Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,156
- 10,974
Hii imekaa kiwaki sana. Nimejaribu kuassume tokea majuzi, naona haiingii akilini kabisa. Mfano ulio hai, nina mke, Mama Chanja. Kusema kweli ninavyovipata kwa Mama Chanja sijawahi kuridhika, kwanza nimezoea na isitoshe siku ninapoitaka, yeye anakuwa out of mood, siku ambayo nimepiga zangu vileo nimechoka, yeye ndo anautaka. Shuwain
Niliamua kutafuta kajenereta ka siri ambako ni kabinti X ka jirani yangu, tukawa tunasambaziana upendo japo kwa siri na tahadhari kubwa sana, usiri huo sio kwamba namuogopa Mama Chanja, bali sitaki wanangu walelewe na mzazi mmoja. Itokee Mama Chanja ajue kuwa mimi ninatoka na binti X, halafu atafute migambo wamteke huyo binti na kwenda kumfanya kitu mbaya ikiwa ni pamoja na kupita barabara linaloelekea Peruu. Kosa la binti liko wapi? Kwanini wasinikamate mimi?
Same applied nimetongoza mke wa mtu kanikubalia, tumekuheshimu tukaamua kwenda kufanyia ufuska mbali na eneo ulipo, yaani sijadiliki kuingia kwenye malango ya chumba chako ama kupanda juu ya godoro ulilolinunua kwa jasho lako. Halafu upate fununu uamue kutuma vijeba waje kwa lengo la kunitindua, umeambiwa hiyo mali safi imepachikwa kutoka kwenye ubavu wako?
Hii sio haki. Hili nalo serikali ikalitizame kwa kina!