Nina App idea naombeni ushauri

Nina App idea naombeni ushauri

hellhound

Member
Joined
Oct 13, 2020
Posts
17
Reaction score
15
Habari zenu wakuu.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, ni kwamba nina idea ya kutengeneza mobile app ambayo itakuwa ni music streaming kama ilivyo spotify ama youtube music n.k.

Kama tunavyojua kwamba app kama spotify haisupport nchi nyingi za Afrika ikiwemo Tanzania labda mpaka tutumie VPN, na matumizi ya VPN wanayafahamu watu wachache kwa hiyo inakuwa ngumu kwa watu wengi kutumia.

Kwa hiyo nilikuwa na app idea ambayo itakuwa ni music streaming app ambayo kutakuwa na artist na users wa kawaida(streamers). Ambapo kutakuwa na system ambayo verified artist tu watakuwa na uwezo wa kupost miziki yao (audio) na pia kujipatia kipato kutokana na idadi ya streamers waliosikiliza miziki yao kama ilivyo spotify.

Ninachohitaji ni mawazo yenu juu ya hii idea tu kuhusu developers, servers n.k hivyo nitajua.

Kama kuna ambaye hajanielewa vizuri kuhusu hiyo idea refer app ya spotify, nataka iwe na features zote kama spotify ila nataka itumike hapa hapa Tanzania yaani artist wawe ni hawa wa hapa Tanzania.

Asante nawasilisha.
 
Wabongo hawapendi kununua miziki mtu atakwambia nikastream wimbo wakati huku kwingine nitaudownload bure na kuusikiliza hata kama sina bundle.

Ndiyo maana wengi wanaoanzisha platform za kuuza nyimbo kibongo bongo wanafail. hata ya wasafi haikudumu wakati wimbo ulikuwa 300 tena unaudownload kabisa. Sikukatishi tamaa ila ndo ukweli. We jiulize wewe mwenyewe umewahi kununua nyimbo ngapi?
 
Wabongo hawapendi kununua miziki mtu atakwambia nikastream wimbo wakati huku kwingine nitaudownload bure na kuusikiliza hata kama sina bundle. Ndiyo maana wengi wanaoanzisha platform za kuuza nyimbo kibongo bongo wanafail. hata ya wasafi haikudumu wakati wimbo ulikuwa 300 tena unaudownload kabisa
Sikukatishi tamaa ila ndo ukweli. We jiulize wewe mwenyewe umewahi kununua nyimbo ngapi?
Dah nikweli mkuu tena huwa nikitafuta mziki nikakutana na site inauza huo mziki huwa nakimbia kama nimeona simba. Ila nilikuwa nimelifikiria hilo nikaona iwe ni kustream bure kwa users wa kawaida, then kutakuwa na system ambayo app itaingiza pesa hata ads na hyo pesa tutagawana percent flani na artist.
 
Dah nikweli mkuu tena huwa nikitafuta mziki nikakutana na site inauza huo mziki huwa nakimbia kama nimeona simba. Ila nilikuwa nimelifikiria hilo nikaona iwe ni kustream bure kwa users wa kawaida, then kutakuwa na system ambayo app itaingiza pesa hata ads na hyo pesa tutagawana percent flani na artist.
Mdundo.com wanafanya hii.
 
Back
Top Bottom