Dah!!! Tunachokosea sisi wanadamu tuliopewa Neema ya kuwa na watu wakutusaidia kazi za nyumbani wakati sisi tukiwa na majukumu mengine, ni vile tunavyowachukulia kama watu wasiohitaji kufikiriwa na kusamehewa pale wanapokosea. Ni vile tunawafanya wao ni wakubwa wanajua kufikiria na wakidanganywa kwa nini wamedanganywa wakati hata wewe mtu mzima unaweza ukadanganywa na mwanaume na ukaingia mkenge vile vile.
Kesi yako dada, unasema huyu binti ulimchukua mdogo, ndo anakuwa hivo.....huna muda wa kutosha kukaa naye, yawezekana hujawahi hata kumpa ushauri na kumfundisha jinsi dunia inavyokwenda....ulikuwa ukimuona anakosea unampotezea....sasa angejua je kama anachofanya anakosea??? Ukisema ajue kile kilichomleta unamuonea kama hujamkumbusha na kumpa elimu ya kufikiria maisha na jinsi ya kupangilia mambo. Kuangalia TV sio dhambi lkn afanye kila kitu kwa wakati,, umemfundisha??? Na kama amedanganywa na vijana wa kiume, sio kosa lake pia ni kama wewe na mm tulivyo/tunavyoweza kudanganywa pia...umewahi kumpa Elimu juu ya hilo??? Ulimuona anabadilika ukampotezea si ndio....kwa nini unamlaumu. Kwa nn unataka mtoto wa miaka 18 hata 20 anayekaa ndani kwako na vyombo na TV na viti awe na akili ya kujua dunia inavyokwenda.
Unataka nani amwambie? Viti na meza na makochi na vyombo anavyoshinda navyo na moto na nguo anazofua ndo zimfundishe???? Tuwe na huruma na upendo kwa hawa watu. Sisi ndio tunaowaharibu. Umeongea naye usiku mmoja tu, unataka awe amebadilika??
Sisi tumewahi kukaa na house maid miaka kumi, mpaka akaolewa akiwa kwetu. Sio kwamba alikuwa hakosei ila mama alikuwa anamlea na kumfundisha kama alivyokuwa anatufanyia sisi. Tena yeye alikuwa hachapwi lakini sisi tulikuwa tunachapwa kama nini. Hakuna kusema huyu ni house girl na ukisikika unasema huyu ni mfanyakazi wetu unachapwa....tulikuwa tunamwita dada... Na ametoka ana maisha yake mazuri tu,ana akili za maendeleo ni mmwera lkn ukimsikiliza utadhani mchagga alivyokuwa na mawazo ya kutafuta pesa....amekuwa ni zaidi ya ndugu yetu. Fanya sehemu yako, ukishindwa kitaeleweka na utakuwa umenawa mikono.
Na hata huyu tuliye naye naye sasa hivi, anafanya vizuri kuliko hata mdogo angu tuliyezaliwa naye na ana umri sawa na yeye. Yani utampenda, anafundishika, na nina muda wa kuongea naye, kila jpili mfano tukitoka kanisani, namwambia umuhimu wa kumtegemea Mungu...na muonya pale anapokosea na anaomba msamaha. Hawezi kuwa sawa asilimia mia moja, lkn anopokosea najua kabisa hata mm nakosea kwa hiyo namfundisha na kumrejesha kwa upendo. Yani namshukuru Mungu manake hata majirani wanaona wivu wanatamani wamshawishi lkn kwa jinsi nilivyomweka karibu, anakuja kunambia fulani kanambia hivi na hivi. Halafu nampa shule mapema kuhusu hilo.
SIO UNAPOTEZEA.
JPIL NJEMA!!