NIMRODI MKONO: Wanaotaka serikali tatu hawafai

NIMRODI MKONO: Wanaotaka serikali tatu hawafai

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Nimrod(7).jpg


Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM) Nimrodi Mkono
Mjadala unaoendelea kuhusu rasimuya Katiba Mpya, unayagusa makundi mengi ya kijamii na watu binafsi, kila upande kwa namna yake.
Lakini sehemu kubwa ya mjadala huo imejikita katika muundo wa utawala wa nchi, ambapo rasimu hiyo iliyotolewa na Tume ya Marekebisho ya Katiba, imependekeza kuwapo serikali tatu.Pendekezo hilo, limechukua sehemukubwa katika mjadala unaoihusu rasimu hiyo.
Mmoja wa watu ni Nimrodi Mkono, Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM) na mwanasheria aliyebobea katika tasnia hiyo kwa miongo kadhaa sasa.
Mkono, anajenga hoja yake juu ya msingi kwamba, Katiba inafaa kuwapo, lakini haipaswi kuwa jambo lenye uzito kiasi cha ‘kuteka’ mapokeo na nia chanya za viongozi waasisi katika nchi za Afrika, hususani kuhusu umoja wa nchi hizo na kupunguza wingi wa serikali zenye mamlaka kamili.
Ndiyo maana, Mkono anasema mfumo wa serikali tatu katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, utakuwa muendelezo wa mbinu za kikoloni, wenye lengo la kuwagawa wananchi na kutoa fursapana ya uporaji wa rasilimali za nchi.
Hivyo anasema, kiongozi yeyote anayeutetea mfumo huo, hapaswi kuutumikia umma wa Tanzania, hasa katika nafasi ya Urais.
Kwa mujibu wa Mkono, Katiba si kitukinachohitaji nguvu kubwa, badala yake nchi inaweza kuweka mambo ya msingi yanayopaswa kukubalikuwa, kufuatwa na kutekelezwa kama ilivyo kwa Uingereza.
“Wanaotaka serikali tatu, binafsi ninawaona kama wenye fikra mgando, hawayaishi mambo mema yaliyoasisiwa na viongozi katika nadharia ya kuwapo Afrika moja, tukagawanywa na wakoloni na sasawanataka kuigawa Tanzania,” anasema.
Mkono anasema tangu wakati wa ukoloni, Waafrika walikuwa wamoja, wakitendewa uovu na wakoloni walioingia barani humo kwa lengo la kupora rasilimali zao.
“Sasa wanaotaka Tanzania igawanyike na kuwa na serikali tatu, wanafanya hivyo kutoa mianyaya wazungu kuendelea kupora rasilimali zetu, watu wa aina hiyo hawafai kuwa marais wa nchi hii,” alisema.
Mkono anasema hoja hiyo alitaka kuiwasilisha bungeni mjini Dodoma, lakini ikadhibitiwa kwa mujibu wa kanuni zinazotoa muda mfupi kwa Mbunge kuzungumza.
Hata hivyo, Mkono, anasema ili Tanzania ijiimarishe kwa umoja, amani, utulivu, maendeleo na ustawiwa jamii, inahitaji kubaki katika mfumo wa serikali moja na kuwa na kiongozi mkuu (Rais) anayesimamia maslahi ya umma pasipo mgawanyiko.
AWASHANGAA WARIOBA, SALIM
Mkono anasema, inashangaza kuona wajumbe wa Tume ya Marekebisho inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba, kuwasilisha pendekezo la serikali tatu, huku wakiwa na uelewa wa kihistoria kuhusu umoja wa kuwapo umoja barani Afrika.
Ingawa hakuwataja kwa majina, Mkono, akaisema wapo watu waliowahi kuwa katika kundi G55 lililoibua hoja ya kuwapo serikali ya Tanganyika, na sasa wanataka kuifanikisha azma hiyo kupitia Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Jaji Warioba, anatajwa kuwa miongoni mwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), walioibua hoja ya Utanganyika mwaka 1994, wakati wa utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi, ambayo hata hivyo, ilizimwa kwa msaada wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Mkono, anasema pia kuwa katika tume ya Warioba, yumo mjumbe aliyewahi kuwa kiongozi wa juu katika Umoja wa Nchi Huru za Afrika(OAU), aliyetekeleza jukumu ya kuihubiri ‘Afrika moja’, lakini sasa ameingia katika orodha ya wanaotaka kuigawa Tanzania.
Mjumbe wa tume hiyo, Dk. Salim Ahmed Salim, alikuwa Katibu Mkuu wa sita wa OAU, ambaye kumbukumbu zinaonyesha aliifanya kazi hiyo kati ya Septemba 19, 1989 hadi Septemba 17, 2001.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI, 11th August, 2013
 
Tume kusoma mzee...kwa sasa kunatofauti gani kati ya wakoloni wa kiingereza na hawa tulio nao? Ukitoa rangi na jinsi wanavyo fika kwenye kilele cha utawala ila matendo yao yako sawa..Hawa wakoloni weusi wanaiba na kupeleka huko huko ulaya. Kama kweli CCM inataka Muungano wenye manufaa kwa pande zote basi tupiganie serikali moja kama kweli mnaweza viginevyo acha Tanganyika ije
 
1)Hivi Serikali ya CCM ilichukua maoni kwa Wananchi ikiwa Tayari ina majibu?
2.Kama kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni kwanini usiheshimu maoni ya mwenzio?
3.Hawa tunaowaita wakoloni si ndio tumewabatiza jina la Wawekezaji?
4.kwanini mbunge huyu asitumie nafasi hii kuwaambia mafanikio yaliyopatikana ndani ya serikali mbili?
 
huyu babu na kujifanya mahiri wa sheria ukiritimba wake ktk serikali utakeketwa na katiba mpya.anajifanya mwanasheria mahiri kwa nini asitettee wananyamongo kama kweli anatenda haki??? safari hii imtajibeba, mmemtukana jaji warioba hadi matusi ya nguoni sasa subirini mnyolewe na vikampuni vyenu uchwara.MNASHINDWANINI KUHESHIMU MAONI YA WENZENU HADI KUSEMA ETI HAWAFAI.POOR MKONO
 
huyu mzee anazeeka vibaya kwanza nasikia nyerere akumtka arudi hapa tanzania kwa wizi wake wa pesa ya umma alipotumwa kwenda kununua meli ya sserikali akachikichia na pesa zote atutolee uchuro wake hapa afanye mambo yake...kwa nn anamsema waryoba wakati wametoka sehemu moja? Mkono kajipange upya ndo urudi tena hapa na maoni yako kwenye juu la katiba hili.
 
Hawa wazee wa CCM kila kukicha wanazuka na kituko kipya!
 
Hawatufai kivipi? asimtelee mtu maoni aseme lake tu yakijumuishwa wenye nyingi ndio washindi.... mbona raisi wa sasa watu wanasema hafi lakini ndie anayeongoza
 
Nimrod(7).jpg


.....
"Wanaotaka serikali tatu,....hawayaishi mambo mema yaliyoasisiwa na viongozi katika nadharia ya kuwapo Afrika moja, tukagawanywa na wakoloni na sasawanataka kuigawa Tanzania," anasema.
Mkono anasema tangu wakati wa ukoloni, Waafrika walikuwa wamoja, wakitendewa uovu na wakoloni walioingia barani humo kwa lengo la kupora rasilimali zao.
"Sasa wanaotaka Tanzania igawanyike na kuwa na serikali tatu, wanafanya hivyo kutoa mianyaya wazungu kuendelea kupora rasilimali zetu, watu wa aina hiyo hawafai kuwa marais wa nchi hii," alisema.
Mkono anasema hoja hiyo alitaka kuiwasilisha bungeni mjini Dodoma, lakini ikadhibitiwa kwa mujibu wa kanuni zinazotoa muda mfupi kwa Mbunge kuzungumza.
Hata hivyo, Mkono, anasema ili Tanzania ijiimarishe kwa umoja, amani, utulivu, maendeleo na ustawiwa jamii, inahitaji kubaki katika mfumo wa serikali moja na kuwa na kiongozi mkuu (Rais) anayesimamia maslahi ya umma pasipo mgawanyiko.....

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI, 11th August, 2013

Blue: Nakubaliana naye asilimia mia kwa mia
 
Hawa wazee wa CCM kila kukicha wanazuka na kituko kipya!
Wako wengi tunaounga mkono serikali moja....tukiamua kuwa na mbili basi serkali hizo ziwe huru siyo kwa mtindo wa CCM wanaotaka...serikali tatu za mtindo wa CHADEMA pia hazikubaliki. Tunataka serikali Moja ili tudumishe muungano.

https://www.jamiiforums.com/katiba-...serikali-tatu-;-sema-ndiyo-serikali-moja.html

https://www.jamiiforums.com/katiba-mpya/495930-serikali-moja-ni-wazo-zuri-ila-nafikiri-iwe-hivi.html

Hii pia inafaa kusomwa>>>>https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/2511-kanuni-15-za-uongozi-za-mwanakijiji.html
 
Back
Top Bottom