Nina hofu huenda nimeambukizwa UKIMWI, Naombeni ushauri wenu jamani!

Onguluo

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2013
Posts
406
Reaction score
116
Habari zenu, poleni na majukumu ya siku!

Ndugu zangu ni muda wa miezi mitatu sasa nikiwa katika hali ya sintofahamu juu ya afya yangu na nimekuwa katika depression kubwa sana..

Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 30. Nina mchumba ambaye nimedumu naye kwa muda wa mwaka mmoja sasa, hatujawahi kukuta kimwili na binti huyo, tuko wilaya tofauti ndani ya mkoa mmoja.

Tarehe15 Novemba 2014, siku ya jumamosi saa moja jioni nilienda kwa mama mmoja ana km miaka 33 hivi ni anafanyabiashara ya asali hapa mjini.

Nilienda kutafuta asali mbichi kwa ajili ya kuchanganya na dawa ya vidonda vya tumbo. nikiwa ndani mwake nilishawishiwa na yule mama kwa namna nisiyojua nikajikuta nimefanya naye mapenzi (ngono zembe) na kibaya zaidi sikutumia kondom, ilikuchukua almost dk 2 kumaliza. Nikachukua asali yangu na kuondoka kwenda kwangu.

Nikiwa njiani majuto yakaanza na kujilaumu kwann nimezini na mtu nisiyefahamu afya yake bila kinga, nilipofika home nilipiga magoti na kumuomba Mungu anisamehe dhambi yangu. Nilifikiria kumpigia yule mama usiku huo ili nimuulize juu ya afya yake ila sikuwa na afya yake, nilazimika kutafuta namba zake na kumpigia simu usiku huo.

Nilimpigia simu nikamuomba aniambie iwapo kama yeye ni mgonjwa (Muathirika wa HIV) ili niwahi kuripoti hospital within 72 hrs. Lakiniyule mama aliniambia kwamba yeye ni mzima na hata nikitaka tukapime. Majibu yake yalinipa matumaini na nikaendelea na shughuli zangu za kila siku, baada ya muda ya wiki 2 net niliugua mafua makali sana makamasi mazito sana yenye mchanganyiko na damu na hata dawa za mafua nilizotumia hazikusaidia chochote!

Baada ya wiki 2 mafua yalikata, kichwa kikaanza kuniuma sana kuanzia kwenye paji hadi utosini km muda wa wk moja hv. kwakweli niliona dalili zilizonitisha, nililazimika kumuambia yule mama kwamba ameamua kuniangamiza maisha yangu kwa kunipa maradhi makusudi, yule mama alikataa kata kata kwamba yeye anajujua ypo vuzuri hata maradhi, kwamba n wasiwasi wangu tu.

Tarehe 02 January tulienda naye tukapima HIV lkn matokeo yakawa negative wote. hyo ilikuwa muda wa mwezi mmoja na nusu tangu nisex naye.

Baada ya majibu hayo nilijipa matumaini ya uzima lakini mpaka naandika uzi huu hapa mambo totauti kabisa nimeona dalili tofauti za kunitisha, mwili hauko vizuri kwa ujumla tatzo kubwa zaidi ni maumivu ya koo na kuvimba kwa tezi shingoni karibu na taya ni muda wa km wiki tatu tangu uvimbe uanze.

Nikijaribu kusoma makala kwenye google juu ya kipimo cha HIV na kufahamu iwapo umeathirika, ile makala inaeleza kwamba kuvimba kwa tezi shingoni (mtiko) ni njia mojawapo ya kutambua kuwa una HIV. njia ya pili ni kupima HIV test.

Leo 19 February 2015 nimepima HIV Hospital ya wilaya nikaambiwa ni Negative. Nashindwa kuelewa kwamba ni muda wa irus kuonekana kwenye vipimo ndo haijafika au namna gani? Kibaya zaidi tulipanga kuoana na yule mchumba wangu mwezi machi mwanzoni na ninashindwa kumueleza kuwa mi ni mgonjwa ili hali vipimo havioneshi kwamba mi ni mgonjwa, atasema ni mbinu ya kutaka kumuacha.

Jamani nifanye nini mie sitaki kumuangamiza roho isiyo na hatia. Naombeni ushauri wenu wanajf wenzangu.
 
Utajiua kwa hofu, mtu usha pima zaidi ya mara moja na majibu ni negative unaacha kujilia ugali wako unabaki kuusikilizia mwili kama simu, itumie akili yako vizuri kuanzia sasa na kuendelea.
 
Pole sana mkuu,nenda kwa daktari/hospital tena halafu ueleze kila dalili uliyonayo wenyewe ndio watajua wakupime nini na matibabu yawe yapi,halafu relax lol naskia ukiwa unawaza sana,immunity yako inakuwa ndogo,unakuwa vulnerable to deseases ....sina uhakika na hii theory lakini lol
 
Zilaumu ny**g mshindo zako! Yaani umekwenda kununua asali ukiwa huna wazo la kusex, then from no where umejikuta umesex kwa kushawishiwa na mwanamke! Uanaume wako uko wapi sasa? Au hujui MAANA ya kuitwa MWANAUME? Miaka 30 bado unafanya upumbavu tu juu ya maisha yako?

Nisamehe kwa kukukemea kama mtoto mdogo ila jombaa umenikera sana kwa kukosa kwako MSIMAMO juu ya maisha yako sababu tu upewe BURE kichupa hicho cha asali mbichi! Sikatai hata mademu wana haki watutongoze lakn kuwa makini kabla ya kufanya maamuzi usikurupuke! Cha kufanya hapo katest tena kwa mara ya mwisho tarehe uliyoambiwa, ukikutwa salama OKOKA kabisa na UBADILI mfumo wako wa MAISHA!
 
Kwani baada ya kusex na huyo mama, hukutumia ile kitu inayoitwa Zuma style, ya kukimbilia bafuni na kuoga chapuchapu na 'kuviflush virusi' vyote?!
 
Acha presha....kwani cha ajabu nini bhana si umepima huna?? Kula maisha kapime malaria afu uwe unavaa masweta inaonyesha ulipo kuna barid na usinywe vinywaji vya baridi mbona utakuwa poa....komaa wewe mtoto wa kiume
 
Nakumbuka hali kama hiyo ilinikuta mimi nikiwa form five tosa boys…nilishindwa hata kusoma nikarudi nyumbani kupumzika nikijikuta naumwa tu kitu nachoumwa hakionekani ila ilikua ni hofu tu baadae nikawa fresh…hiyo ni hofu tu tulia mkuu utakua poa usijali!!
 
Kinacho kusumbua wewe ni hofu na umeugua kwa hofu tuu lakini ni wazi wewe ni mzima! Unatakiwa ujifunze kutovamia kila mtu hata kama una condom! Tatizo lenu mnavamia kila zizi hata mnayo jua wanyama waliyomo ni wabovu mnakwenda tuu tena peku! Halafu lingine huna elimu juu ya ukimwi na virusi yani unafikiri hizo ni dalili za virusi?Virusi havina dalili maalum na hata ulicho kisoma ujakielewa.

Unafikiri ukiumwa hayo ndio una virusi? Elimu inahitaji sana kuna tatizo kubwa na huyo mama aliye kwambia kuwa ndani ya saa 72 unaweza kukimbia ukapewa dawa za kuzuia anafikiri zinatolewa ovyo ovyo?Yani ufanye uzembe halafu utegemee kupewa dawa? Hizo dawa zinatolewa kwa case maalum..hasa kwa wanao fanyia watu operation.
 
Yaani wewe ulikua umekaa tu wakati unaanza kushawishiwa ukazidi kutega sikio na hisia mwisho ukajikuta sivyo ndivyo pole sana . Sasa cha msingi hapo ondoa hofu hata kama umeathirika usiogope kwani hauko peke yako wapo wengi wameathirika si kwa uzinzi bali zipo sababu nyingi zinazopelekea kuathirika. Huyo mchumba wako mwambie masahibu yaliyokupata lkn usiseme umelazimishwa tafuta namna nyingine au sema mwende mkapime kabla ya ndoa naamini hawezi kukataa.

Sali zaburi ya 51 kila siku mpaka utakaposikia amani moyoni mwako.
 
Achen kuutamani ukijana wakati mumezeeka miaka 30 unajiita kijana. hahahahaha. kazi kwel.
 
duh uzee ukiwa miaka 30 wote ni wazee tanzania haina vijana.
 
Wewe ni binadamu wa ajabu kabisa. Unaupenda UKIMWI.

UNA HATARI.
 
Mm dakika mbili umesha kojoa?

hahahaha hizi chipsi hizi?

NIRUDI KWENYE MADA MKUU NENDA PIA

KAPIME NA KIFUA KIKUU TB
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…