Nimfanyeje mdogo wangu?

Nimfanyeje mdogo wangu?

Zamaulid

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2009
Posts
19,697
Reaction score
15,497
Wakuu,
mimi na mke wangu tulimchukua mtoto wa kike wa shemeji yangu kuishi naye hapa mjini!
juzi wife(shangazi wa binti) ameniambia kuwa mdogo wangu anavinjari na huyo binti ambaye anatuita mjomba!!nimechunguza nimeona ni kweli,je nichukue hatua gani kwa mdogo wangu!na kwa huyo binti je?

natanguliza shukrani
 
Watenganishe....
umemletea mbuzi majani, akiyala utamlaumu?
 
Watenganishe....
umemletea mbuzi majani, akiyala utamlaumu?

tatizo si mbuzi kaletewa majani!kumbuka sisi ni waafrika na tunaishi katika extended family!!
huoni kuwa hawa ni ndugu kwa wanacho kifanya?!
 
tatizo si mbuzi kaletewa majani!kumbuka sisi ni waafrika na tunaishi katika extended family!!
huoni kuwa hawa ni ndugu kwa wanacho kifanya?!
hawa ni ndugu lakini si ndugu wa damu hivyo kulana au kuoana sio issue sema tu kwa sasa inabidi mmoja atenganishwe wasije wakazaa kabla ya muda wao na kukuleteeni tegemezi wengine na kama vp mumpeleke boarding mmoja na muwaeleze live kuwa wanachofanya si kizuri
 
Katika mazingira ya kawaida ni ngumu sana kuwa control watoto wasiousiana wanapokutana katika nyumba moja, nimeishi katika familia , kuna mambo ambayo yalikuwa magumu sana kuzuilika, mfano unapokuwa na housegirl ambaye ni mtoto wa binamu yake baba!!, huyo anakuwa halali, Ni ngumu sana kuishi na mtoto wa kike na kiume kama hawahusiani katika nyumba moja kwa usalama!!, Angalia lengo la kuishi na hao vijana pamoja,Ni shule?kazi? ni nini hasa? Kama unataka kumsaidia mdogo wako angalia ni namna gani unaweza kumsaidia bila kukaa nyumbani kwako! Hata huyo binti pia. Naishi na wadogo zangu, wa kike na kiume, wa kiume yuko boarding anakuja likizo tu,wa kike amemaliza Form six anasubiri kuingia chuo. Nimelazimika kuwaangalia baada ya kuona kuwa nikiiwaacha kwenye nyumba ya Familia imejaa wasela na hakuna maadili.
Kuna madogo wengine wawili wanaishi kibachelor , watacopy tabia isiyofaa na sikutaka wawe free kama wale wakubwa wenye kazi zao. Hivyo nikawachukua.Lakini ninawaangalia sana, niko serious na wanalijua hilo. Marafiki wa ovyoovyo hakuna nyumbani, kutoka ni kwa mpangilio.Nje ya nyumbani kwangu wako free, ndani ya nyumba yangu wapo chini ya sheria. PERIOD.

Angalia kwanini unaishi na hao ndugu kwanza.
 
tatizo si mbuzi kaletewa majani!kumbuka sisi ni waafrika na tunaishi katika extended family!!
huoni kuwa hawa ni ndugu kwa wanacho kifanya?!

Umeshaongea nao kuhusu hilo? au umewachunguza tu bila wao kujua?
 
Wakuu,
mimi na mke wangu tulimchukua mtoto wa kike wa shemeji yangu kuishi naye hapa mjini!
juzi wife(shangazi wa binti) ameniambia kuwa mdogo wangu anavinjari na huyo binti ambaye anatuita mjomba!!nimechunguza nimeona ni kweli,je nichukue hatua gani kwa mdogo wangu!na kwa huyo binti je?

natanguliza shukrani

Sijakuelewa vizuri huyo binti undugu upo kwako ama kwa wife wako!!!

Kama undungu uko kwa wife wako na anamuita shangazi basi sio mbaya kwa mdogo wako kula maana hapo hakuna undugu wa damu na huyo binti na kama ni ndugu kwa upande wako inategemea na makabila maana kuna makabila mengine wanaowana mabidamu (binamu nyama ya hamu)

Hatua za kuchukua ni kutochukua hatua yeyote. kama umri wao unadhani ni watu wazima. mkeo amkumbushe binti na wewe umkumbushe kijana juu ya maswala ya ngono salama.

Baada ya muda yataisha tu. si unajua mpaka kuja kuoa au kuolewa au lupata mpenzi wa kudumu watsani watu wanakuwa wamepita kwenye relation si chini ya tano
 
Wakuu,
mimi na mke wangu tulimchukua mtoto wa kike wa shemeji yangu kuishi naye hapa mjini!
juzi wife(shangazi wa binti) ameniambia kuwa mdogo wangu anavinjari na huyo binti ambaye anatuita mjomba!!nimechunguza nimeona ni kweli,je nichukue hatua gani kwa mdogo wangu!na kwa huyo binti je?

natanguliza shukrani

Wafungishe ndoa...:glasses-nerdy:
 
Wakuu,
mimi na mke wangu tulimchukua mtoto wa kike wa shemeji yangu kuishi naye hapa mjini!
juzi wife(shangazi wa binti) ameniambia kuwa mdogo wangu anavinjari na huyo binti ambaye anatuita mjomba!!nimechunguza nimeona ni kweli,je nichukue hatua gani kwa mdogo wangu!na kwa huyo binti je?

natanguliza shukrani

Mrudishe kwao huyo niliyem highlight kwa red color
 
Kama kaanza kwa binamu, angalia asimalizie kwa shemejie, simba akionja nyama ya mtu ni baraa!
 
Hatua za kuchukua ni kutochukua hatua yeyote. kama umri wao unadhani ni watu wazima. mkeo amkumbushe binti na wewe umkumbushe kijana juu ya maswala ya ngono salama.

Baada ya muda yataisha tu. si unajua mpaka kuja kuoa au kuolewa au lupata mpenzi wa kudumu watsani watu wanakuwa wamepita kwenye relation si chini ya tano

Mtanzania umeweka point muhimu mbele yetu!!!

Naongezea ...

1. Hakuna haja ya jamaa kumuogopa Mdogo wake wala huyo Binti! .... Na kuwafukuza au kuwa tenganisha.... Huo Ni woga na kutojiamini ..na nikushindwa malezi..!

2. Face them!! Show your maturity on that issue kwa dhati bila papara...onyesha ambavyo umepitia vituka karibu na hivyo na wape mwanga!! Labda kama huna huo uwezo!! lakini take your time waelimishe both side of what they are doing... hujafanya hivyo na kuona how it will work and its impact ..alafu unataka kuwatosa ..bording..au arudishwe kwao etc ...alafu huko who will take care of what you failed to manage..!

3. Baada ya kufanya wajibu wako ..bila kuukimbia wala kuukwepa ...then tuletee majibu ..kuonyesha imeshindikana au imewezekana...and we will make onather comments!! Nakutakia malezi mema mkuu...!! Ndio kukuwa huko!! kuna watu walikuhudumia vijambo kama hivyo hadi kufikia hapo ulipo!! Sasa ka umri kamekuletea hayo ujionee mwenye we na upasue kichwa..!!
 
Safi Saaana Jamaa anaonesha udume wake,sasa kazi kwako na wewe kuonesha U Baba wako ndani ya familia unayoimiliki
 
Back
Top Bottom