Nimezunguka baadhi ya mitaa sijafanikiwa kupata Sukari Dar, kuna nini kinaendelea?

Nimezunguka baadhi ya mitaa sijafanikiwa kupata Sukari Dar, kuna nini kinaendelea?

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Wazee nimezunguka mitaa kadhaa ya Kawe na Mbezi Beach na maeneo mengine ya karibu na hayo Dar es Salaam, siku mbili hizi kwa ajili ya kutafuta sukari lakini sijafanikiwa kupata kwenye maduka yote niliyoenda.

Kwani hii hali ipo pia mitaani kwenu?

Sukari iko wapi kwani? Au baada ya Serikali kuratibu zoezi la bei elekezi ya sukri ndio sababu ya kupotea sukari mitaani?
 
Nimeona watu wamepanga foleni nje ya duka maeneo ya Mbuyuni (Kinyerezi) nikauliza foleni ni ya nini naambiwa wanauziwa sukari
Imenikumbusha miaka ya nyuma tulipokuwa tukipanga foleni kwenye maduka ya RTC 😀
 
Hii inaonyesha dhahir kwamba wafanya biashara wana nguvu zaidi ya mamlaka
 
Wazee nimezunguka mitaa kadhaa ya Kawe na Mbezi Beach na maeneo mengine ya karibu na hayo Dar es Salaam kwa ajili ya kutafuta sukari lakini sijafanikiwa kupata kwenye maduka yote niliyoenda.

Kwani hii hali ipo pia mitaani kwenu?

Sukari iko wapi kwani? Au baada ya Serikali kuratibu zoezi la bei elekezi ya sukri ndio sababu ya kupotea sukari mitaani?
Mie ipo ,kimara
Kilo 4800....last week
Sahivi itakuwa 5000
 
Back
Top Bottom