mchezo wa kuchagua sana utajikuta unachelewa kuoa (au kuolewa kama yule dada yetu mwenye miaka 35 anayetafuta mume).
Oa kaka, oa kaka, oa kaka, oa kaka, tena usichelewe ukaja zini. Kama WALLET yako imefulia JF itakuchangi pesa ya mahari (sio pesa ya kufanya sherehe)
 
Love from the first site?!: toooo theoretical.
 
I wish ingetokea tu natural disaster na mara nikawa nae. Tatizo sijui ni wakati gani wa kusikiliza moyo au akili yangu

Wallet umeongea kitu kimoja muhimu sana, kuwa unaogopa usije kufuata channels zote hizo halafu ukaja kugundua kuwa kumbe binti labda hutaweza kuwa nae... nina mfano kama huo, wakati tuko wadogo tulikuwa na msichana msaidizi wa kazi za ndani (kama unvyoita wewe HG) mmoja, basi akatokea jamaa akajidai anataka kumchumbia, akaja home akajitambulisha kabisa, sasa wakati mama yangu anafanya mipango ya kuwasiliana na wazazi wa yule msichana jamaa akawa kumbe ana chakachua, mara jamaa akamtosa yule binti. You know what happened yule binti akachangayikiwa akataka mpaka kunywa sumu, mara akawa muhuni sana na hakuwa hivyo before, yaani vijana mtaani walitungua mpaka ikawa noma, ikabidi arudishwe kwao, tulikuja kupata taarifa kuwa alikufa kwa ukimwi. Ilinisikitisha sana kwani hakuwa hivyo kabisa na linilea vizuri sana.
Sasa mzee ushauri wangu hapo ni kuwa, labda wewe kiaina mtafute mwenyewe kwa muda wako, yaani isiwekwe rasmi sana kwani na yeye anaweza kujipa hope.. jamaa yako atengeneze mazingira tu kiujanja ili wewe uweze kuongea nae na kumpima.
I hope hiyo itasaidia.
 

nimekupata mkuu. Hata hilo wazo la kumuendeleza akiwa pale, jamaa alitoa wazo kama hilo. But where the hell is that time
 

ilibidi kusema hivyo mkuu maana nami pia mtazamo wa kijamii umeniathiri
 

nimekusoma kaka ila huwezi kujua kama ile ni infatuation tu. Muda unahitajika na nisingependa kuonana nae kwa vigezo vyao kwani viko formal kiasi. Hadi maza haus ampe ruhusa kiaina akijua mie gendaeka nakutana na huyo kigori?
 

mkuu nimekusoma na inategemea na mode yao ya kukutana. Yawezekana walikutana chuo cha ualimu wakiwa level. Then toka hapo mdingi akawa anaongeza vidato huku mama akihangaika na malezi.
 

nimekupata mkuu. Nitalifanyia kazi
 
mkuu nimekusoma na inategemea na mode yao ya kukutana. Yawezekana walikutana chuo cha ualimu wakiwa level. Then toka hapo mdingi akawa anaongeza vidato huku mama akihangaika na malezi.

Hapana mazee! Dingi alikuwa tayari ana degree yake. Akaongeza ya pili ndipo akaona si vema mkewe akawa mama wa nyumbani. Akamfanyia mpango akaenda kusomea ualimu. Mama alisomea ualimu mimi nikiwa na miaka 7! Yaani akiwa tayari ana watoto watatu!

Oa huyo binadamu kama unampenda kwa dhati. Elimu is not a big deal kijana. take it from me! Kwenye ndoa kuna mengi sana zaidi ya elimu. Hapa nazungumzia uzoefu.
 

nimekupata kiongozi. Msisitizo wako una tija
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…