Nimfanyeje huyu mwenye nyumba

Michael Ngusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2014
Posts
1,637
Reaction score
463
Jamani naombeni ushauri.

Nilipanga nyumba self, doubleroom, miezi 6 kwa ths 80,000 kila mwezi, mwenye nyumba alisema baada ya wiki 2 umeme na maji vitakuwa vimeingia...hivyo sikuona shaka. Sasa mwezi umeisha na majibu yake ni yale yale tu kwamba ooh nimeshalipia tanesco blah blah blah. Na mimi kazi yangu inategemea umeme 100%, nimepoteza dili kibao mpaka sasa.

Kuna jinsi yoyote sheria inaweza nisaidia? ingawa hatukuandikishana kwenye kikaratasi kuhusu hayo mambo mawili (ujio wa maji na umeme) lakini watu walisikia na nina mashahidi. Maana siwezi kuendelea tena. Nianzie wapi? Itanigharimu vipi?

Asanteni.
 
Hataki. Nimeenda polisi wakasema ati hii ishi inategemea makubaliano, hivyo wakaandika barua ya wito lkn nae hajulikani alipo. SImu yake hapokei.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…