Nimeyumba kiuchumi. Naombeni mnitajie Guest House za kulala kwa Tsh 4,000 au chini yake

Nimeyumba kiuchumi. Naombeni mnitajie Guest House za kulala kwa Tsh 4,000 au chini yake

Unataka kulala au kula mzigo! Kama ni kulala gest 4000 utaipata wapi huku mabwepande tunalala za 10000;
Ushauri wangu tafta box, nenda kariakoo ongea na walinzi watoe buku 2000 kila siku lala vibarazani tena wakiwa wanakulinda! Kwa mda unakuwa umemeki kiasi cha kutosha
 
Kichwa cha uzi kiko wazi!
Nimepata teteleko la kimaisha upande wa uchumi.
Naombeni mnitajie Nyumba za kulala wageni kwa pesa kiasi cha shilingi elfu nne au chini ya hapo kwa hapa Dar!
Asanteni!
Mwenye kibarua naomba tuwasiliane pia.
Nenda uwanja wa fisi.Hata chini ya bei hiyo utapata.

Lakini jiandae kukuta kopo la mavi na mikojo chini ya uvungu wa kitanda cha teremka tukaze.
 
Guest 4,000 kwa siku ni karibu 120,000 kwa mwezi. 120,000 kwa mwezi unapata ghetto poa kenye umeme maeneo ya uswazi. Wewe jamaa huko vizuri ila tu ujiamini!
Huyu hela kwa ghetto imevuka kiwango cha uswazi... Hapo ni room safi kabisa maeneo yenye afadhali
 
Jamaa atakua anazingua nahisi. Ila kama yupo serious atafute kuna wana uswazi wana maghetto ila hela ya kula hamna hiyo 4000 iwe budget ya msosi wakati wanajipanga na mishe zingine.
Inawezekana asiwe na hela yote kwa mkupuo,labda ana uwezo wa kupata hiyo buku nne kwa siku ndio maana anatafuta sehemu ya kulala akiwa anaendelea kufanya saving labda apange!

Hiyo ya kutafuta washkaji wenye mageto nafikiri ni wazo zuri
 
Guest 4,000 kwa siku ni karibu 120,000 kwa mwezi. 120,000 kwa mwezi unapata ghetto poa kenye umeme maeneo ya uswazi. Wewe jamaa huko vizuri ila tu ujiamini!
Hizo hesabu za mwezi kawapa nani?
Mmekazana kuzidisha utadhani hiyo hela mmenipa. Hela iliyopo inatosha siku 3 au nne. Sasa nyie mmekaza 4,000 x 30. Utadhani hiyo hela mmenipa.
 
Jamaa atakua anazingua nahisi. Ila kama yupo serious atafute kuna wana uswazi wana maghetto ila hela ya kula hamna hiyo 4000 iwe budget ya msosi wakati wanajipanga na mishe zingine.
Atakuwa mzinzi tu kaopoa house girl wa mwenye nyumba
 
Back
Top Bottom