Kuharisha damu ni swala moja ila tumbo kutokuuma hilo ni swala tofauti kabisa.
Kwa uzoefu wangu utotoni niliwahi kuumwa Amoeba ila sikufika hatua ya kupata choo chenye damu lakini tumbo lilikuwa linauma kwa kukata mpaka unaenda chooni unatembea ukiwa umeinama, hivyo kwa maelezo yako sidhani kama ni Amoeba.
Pia sidhani kama ni Ulcers maana mpaka muda huu ninaandika ninazo na huwa zikichachamaa tumbo linauma unaweza kupiga ukelele wa kuomba msaada, pamoja na hayo sijawahi pata choo chenye damu hivyo sidhani kama ni Ulcers.
Kuhusu kichocho sina uhakika kwa sababu sina experience nacho ila ninachojua dalili moja wapo nikutoa mkojo uliochanganyika na damu kwa sababu wataalamu wanadai kichocho ni UTD's (Urinary Transmitted Disease) kwa mantiki ni kwamba zinaaffect njia ya mkojo sasa kwa haja kubwa sijajua, labda tusubiri wataalamu.