Diwani hajawahi kuwa TISS kablaUshushu hauitaji udaktari wala uphamacia mkuu,
Upelelezi ni taluuma mtambuka , hapo wako wale wanaowekwa kwenye taaluma hiyohiyo mfano police kuna police ambao ni tiss kama alivyokuwa Diwan Athumani, na wanajeshi ambao ni tiss pia,
lakini sio lazima kila tiss apelekwe kwenye taaluma aliyosomea haiko hivyo mkuu, unaweza kumkuta popote.
Kama watafiti wenyewe ndiyo hawa walitengeneza hii kachumbari bora serekali isitoe fedha aiseeTatizo ambalo lipo kwenye taasisi zetu za utafiti ni low funding, serikali inatakiwa itoe 6% ya GDP iende kwenye utafiti, badala yake pesa kibao wanapewa viongozi wa kisiasa na kiserikali kama posho, gari, marupurupu, mishahara mfano wale wagonga meza. Badala yake watafiti wanabaki wakiwa hawana la kufanya hata kama ana kitu cha kufanyia utafiti, anakaa ofisini na kupiga miayo. Kwenye nchi zilizoendelea mbali na serikali sekta binafsi inajihusisha na ku-fund research ambazo zitawasaidia kupata products, mfano kwenye upande wa sekta ya afya, madawa, chanjo na vifaa tiba. Mfano, kampuni la madawa linaweza kutoa hadi billions of money kwenye taasisi ya utafiti, mfano chuo kikuu kwa ajili ya kupata aina mpya ya dawa, chanjo au technology ambayo watapata hati miliki na kuuza kwa faida kubwa....
Duh unaweza kukuta huyu ni reseacherYaani!!! nifanye refference ya mutu ya kijicho??
nenda kazini upesi!! acha sisi tule ruzuku tuliobarikiwa matunda ya nchi!!! tunawatafutia dawa! tulieni!! mtainywa tu!
National Institute for Medical Research .Samahani nndugu Ralph Tyler kwa faida yangu na wengine NIMR kirefu chake nini?
Wacha watu wapewe kazi waweze kulipa loan board1. Miaka yote zaidi ya 40 ya uwepo wa NIMR, wameongeza nini katika ufahamu wa mambo ya tiba Tanzania? Ni utafiti gani waliowahi kuufanya ukaleta tija katika kupunguza au kuondoa tatizo lolote la kiafya? Jibu ni zero.
2. Hivi kuna dawa yoyote sokoni (dawa ya maana yenye viwango stahiki, na siyo ile michanganyiko ya pilipili kichaa na tangawizi waliyoiga kutoka kwa waganga wa kienyeji) au vifaatiba hospitalini au maarifa mapya yoyote ya tiba yaliyowahi kugunduliwa na NIMR? Jibu ni hakuna.
3. Nina jamaa zangu nimesoma nao History na English pale Mlimani, eti nao wanafanya kazi NIMR wananiambia wanaitwa "Research Scientist". Hiki ni kituko! Scientist wa history, English, Kiswahili, sociology na Political Science anafanya nini kwenye MEDICAL research? Ingekuwa HEALTH research ningewaelewa kwa kuwa afya ni suala mtambuka lenye mambo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yanayoathiri afya, lakini medical research ni mambo ya maabara, madawa, mawodini huko wanakotibiwa wagonjwa, operations mpya mpya kama hizi za moyo na figo nk. Tunasikia huko Jakaya Kikwete institute, Benjamin Mkapa Hospital na hata MOI wakifanya innovations mpya mpya, lakini mchango wa NIMR kwenye hizi innovations uko wapi?
4. Mkurugenzi wa NIMR ni profesa wa Marine Biology. Hii ndiyo medical research? Hakuna medical researcher nchi hii mwenye sifa ya kuwa mkurugenzi wa NIMR? Sasa marine biologist na medical research wapi na wapi? Ndio chanzo cha kwenda kudesa michanganyiko ya waganga wa kienyeji na kutuambia ni dawa za korona!
5. Kwa ujumla NIMR ni kimeo, haina faida kwa nchi, ifutwe tu.
Naam, ni upumbavu mkubwa kuwa na NIMR kwa mfumo wa sasa.1. Miaka yote zaidi ya 40 ya uwepo wa NIMR, wameongeza nini katika ufahamu wa mambo ya tiba Tanzania? Ni utafiti gani waliowahi kuufanya ukaleta tija katika kupunguza au kuondoa tatizo lolote la kiafya? Jibu ni zero.
2. Hivi kuna dawa yoyote sokoni (dawa ya maana yenye viwango stahiki, na siyo ile michanganyiko ya pilipili kichaa na tangawizi waliyoiga kutoka kwa waganga wa kienyeji) au vifaatiba hospitalini au maarifa mapya yoyote ya tiba yaliyowahi kugunduliwa na NIMR? Jibu ni hakuna.
3. Nina jamaa zangu nimesoma nao History na English pale Mlimani, eti nao wanafanya kazi NIMR wananiambia wanaitwa "Research Scientist". Hiki ni kituko! Scientist wa history, English, Kiswahili, sociology na Political Science anafanya nini kwenye MEDICAL research? Ingekuwa HEALTH research ningewaelewa kwa kuwa afya ni suala mtambuka lenye mambo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yanayoathiri afya, lakini medical research ni mambo ya maabara, madawa, mawodini huko wanakotibiwa wagonjwa, operations mpya mpya kama hizi za moyo na figo nk. Tunasikia huko Jakaya Kikwete institute, Benjamin Mkapa Hospital na hata MOI wakifanya innovations mpya mpya, lakini mchango wa NIMR kwenye hizi innovations uko wapi?
4. Mkurugenzi wa NIMR ni profesa wa Marine Biology. Hii ndiyo medical research? Hakuna medical researcher nchi hii mwenye sifa ya kuwa mkurugenzi wa NIMR? Sasa marine biologist na medical research wapi na wapi? Ndio chanzo cha kwenda kudesa michanganyiko ya waganga wa kienyeji na kutuambia ni dawa za korona!
5. Kwa ujumla NIMR ni kimeo, haina faida kwa nchi, ifutwe tu.
NIMR ni upumbavu. Ifutwe.Exactly. Nimeona mahojiano kwenye TV na mkurugenzi mmojawapo (siyo mkurugenzi mkuu Prof Mgaya), akasema wanafanya research kwa kutegemea grants ambazo watoaji wa grants hizo ambao ni mataifa ya nje ndio wanaoamua research agenda. Kwa hiyo tuna taasisi ya utafiti wa tiba (ndiyo tafsiri ya institute of medical research, ingawa wenyewe wanaita taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu) ambayo haina uwezo wa kuendesha research agenda zake. Matokeo yake imejaza "scientists" wasiokuwa wa tiba kwenye ranks zake: sociologists, politicians, linguists, historians, marine biologists na wengine wa hivyo, eti hawa ndiyo waendeshe agenda za medical research! Hii siyo dharau?
Ndiyo maana tafiti zake ni kichefuchefu kitupu, hata sisi tuliosoma "ungwini" tunawashangaa.
yes i was talking about funding agencies. but then hata ukiielekeza serikali.. pesa watatoa?Unaanzishaje research bila pesa? Wadau wa kusupport ninaamini unamaanisha funding agencies. Kama ni hao, basi wao hucirculate calls for funding opportunity, na zinakuwa zinasema wanataka kutoa pesa kwenye tafiti za uelekeo fulani. Ni jukumu lako kupima interests zako na competency individually au kitaasisi kisha kupambana na applicants wengine duniani au nchini au kwenye ukanda kulingana na scope. Kumbuka hapo idea ya proposal utakayoshindsnisha lazima iwiane na vigezo wenye fedha walivyotoa. Kama mkiona havifai, hamlazimishwi ku apply.
Kifupi, iambieni serikali na wadau wengine wawekeze kwenye tafiti za kipaumbele badala ya kutaka tu NIMR ifutwe.
Mkuu wa Tiss ni nani mkuu?!Diwani hajawahi kuwa TISS kabla
Ndio nashangaa!
Dah!! Mkuu dogo ana maudhi sana watu wale, wanakesha ili yeye awe salama wameapa kufanya hivo!! kazi ile ina mateso sana!Duh unaweza kukuta huyu ni reseacher
Teeh!! teeh! teeh! Babu sikiliza USA ni wazungu tu!! ndo wenye nchi kila kitu ni chao!! hkn mwingine na hata nyanyuka zaidi yao!! hata Obama ni mzungu yule aliandaliwa maksudi wewe!!Wewe kweli nutcase, unafikiri Marekani ni wazungu tu! Mmekaririshwa propoganda mpaka vichwa vimebaki kama mifuko ya kubeba meno tu.
Haya waangalie Mugabe, Kagame, M7 ,Gaddafi na Kinjikitile.
Hizo Styles zenu za wakina Kinjekitile zingekuwa zinawachanganya maadui mngebaki mafukara miaka 60 baada ya uhuru huku hao "wazungu" wakijichotea mali tu.
Hujui unachokiongea. Unadhani research Institutions zote duniani zimegundua hayo uliyoyasema. Lakini zime advance knowledge for betterment of human life/health in one way or another.........Kwa vile umejaa chuki, basi huwezi kuona any positive output from NIMR. Ngoja wale per diem safiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, roho ikutange ufe na pressure ya kupanda na kushuka!Ok, clarify.
Kwahiyo hizo ndizo kazi NIMR imefanya tangu 1980?
Jibu hoja kwa hoja, acha kulalama
- Hakuna tangible product waliyogundua ikaingia kwenye soko la tiba
- Hakuna medical procedure mpya waliyoigundua ikaingia kwenye mfumo wa tiba kwenye mahospitali yetu
- Hakuna changamoto ya tiba waliyotatua, wanazunguka tu kugawa dawa za matende na mabusha zilizofanyiwa utafiti nchi nyingine tangu zamani za kale
- Hakuna ujuzi mpya waliogundua usaidie madaktari na manesi wetu katika kazi zao. Hivi katika vyuo vya madaktari, manesi na wafamasia vilivyoko nchini, kuna kitu gani angalao hata mada moja tu wanayofundishwa ambayo imegunduliwa NIMR? Watu mko busy kugawana perdiems halafu mnaita "capacity building", feki tu.
Hebu weka hapa orodha ya hizo knowledge unazosema zimekuwa advanced, na kwa kila moja useme taifa limepata faida gani.Hujui unachokiongea. Unadhani research Institutions zote duniani zimegundua hayo uliyoyasema. Lakini zime advance knowledge for betterment of human life/health in one way or another.........Kwa vile umejaa chuki, basi huwezi kuona any positive output from NIMR. Ngoja wale per diem safiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, roho ikutange ufe na pressure ya kupanda na kushuka!
''Anaye mlipa mpiga zumari ndio huchagua wimbo''. Hahaaa... wanasiasa watakuambia hujuma za mabeberu hizo; wanatoa grants halafu wanaelekeza ni tafiti zipi za kufanya ili kuvuruga malengo ya NIMR. Tuko vitani; ha ha ha!