Muhimu ni kujua tractor unit model ipi inafaa kwa sasa kwa matumizi ya kibiashara kwa Tanzania kwa kufanya local trips.
Model zipi zimeonekana na usumbufu (spare parts na mafundi), uimara wa gari kufanya trip nyingi bila break down, etc.
Trucks nyingi kwenye mtandao ni automatic gearbox. Je vipi hapa kwetu madereva wanazimudu? Vipi kuharibika haribika, etc
Ukizungumzia local trips kwa Tz bado huwezi kuacha kuziongelea safari ndefu!
Upande wa scania, R series ndiyo ilikuwa designed kwa safari ndefu though kwa sasa imeongezeka S series.
Sijui uwezo wako kifedha plus uzoefu wako ila usibaki nyuma saaana, chukua R440 2012 model hasa lile khadija kopa (tag axle).. nadhani hata wewe unaziona zilivyozagaa!!
Haiteseki na milima, kwa mbio hapo ndiyo kwao!!
Hazina magonjwa ambayo ni common hivyo itategemea na unavyoitunza ukizingatia mafundi wako kila kona hadi mafundi pikipiki wanaweza kufix matatizo ya scania [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kwenye miji mikubwa, spare zimezagaa kiasi kwamba vitu kama filters, water separator unaweza kununua hata Kwenye duka la mangi [emoji28][emoji28][emoji28]
Kuhusu madereva aisee hapa tuwe serious kidogo! Ajiri mtu ambae atleast anaweza kusoma kingereza na kukielewa. Awe trained, na aendeshe kwa kufuata user guide!
Hizo gari ni smart trucks zinazohitaji smart drivers.. lazima dereva ajue kila kilichopo ndani ya cabin kina kazi gani na kinatumika wakati gani!!
Ile instrumental cluster inatoa taarifa mbalimbali ambazo ni lazima dereva ajue hiyo taarifa inahusu nini..
Mwisho dereva lazima awe msafi tena msafi sana, ikiwezekana awe ni mtu anaependa magari!
Ngoja niishie hapo wataalam watakuja kufafanua zaidi!!