Nina gagaziko la uelewa wa sheria na kanuni za mpira wa miguu. Naomba ufafanuzi kwa mwenye uelewa

Nina gagaziko la uelewa wa sheria na kanuni za mpira wa miguu. Naomba ufafanuzi kwa mwenye uelewa

cafolola

Member
Joined
Dec 25, 2020
Posts
46
Reaction score
44
Ikitokea Timu X na Timu Y zinacheza fainali ya maamuzi ya mpira wa miguu. Mpira ukachezwa kwa dakika 120 ngoma droo. Lakini Timu X iko pungufu baada ya wachezaji wake wawili kutolewa nje kwa kadi nyekunda ndani ya dakika 90 za mchezo.

Timu zimekwenda kwenye mikwaju ya penati na Timu zote zimepata penati Tisa Tisa. Timu X wapiga penati wamekwisha lakini Timu Y Ina wachezaji wawili zaidi hawajapiga.

Je, hao wachezaji wawili Wataruhusiwa kumalizia kupiga penati zilizo salia?

Na Kama watafunga Je watatawazwa kuwa mabingwa wakati Timu X hawakukamilisha penati 11? Naomba Ufafanuzi kwa wajuzi wa sheria za mpira wa miguu.
 
Timu ambayo inawachezaji waliotimia lazima ipunguze wachezaji wawili kufanya uwiano
Hili ndio jibu sahihii. na lazima kabla ya upigaji wa penati, mwamuzi lazima apewe majina ya hao wachezaji wawili na jezi namba zao. Hivyo wakati wa upigaji wa penati hao watajitenga.
 
Hili ndio jibu sahihii. na lazima kabla ya upigaji wa penati, mwamuzi lazima apewe majina ya hao wachezaji wawili na jezi namba zao. Hivyo wakati wa upigaji wa penati hao watejitenga.
na ikitokea wote wamepata penalt shillingi/coin itaamua mchezo au wataanza kujirudia?
 
na ikitokea wote wamepata penalt shillingi/coin itaamua mchezo au wataanza kujirudia?
Mmarudia tena mpaka mmoja wenu akose.

Kwenye history ya penalties ipo rekodi ya Washington na Bedlington hawa walitoka sare ya 3-3

Wakaenda matuta, zile shootout tano za mwanzo kila mtu alifunga. Wakaenda mpaka 25-24
 
Sio kwamba mnarudia baada ya wachezaji wa timu zote kupiga?
Napa ni tofauti kidogo. Timu moja wachezaji wote 9 wamepiga wakati timu nyingine Ina wachezaji wawili hawajapiga. Hii imekaaje?
 
Timu ambayo inawachezaji waliotimia lazima ipunguze wachezaji wawili kufanya uwiano
Naomba nikuheshimu zaidi kuanzia Leo. Si kwamba Nilikuwa nakudharau, hapana. Lakini jibu hili sahihi linaonyesha wewe na soka ni damu damu. Big up Mkuu.
 
Back
Top Bottom