Nimsomeshe kisha nimuoe aje kua mke(akimaliza form four)

haszu

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2017
Posts
978
Reaction score
2,313
Kumsomesha mchumba najua kumewaliza na kuwatesa wengi, bahati mbaya au nzuri nami nimeangukia katika mtego huo.

Kutokana na hali ya kiuchumi najua sitaoa kwa miaka miwili mitatu ijayo.

Nimeona nimlee mtoto ambae kwa kweli ni mzuri na anazidi kupendeza.

Yeye hajui chochote, nimeongea na mlezi wake kakubali. Ila najua kuna mawili, ukiacha kifo kututenganisha, ni aje abadilike awe na tabia mbaya au anikatae.

Najipanga kisaikolojia kwa yote huku nikimuomba Mungu kwangu na kwa huyu mtoto asibadilike na aje anipende.

Dua zenu pia ushauri nini naweza fanya kudhibiti tabia na mengineyo kwa wenye uzoefu na wajuzi.
 
Mchumba hasomeshwi mkuu hizo pesa mpelekee mama yako kule kibaon kama bado yupo hai atumie atakuombea baraka
Je nifanye ili nimpate nikiwa ninania nae na sitaki kupita njia za panya? Vp nikifanya kma msaada?
 

Hapo bolded black utakuwa umefanya jambo la maana, kujiandaa kisaikolojia ndicho kitu wengii huwa wanakosa.
 
Pumbavu.
Girlfriend hasomeshwi
 
Kama umejipanga kisaikolojia hapo sawa nakubaliana nawe ufanye unachotaka vinginevyo siku shauri ni sawa na kukisomesha kifo chako.
 
Je anajua kuwa umejitoa kwa ajili yake?
Ukweli hajui kma ninania hiyo, ila akiniona anaaibu sana na muda mwengine hujificha , sijajua kma hanipendi au nini, ila mimi namkubari sana ingawa najua safari sio ndogo mana four years ahead apo kati kunamengi
 
Hii bado ijaniingia akilini bado inazunguka tuu nje ya kichwa unamaanisha bado ajaanza form one aunimesoma vibaya yani ni mtoto adi basi arafu unasema ni mzuri umempenda kuwa serious we una miaka mingapi kwasabu akifikia umri wakujielewa awezi kukubali ata kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…