Nimsaidieje mpenzi wangu?


Hata kama kazi imeisha, ni jambo la kheri kumalizana na mwajiri wako kwa uzuri. Kama ulikopa si budi ulipe? Kuna leo na kesho. Ukiondoka vibaya watakapohitaji reference zako zitajazwa hivyo hivyo. Swala la kujaziwa fomu za NSSF, mwajiri hawezi kujaza hizo fomu kabla ya kufanya "Clearance" si kwa ubaya au chuki binafsi, kuna auditors wakija kuta Ex-employee anadaiwa hiyo ni Query. Sorry kwa hilo mimi ni mkaguzi huwa tunauliza sana jambo la Clearance kwa mfanyakazi aliyeondoka hasa pale ambapo bado anadaiwa.
 
Kiranja Mkuu kosa umetenda wewe, kwanini wewe ulichanganyikiwa
Wewe mwanaume mlume ndago kisabuni hungeepuka kuchanganyikiwa
Mkeo tamko la msaada alihitaji toka kwako na sio kuparanganyikiwa
Mpe moyo mkeo nawe uwe mstari wa mbele kuchakarika
Msaada mkubwa unao mtoto wa kiumeni wewe husichanganyikiwe
 
Huu ni mtihani tu kama ilivyo mitihani mingine cha muhimu zaidi ni kujipanga ili kupata njia iliyo sahihi kulitatua. Mwambie aache kulia na umtie moyo kuwa haya yote utayashughulikia.
Kaachishwa kazi na wala hakunyang'anywa vyeti, ambavyo ndo silaha yake.
Kwa kuvitumia vyeti hivi ataweza kuugeuza upande wa pili wa shilingi.
 
pole sana Kiranja na familia yako,for what you are going through.....tupo na nyie kimaombi
 
Kwani alizaliwa na hiyo kazi? Kwani aliipataje? Kwani elimu yake si inamruhusu kutafuta ajira nyingine? Alifanya kosa gani? We si upo kuendesha maisha? Yeye bila kazi hutampenda? Kama alikopa anategemea angerudisha vipi mkopo? Akiyajibu haya maswali hana sababu za kulialia. Vinginevyo anaona huwezi kumudu kumtunza. Wakati mwingine uwe mkali kidogo kwani ukimwonea huruma sana nae anakujengea picha ya jinsi anavyotaka uone anavyoumia
 
Dont remind me of lady boses.....especially kwenye kutoa references....wabaya:A S 39:

Acha kabisa hii kitu!

Ndo maana nikisikia habri ya woman emacipation natafari sana na kujiuliza was God crazy kutupatia uongozi juu ya hawa viumbe?
 
.............dont wory...........evthng gona b alrght...........
mungu anaona na mungu amtupi mja wake........
 
Waajiri wengine wanakamata hiyo kadi ya mfuko mpaka uipate akili ishaka sawa..
Msikate tamaa chini ya jua kila kitu chawezekana...
 
That is so wahindi!
Hakuwa kwa chama chochote cha wafanyakazi? cuz wao ndo kimbilio la kwanza if something like that happened.
 
Nafikiri hana sababu ya kukata tamaa kiasi hicho, kitu cha msingi aende huko NSSF akawaambie jibu alilopewa na mwajiri wake .Nafikiri alipokuwa anakopa huko kazini lazima kulikuwa na makubaliano kuwa ikitokea mtu akiachishwa kazi wakati bado hajakamilisha Deni ni kipi kinafanyika. kuanzia hapo ndiyo atapata ushauri nini cha kufanya. Utaratibu wa kulia hautamsaidia kitu chochote zaidi ya kumpotezea muda wa kutafakari kipi cha kufanya. kuacha kazi sehemu moja ni njia ya kupata sehemu nyingine kibaya ni kifo au ugonjwa lakini vinginevyo aangalie mbele, suala lake hilo ni la kawaida siku hizi hasa kwa wale wanaokopa bila kujua namna ya kulipa deni pindi linapotakiwa. hivyo ajitie nguvu.πŸ˜›ound:πŸ˜›ound:πŸ˜›ound:
 

nimekubamba leo..
 

nimekubamba leo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…