Nina hamu sana ya kubeba mimba

Kuna msicha flani aliolewa akiwa na mimba lakini cku ya kujifungua kwabahati mbaya mtoto alifariki! Basi maisha yakaendelea takribani miaka mitatu bila ya kushika mimba tena! Ikawa marumbano,ungomvi,chuki na kutokuelewana ndani ya nyumba. Wiki moja mbele yule mwanaume akamfukuza yule mwanamke. Ila kwa7bu ya ukarimu na uzuri wa yule mwanamke akapata mfadhiri ya kumsaidia sehemu ya kuishi kwa muda basi maisha yakaendelea kwa miezi mitatu mbeleni yule mwanamke akashika mimba ya yule yule aliyemfadhili. Kwaiyo sometimes tatizo ilanaweza kuwa kwa huyo mwenzako.
 
Jf bwana yaani huku kuna watu waliopinda hadi hawafai tena yaani mtu anaomba ushauri nyie mnamshupalia na majibu ya mkato hv maadili yameenda wapi [emoji86] jamani!! Hv ingekuwa ww ndo umeomba ushauri ukajibiwa hivyo utajiskiaje
 
Pole dada, ushauri wangu ni mdogo tu lakini ukiuamini utapona tatizo lako.
Naamini unamwamini Mungu hivyo yaachilie maisha yako kwa Yesu, omba kwa kumaanisha ikiwezekana ufunge hata siku moja kwa wiki, ukiamini hakika Mungu atakuponya, mimi nilishapona vidonda vya tumbo kwa kuamini maombi, naamini hata hilo lakwako linawezekana ukiamini na kuyaachilia maisha yako kwa Yesu.

Msalimie sister mbwambo hapo st. Thomas
 
1. Mtangukize Mungu.
2. Kula chakula bora
3. Kama upo overweight hakikisha unapunguza uzito....fanya mazoezi kwa kiasi. Na hakikisha dinner ule kabla ya saa moja na nusu jioni
4.fuata ushauri wa daktari
5. Usisahau dawa za virutubisho (kama prenatals nk nk) ili upate nutrients na vitamini
 
Pole sana nimewahi kusikia kaina dada wenye matatizo ya kupata mimba na kutumia dawa za miti shamba na wakafanikiwa. Sijui kama kufanikiwa huko ni kutokana na miti shamba au ni uwezo wa Muumba wetu. Pia nimewahi kusika wengine ambao wanakuwa na pressure kubwa sana (mke na mume) wanapokuwa wanatafuta mtoto kiasi ambacho hata tendo la kugegedana linakuwa halina utamu tena. Wao wanagegedana ili tu kupata mimba na kila yule mheni anapojitokeza basi hunyong'onyea. Ushauri wa madaktari baada ya kuwapima na kuwaona wote wako bomba ni kwamba wasiweke kwenye pressure kubwa wafurahie maisha ya na ndoa wafurahie tendo la ndoa. Na mara nyingi ndani ya miezi sita mdada hushika mimba. Hivyo nawe acha kujiwekea pressure kubwa sana labda Mungu ataleta neema zake upate kile ukitakacho. Kila la heri na Baraka.
 
Nitafute mimi nikutibie upate mimba na kuzaa mtoto. Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…