Katika mazingira ya kawaida ni ngumu sana kuwa control watoto wasiousiana wanapokutana katika nyumba moja, nimeishi katika familia , kuna mambo ambayo yalikuwa magumu sana kuzuilika, mfano unapokuwa na housegirl ambaye ni mtoto wa binamu yake baba!!, huyo anakuwa halali, Ni ngumu sana kuishi na mtoto wa kike na kiume kama hawahusiani katika nyumba moja kwa usalama!!, Angalia lengo la kuishi na hao vijana pamoja,Ni shule?kazi? ni nini hasa? Kama unataka kumsaidia mdogo wako angalia ni namna gani unaweza kumsaidia bila kukaa nyumbani kwako! Hata huyo binti pia. Naishi na wadogo zangu, wa kike na kiume, wa kiume yuko boarding anakuja likizo tu,wa kike amemaliza Form six anasubiri kuingia chuo. Nimelazimika kuwaangalia baada ya kuona kuwa nikiiwaacha kwenye nyumba ya Familia imejaa wasela na hakuna maadili.
Kuna madogo wengine wawili wanaishi kibachelor , watacopy tabia isiyofaa na sikutaka wawe free kama wale wakubwa wenye kazi zao. Hivyo nikawachukua.Lakini ninawaangalia sana, niko serious na wanalijua hilo. Marafiki wa ovyoovyo hakuna nyumbani, kutoka ni kwa mpangilio.Nje ya nyumbani kwangu wako free, ndani ya nyumba yangu wapo chini ya sheria. PERIOD.
Angalia kwanini unaishi na hao ndugu kwanza.