naishi moshi mjini na nimeajiliwa kwa mhindi mmoja, kwa sasa nina miaka 3 nkimsaidia kutunza stoo yake vifaa vya ujenzi. sasa nmejichanga kwa mda wote huu na sasa nimepata tsh milioni 5. mimi nimefikiria ninunue gari aina ya markII niifanye tax. sasa naomba ushauri wenu kuhusu biashara ya tax kwani sina uzoefu nayo. pia kama una uzoefu wa biashara kwa mtaji huo nifungue biashara gani lengo nipate faida ya tsh 20000 kwa sku.