Watanzania wenzangu, hili ni janga kwa Taifa letu, yaani ingekuwa katika nchi za wawajibikaji, leo kawambwa na mulugo wasingekuwa mawaziri kwa kujiudhuru auvinginevyo ungekuta ni baraza zima limejiudhuru. Leo ni siku ya msiba ilistahiri hata bendera zipepee nusu mlingoti. Serikali inastahili kubeba lawama zote katika hili, nafikiri pia matokeo haya yana uhusiano wa karibu na mgomo baridi unaoendelea wa walimu maana serikali inatumia mabavu kushinikiza walimu, wao wanatumia akili zao. Kweli tunakoelekea ni kubaya mno. Nimeishiwa maneno stahili katika hili, ila nimeumia sana na siku yangu haijaend vizuri kabisa.