Elections 2010 Nimrod Mkono uso kwa uso na TAKUKURU

huyu jamaa hamna mtu wa kumfanya kitu nchi ii, iyo chamber yake ya law duniani ipo kwenye chati, hata iyo kesi, ataimaliza kiulaini kwani sidhan serikali kama ina wakili wa kumpelekesha uyu jamaa mahakamani!


Bona,wewe ni mdanganyika!Kusema Mkono advocate ipo kwenye chati ni propaganda za watu ambao hawajui wanachofanya.
Kuwa na mzungu mmoja au wawili ,au mhindi kazini kwake sio nyenzo ya kuwa chati duniani!What a cock up.
Hii law firm imeshiriki kuiibia serikali billioni nyingi toka kwa mikataba feki ya BoT eti kuiwakilisha BOT.

Kuwa na uwakilisha kwenye nchi fake na poor duniani ,doesnt make you international.Eti Mkono do you think anaweaza kukuwakilisha mahakamani UK au USA?a total joke.
Firm hii kama IMMA na wengineo,wanaenjoy usanii na ulaza wa serikali ya sasa,no rule of law etc.Firm hizi sasa ziko kuwakilisha makampuni ya kigeni kwenye mikataba na serikali ,madini,uwindaji,govt contracts etc.

Huyu Mkono & coy wangekuwa CHINA wangekuwa tayari mahututi.
Na uchawi wao,iko siku itafika
 
Huyu anatakiwa awe KEKO !Mabillioni feki toka BoT bado yananuka.

KEKO akafanye nini.siumeona alivojibu kwa jeuri kuwa sio 80 ni zaidi ya simu 800....hahaaaaa
 
Sikuhizi hao waheshimiwa ndio wanatimiza eti ilani za chama chao cha Sisiem siku zote walikuwa wapi?tumesikia pikipiki zikimwagwa je huyu mwajiriwa wa serikali kapata wapi huo uwezo na kwanini mwajiriwa wa serikali awe mbunge? Nauzika kwelikweli halafu mijitu mizima inakubali kuhongwa simu ili kumpa ulaji tycoon fisadi huu ni ujinga ,dunia ya siku hizi watu wazima na akili yao wanajidharirisha kuhongwa simu,kweli kura yako inathamanishwa na vijisimu?na ndio maana nimeamua kutopiga kura kwa mchezo huu hakuna kura ya haki na halali ni kama kupotezeana muda.Pia takukuru ni sawa na Ze komedi sijui wanachunguza nini kwanza kwa swala la Nimrod takukuru hawatafanya lolote kwani huyo Hosea baba yake ndie aliemsomesha Mkono ni watu wa karibu hao,na mwisho Nimrod anamdhalilisha Mwl Nyerere ambaye ndie pia alimsomesha na kumfanya kama mwanae ,Mwl hakuwa na hayo mambo ya hovyo hovyo
 

Mzee, huyu jamaa Mkono siyo profesa na wala hajawahi kusimama mbele ya lecture room yoyote kumwaga matirio. Patner wake mmoja ndiye profesa wa chuo kikuu cha dar es Salaam. Usije kuwa unamchanganya na Profesa G. Mgongo Fimbo kwa vile majina hayo ya mkono na mgongo yanaelekea kushabihiana.

Mkono amekuwa jeuri sana tangu alipotajirika ghafla baada ya kukomba mabilioni ye fedha kutoka pale benki kuu. Huwa anaongea kwa kiburi kweli kweli, mojawapo ya matamshi yake ni kama ifuatavyo: "..... Padri Slaa hana fedha za kunilipa kwa hiyo sitaweza kumfungulia mashtaka kwa kunichafulia jina kudai mimi ni fisadi.....","... inabidi CCM itambue kuwa siyo ya wakulima na wafanyakazi tu, bali inabebwa na sisi wafanya biashara kama sisi...", ".....kampuni yangu siyo cheap, tunachaji dola 500 kwa saa...", " sikupeleka simu 80 bali ni zaidi ya simu 800..." Yote ni katika kuonyesha majivuno tu kuwa na pesa.
 
Hahahaha! tatizo letu hatupendi watu wanaojiamini...sasa yeye kusema amegawa simu 800 na sio 80 ni kosa? yaani asiseme ukweli??
Tuwaachie TAKUKURU wafanye kazi yao ambayo ni kuchunguza kama alichotenda Mkono ni kosa la rushwa au amevunja sheria ya gharama za uchaguzi kisha watupe majibu. Iwapo hatutaridhika nayo ndo tuwakosoe. Haiwezekani ukamwambia mtoto wako anayefanya mitihani kuwa najua lazima ufeli mitihani hii hata ufanye nini badala ya kumpa moyo, na kumwongoza ili afanikiwe katika mitihani hiyo. Tuwasaidie TAKUKURU japo kwa mawazo pale tunapoweza...kwanza TAKUKURU yenyewe changa sana, jaribu kuilinganisha na Polisi ambayo mpaka leo hii kesi kubwa inashindwa kuzifikisha mahakamani na kushinda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…