Nina changamoto na namna ya kupata huduma BRELA

Silicon Valley

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2012
Posts
1,092
Reaction score
1,118
Wananchi wenzangu natumaini hamjambo.

Wadau wote wa BRELA natumani mko salama,
Nina changamoto na namna ya kupata huduma BRELA

Ni muda sasa nahangaikia hili swala , ukienda ofisini kwao makao makuu wanakuambia hakuna kitu kinafanyika pale mambo/huduma zote ni mtandaoni tena anakujibu mkato tu na anahamia kwa mwingine.

Ukifungua WEB SITE yao ni complicated kiasi kwamba SIO RAFIKI KABISA kwa mtu wa kawaida.

SWALI LANGU twende wapi kupata huduma ? au ni mazingira ya kuwatengenezea VISHOKA ? ? maana hao wamejaa hapo tu nje ya ofisini kwao

MFANO TU: TO RE-ACTIVATE the old company , How to select exactly the service you want, ni ngumu terminology zilizotumika ni kama za Law kwa mtu wa kawaida ni ngumu kuzibainisha tofauti zake km zina fanana then ndio upload documents
 
Mkono mtupu haulambwi
 
Wapeni watu kazi. Hizo ndio fursa zenyewe. Kama mambo ya mtandao huelewi mpe anaelewa akufanyie. Serikali imehamishia huduma nyingi kwenye mitandao. Sasa wewe kama unaona huwezi tafuta wanaoweza wakufanyie.

Kwangu mi naona hii kila kitu mtandaoni ni nzuri sana. Imepunguza kutembea tembea sehemu moja kwenda nyingine. Unakaa ofisini unafungua kampuni, unafile return and everything. Hii imepunguza mianya ya virushwa visivokua na masikio.

Changamoto ya website ya brela nayoona kuna siku inakua slow mno lakini with time vitu vitaenda tu sawa.
 
Njooo PM nikutengenezee fasta. Mimi nilikuwa na tatizo kama lako nikakomaa nao mpaka nikafanikisha
 
Pole sana kiongozi. Hawa Brela sijui shida ni nini email hawajibu nimewaandikia zaid ya mara tatu lakini wapi. Mwenyewe shida yangu niliisha sajil jina la biashara lakin wakati wanafanya maboresho ya website yao wakatulazimisha kutumia usee Id na pasword ambayo ni system generated, pili jinsi ilivyo humo ndani sio rafiki kabisa
 
Mkuu unashida gani hasa?
 
Pole sana...

Ila mbona kwenye website yao fomu zipo kwa lugha ya kingereza na kiswahili?

Kama unashindwa tafuta mtu akujazie... tena kwa website haichukui hata dakika kumi kujaza kila kitu...



Cc: mahondaw
 
Mkuu unashida gani hasa?
MFANO TU: TO RE-ACTIVATE the old company , How to select exactly the service you want, ni ngumu terminology zilizotumika ni kama za Law kwa mtu wa kawaida ni ngumu kuzibainisha tofauti zake km zina fanana then ndio upload documents
 
MFANO TU: TO RE-ACTIVATE the old company , How to select exactly the service you want, ni ngumu terminology zilizotumika ni kama za Law kwa mtu wa kawaida ni ngumu kuzibainisha tofauti zake km zina fanana then ndio upload documents
Pole sana Mkuu
Lakini katika suala la kusajili au kuifuta kampumi kuna masuala ya kisheria ambayo ni vema ukawatumia wataalam (wanasheria, consultants et al) ili kufanikisha jambo lako kirahisi zaidi na kwa ufanisi zaidi. Unaweza kuwalaumu BRELA kumbe tatizo lipo kwako mwenyewe! Kwa ujumla website ya BRELA ni elekezi sana na pia kuna lugha mbili za kiswahili na kiingereza hivyo kukupa nafasi y a kufanya unachohitaji kwa lugha unayoimudu vema.
 
Shukran sana nakuelewa , ndio maana tunasema SIO RAFIKI kwa wazalendo wa kawaida, Pili mm naamini hakuna terminology ya kisheria au taaluma yeyote isiyoweza kutafsiriwa ili mtu wa kawaida aielewe hata tu kutumia Q&A tab ili ukikwama una refer pale then unaendelea hatimaye unamaliza.

Huoni pana uzembe hapa ? kama kweli panahitajika mtu anayejua ili kumfafanulia mteja wao KWA NINI BASI WAO WASILIFANYE HILO, Yaani waruhusu wateja kuingia ofisini kwao na kuwahudumia ndio kazi yao walioajiliwa,

Ni haki kweli tena sisi wateja kuchukua gharama zingine kwa mwanasheria au KISHOKA na ilihali ofisi ya serikali ipo na haipo busy kisa ONLINE SERVICE
 
Nimekuelewa Mkuu Silicon Valley
Ni vema ukatambua ya kwamba BRELA wanahusika na USAJILI na LESENI TU na sio KUHUDUMIA UANDAAJI WA VIELELEZO VYA KWA AJILI YA USAJILI japo wamewekwa Mwongozo wa vielelezo gani vinahitajika katika usajili wa hitajio lako.
Huhitaji kishoka bali mtu mwenye sifa stahiki kuifanya kazi yako. Nakupa mifano hii michache

1. Kuandaa MEMARTS
Je hapa terms zote za kisheria utazijua vema ikiwa si mtaalam wa sheria? Kwa hy utaona namna gani mwanasheria anahusika hapa na sio BRELA. Ina maana MEMARTS yako ikiwa haijakidhi vigezo jukumu la BRELA itakuwa ni kuikataa

2. Kuhamisha hisa/kufuta kampuni
Utahitaji uwasilishaji wa vielelezo kama "share transfer certificate" kutoka TRA, ktk hili utaona lazima uandae hesabu za mizania, hivyo usipowasilisha ktk mfumo wa ORS kitakachofanywa na BRELA ni kurudisha maombi yako na kukuelekeza tu ni cha kufanya

Conclusion
Pia BRELA kuna namba za simu za kuongea nao moja kwa moja. Kwa kuwa ukienda wanakupiga chenga ni vema cheki namba zao zipo ktk website yao utaongea na wahusika mfano upande wa usajili kampuni au alama za biashara au leseni nk nk
 
Shukran sana na unaeleweka vema, utaratibu huo hapo juu unaeleweka vema tu, kuhusu shida yangu hii ni kampuni iliyokwisha sajiliwa zamani vyote hivyo hapo juu vipo hakuna pungufu, ni vile walibadili utaratibu wa manual na kuhamia mfumo wa TEKEHAMA tunahitajika ku RE ACTIVATE kwa mfumo mpya.
 
Sawa Mkuu
Kwa mahitaji yenu ina maana mnahitaji kwanza kuhuisha maelezo ya kampuni yenu baada ya hapo ndiyo uendelee na nini hasa unachotaka
Kuna uzi niliuweka hapa chini waweza kuwa msaada mkubwa wa changamoto unayopata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…