Nimjibu nini binti wa aina hii.

mbona michango mingi hapa inasema amrudishe,jamani where is the love????:wink2:
 

Hahaa haaa Pauline jamani, mdogo wangu hua hana mpango nae kabisa, sijui alienda kufanya nini, ni swali ambalo tunajiuliza mpaka sasa wote. Napia sijui alivyotoka na mabegi alipeleka wapi na alirudi kwetu kufanya nini. Na muhurumia pia ila nataka ajifunze kidogo.
 
Mrudishe tu kwao.
Halafu hawa watu sijui kwanini huwa wanajisahau!
Ukiishi nae vizuri atataka yeye ndio atawale nyumba. Kazi kweli kweli.

Kinacho nishangaza ukikaa nao vizuri ndo wanakudharau, kule wanako teswa ndo wanadumu.
 
Kinacho nishangaza ukikaa nao vizuri ndo wanakudharau, kule wanako teswa ndo wanadumu.

Kweli kabisa....Hawa wahudumu hata hawaeleweki. Ukienda kwa waarabu na wahindi...wanafanyakazi nyigni sana na wanakaaa muda mrefu hadi migongo inapinda...Labda kwa kuwa wanalazimishwa kunywa chai zao kwenye vikombe vidogo kama vifuniko vya bia kabla ya kuanza kazi.

Binadamu hawana jema...Achana na huruma. Rudisha binti kwa ndugu zake.
 
Utaumiza kichwa bure,hg akishaanza kuleta nyoka nyoka ujue hamna k2 hapo mrudishe yasije yakakukuta makubwa
 

Hahaaa Babu lao, hajakatazwa kupata huduma kama atajali na kaziake, hujawahi kujiuliza kwa nini ma house maid wakianza kupata huduma na kazi hua wanaacha? Mbona sisi tusiache kazi maofisini kwa sababu ya huduma? Haha haaa, halafu mdogo wangu hamchakachui kabisa, yeye ana mipango yake mingine nadhani.
 

Na mi nimefikiri hilo la wa vulana kumdanganya, kwani hata yule kijana wa kwenye maziwa ameacha kazi jana, na nimara nyingi nikitoka job hua nawakuta getini wanaongea, kisingizio yule kaka kamsaidia kuleta maziwa, wakati anatakiwa aendee asubuhi. Jibu: kuhusu mdogo wangu nina uhakika hachakachui kwani yeye anarudi jioni na hua anaondoka mapema sana, afu hua hana mpango nae kabisaa, hata asubuhi hakumuona kwani alikua amelala na mi nilikua nikifanya usafi.
 
Dah wafanyakazi wa nyumbani hua wanachosha wakati mwingine!!!
Ukishaona hivyo jua kuna mtu anamjaza kichwa mahala and there is no telling ni mtu wa aina gani!!
Bora umrudishe kwao mapema kabla hujapishana na pick up ikitokea nyumbani kwako!!!!

Mh ukweli inawezekana pia, ila lizzy kumbuka hata kusoma hakijui, halafu haijui dar kwani hata outing nimpaka tukitoka wote pamoja ndo tunamchukua, ila unalosema ni kweli, yaweza kua ashapata walimu.
 

Hahaaa, na hilo la simu, yani chumbani kwake kumepakana na kwangu, yani utamsikia anaongea mpaka unapitiwa na usingizi, wachumba kibao kila mtu anampa namba, kasheshe kabisa.
 
mbona michango mingi hapa inasema amrudishe,jamani where is the love????:wink2:

Jamani una huruma eeeh, mwenzio nawaza sijui yuko wapi? Au sijui ndo kwa wamakonde mungu wangu.
 
Miye nakuomba umsamehe lakini umwangalie nyendo zake za kila siku kwa karibu sana kuhakikisha anafuata mstari unaoutaka wewe, ukigundua tu kwamba bado ana vijimambo vyake basi ni bora tu umpoteze. Tafadhali msamehe labda samahani yake ni kweli kabisa inatoka moyoni, lakini kabla ya kumsamehe umsomee risala iliyokamilika ili aulewe msimamo wako.
Happy - Leona Lewis | Music Video | VEVO
 

Duh, sijui warabu na waindi huwa wanatumia mbinu gani kuwa zubaisha, nakuwafanya wasahau kwao kabisaa.
 
Mh ukweli inawezekana pia, ila lizzy kumbuka hata kusoma hakijui, halafu haijui dar kwani hata outing nimpaka tukitoka wote pamoja ndo tunamchukua, ila unalosema ni kweli, yaweza kua ashapata walimu.

Walimu wako wengi.....hata wamama wa jirani!!!Zaidi ya wafanyakazi wetu watatu wamewahi kua wanachukua vitu vya ndani kupeleka kwa majirani!!!
Kwasababu hajasoma jua ni mwepesi sana kudanganyika!!Akiambiwa hapo unanyanyaswa tu mi ntakuoa unadhani atakataa???Au akiulizwa ndani kuna nini na nini unadhani ataacha kusema???Kutokua kwake na elimu kusikufanye udhani hawezi kufanya chochote!!!Kua mwangalifu!!!
Sisi tuliwahi kuchongewa majambazi japo ilikua na mfanyakazi wa kiume ila huwezi kuamini yule kaka alivyokua anasaidiwa.....kama ndugu vile!!!!
 
Hawa wasichana bana ukitaka akae sana usiweke mazoea sana nae mfanye rafiki mliipe kwa wakati mpe zawadi ikibidi ila mpe sheria unazotaka, na ukiona kakosea mseme kwa ukali kama unamsema mdogo wako, na baada ya hilo sahau endelea kuongea nae vizuri kama kawaida. mimi nishaona na inafanya kazi. unaweka sheria kama vile kufunga tv saa tatu au nne week end. hiyo ni nyumba yako na kila mtu anayeishi chini ya dari la nyumba yako lazima afuate sheria yako hapo utaishi kwa amani na upendo.
 

DC Umenipa ukweli ndugu yangu, leo ungeona wenyewe, tumegawana kazi na tukazifanya mapema tumemaliza na msosi wa moja kwa moja bila shida. Ila ulosema ni kweli hata tukipata msichana mwingine itabidi tufanye utaratibu huo wa Tv no.
 

Ni kweli ndugu yangu. Hata wewe mwenyewe huwezi kuangalia TV muda wote na huwezi kufanya kila kitu kwa sababu ya mazingira. Sasa inakuwaje watu wanawapa ndugu na wafanyakazi uhuru usio na mipaka? Inabidi kila familia iwe na sheri na wakuu wa kaya wawe wa kwanza kuzifuata. Hapo heshima lazima itakuwepo.
DC Umenipa ukweli ndugu yangu, leo ungeona wenyewe, tumegawana kazi na tukazifanya mapema tumemaliza na msosi wa moja kwa moja bila shida. Ila ulosema ni kweli hata tukipata msichana mwingine itabidi tufanye utaratibu huo wa Tv no.

Umeona sasa Mamushika...Hawa wasichana wanajiona kama vile kazi za nyumbani wao tu ndio wanaziweza. Kwangu huwa hakuna kuremba remba. Wakileta nyodo tunatimua na kufanya kazi wenyewe.
 
Mamushka usirudi nyuma, wewe umetoa gari unamfata umbembeleze arudi yeye hataki, pili ameondoka bila hata kukuaga meaning kutoroka hakutakii mema sasa kama sasa ivi asinge hata piga simu huko mwanza ndugu zake wangekuelewa? hilo ni bomu lililoisha muda wake liteketeze kabla halijakulipukia kama yale mabomu ya gongo lamboto. Muambie arudi ila umuandalie safari yake ya kwenda mwanza by the way nategemea umeshawapigia ndugu zake wa mwanza simu kuwaeleza yote yaliyojiri ili wasikulaumu. Ila tafuta mwingine lazima kuna kitu kinamrudisha hawa watu hawafai bwana. Wanaotetea nakusema where is love, hayajawakuta jamani, hawa ni nyoka wenye sumu kali sana wakishajua mji na kupata vidume vinavyowachakachua nyumba nzima anawazarau.

Note: Utayakumbuka haya siku moja mrudishe halafu after one month utaniambia,!:hand:
 
Usimfukuze mrudishe nyumbani na wala usiwe na wasiwasi nae...unaambiwa siku za mwizi ni arobani...so kama kuna deal anacheza na humo ndani utagundua tu...pia sasa hivi cha kufanya jaribu kufatilia humo ndani na ujue kitu gani ambacho hakipo maana huwezi jua mule kwenye mabegi alibeba nini siajabu kashachukua vya kuchukua amepeleka mahali sasa anajifanya anataka kurudi hamna lolote....so jaribu kucheck kwanza ila usimfukuze....
 
Mi nakushauri muache aje home kwanza ikisha muangalie taratibu nyendo zake,pia muonye sana,mtafutie shule asome,huyo mtoto ni masikini ikisha ni yatima,mpe last chance,japokuwa umemchukua kwa kufanya kazi lakini mpeleke shule atakusaidia kwa wema wako,mtu akitenda baya mtende wema,isitoshe unae muda mrefu,pengine umemchukua akiwa gharika dogo sasa ni mwari, malipo yako kwa mungu,mungu anasamehe na wewe samehe pia,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…