NIMR yaja na utafiti kugundua ni idadi gani ya watanzania waliambukizwa virusi UVIKO19, COVID19. Safi sana

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2022
Posts
3,644
Reaction score
4,315
Tanzania inakwenda kuingia kwenye medani za kisayansi kwa lile 'jaribio lake la nchi nzima la kujiachia badala ya kujifungia kipindi cha korona'. A nationwide display of herd immunity at its best.

Hii itatusaidia sana kujua je ni kwa kiwango gani hii 'herd immunity' imetubeba.

Na itasaidia hata kuonesha kiwango gani chanjo, au ugonjwa wenyewe umesaidia kuwapatia wananchi kinga dhidi ya janga lile. Na ni kwa kiwango gani.

Kwa sasa unafanyika kwa watu wa Mbeya tu lakini itatupatia picha hata kwa Tanzania nzima hali inawezekana ilikuwajekuwaje?

Utafiti unamshirikisha mjerumani, hivyo tutegemee kazi ya uhakika. Tusubiri matokeo na majibu yoyote na tukubaliane na huo ukweli aidha tuliboronga au tuliscore (cheza kama Pele)

Hongera sana NIMR na LMUπŸ€πŸ‘πŸ‘

Disclaimer: Sihusiki mojakwamoja na utafiti huu, na nitakayoandika yaweza kuwa sio maoni halisi ya taasisi na mtafiti. Mimi ni mwananchi mpenda tafiti tu. Umeelewa??



 
Kuna wafadhili wa nje watapigwa na kitu kizito kichwani
Hapa wajanja wanataka kupiga hela, hakuna tafiti wala nini
 
Kuna wafadhili wa nje watapigwa na kitu kizito kichwani
Hapa wajanja wanataka kupiga hela, hakuna tafiti wala nini
Nimeipokea comment hii kwa masikitiko.


Utafiti unapaswa kuaminika maana hii ndiyo sayansi inavyoendelea.

Wanasayansi wote ni profesheno usiwasingizie.

Siasa zimekuathiri kuhisi kila kitu ni janjajanja. Ila nikuhakikishie kuwa sayansi ni hicho kitu, ni mahesabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…