Nimsaidiaje huyu jamaa yangu! Huwa anaota

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2008
Posts
3,173
Reaction score
482
Nina mshikaji wangu mmoja hivi. Tunaelewana sana ila ana shida kidogo. Anapenda totos kwa sana. Tatizo lake ananambia kuwa akido tu nje mywife wake humuuliza kesho yake jana ulikuwa wapi na nani. Je ulitumia co***mu ama. Kisha hushuka valangati la kuua mtu. Mimi nimehisi huwa anaota hivyo kumpa mwanya mke wake kujua kuwa alikuwa kwa small house. Anaomba ushauri afanyeje!
 
Aache mechi za ugenini..
 
Ushauri simpo mwambie aache ngono za nje..kwani mkewe hamtoshi???
mkewe nae akienda afu aote ye amsikie ye atajisikiaje au atachukua hatua gani..mxiii
kujiendekeza tu huko
 


mkuu hapo ushauri wa nini wakati anajua kabisa tatizo ni nini? aache kazi za nje tu
 
Imemuwia shida sana kuacha small house. Huwa anamkwepa hata kwa mwezi ama zaidi lakini small house huwa inamuibukia kiaina na akimwona tu ka mbwa na chatu!
 
Kuna taarifa hazipo hapa,uwezo wake wa kuchakachua,umakini wa kujipanga,n.k.Kwa nini nae ameoa na anaenda nje ya ndoa.Mshauri jamaa yako aache kupenda ngono!!!Kwa upande mwingine anaonekana sio smart huenda anafanya sana kwa small house akirudi yuko hoiii anashindwa kutimiza wajibu wake na kuota ovyo.Yeye atulie na mkewe kwani hampi mambo??Kama hawezi kuacha ajipange kwanza huenda uwezo wake kumudu ngwe ni mdogo
 
natamani nipate mume wa design hii kwani ni rahisi kumdhibiti
 
Sasa kwa nini alioa kama bado ana-feel kutoka nje ya ndoa?? alilazimishwa kuoa au?? Mwambie aache tabia za kutoka toka nje. Muasi siku zote hujulikana tu, kutokana na kujishtukia shtukia!!!
 
huyo mama angemuacha mumewe ili angonoke tani yake,kama amerudia zaidi ya mara moja means hamtoshelezi au huyo baba ana pepo la ngono either way hafai,asije akamletea magonjwa ndani dada wa watu buree...
 
mmmh????!!! MARYTINA umeniacha njia panda SIJAKUELEWA,,,,WEWE UNGEMDHIBITI VIPI HUYO MUME MPENDA VISMALL HSE?
 

Niweke sawa hapo kwenye red ni wewe au huyo rafiki yako.?

Nauliza nina sababu ya msingi kwamba kama ameweza kukwambia hayo yote kwanini hilo la kuwa anaota asikwambie?? Huyo ni wewe sema ukweli wako kama sio wewe basi rudi umuulize vizuri huyo mkewe hujuaje kama katoka nje??
 
Haya mambo ya small house mi yananikatishaga tamaa sana!!!
Sijui kuna siku, nitayaona ya kawaida.
Nyie wanaume bwana. Khaaaaaaaaaaaaaaah!!!
 
Imemuwia shida sana kuacha small house. Huwa anamkwepa hata kwa mwezi ama zaidi lakini small house huwa inamuibukia kiaina na akimwona tu ka mbwa na chatu!

Umejuaje haya yote???!!


Dena, hii inaweza kuwa kweli...ni yeye tu mwenyewe anakuja kwa jina la rafiki yake!

Kwa hali hii, kuna safari ndefu ya kuondokana na ukimwi! Muogopeni Mungu jamani!!
 
]Imemuwia shida sana kuacha small house[/COLOR]. Huwa anamkwepa hata kwa mwezi ama zaidi lakini small house huwa inamuibukia kiaina na akimwona tu ka mbwa na chatu!



Unazidi kunichanganya kabisa
 
Umejuaje haya yote???!!



Dena, hii inaweza kuwa kweli...ni yeye tu mwenyewe anakuja kwa jina la rafiki yake!

Kwa hali hii, kuna safari ndefu ya kuondokana na ukimwi! Muogopeni Mungu jamani!!

Umeona eeehhh huyu jamaa anajichanganya mwenyewe mambo yote hayo atayajuaje???
 
Nimeisoma hii thread toka mwanzo na comment zote, inaonesha wazi mkuu huna rafiki bali ni wewe ndio una tatizo hili.... ushauri wa bure: Acha kabisa mechi za ugenini kwani siku kiatu kikivuka utajikwaa na kupata donda ndugu:hatari:!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…