Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,433
- 8,585
Hodi Yanga Afrika, najua hampo katika nyakati bora sana, sijui kama mnapokea wageni kwa sasa. Najua nimekuja pasi na taarifa, kama mtanipokea nitakaa, kama mtanikataa basi kheri. Lakini, nimekuja na hoja zangu Twiga na Jangwani.
Kwanza kabisa Wananchi, Naheshimu historia iliyopo hapa, Natambua heshima iliyopo hapa, natambua ukubwa wa hii timu. Ninyi si ndio mabingwa wa kihistoria?? Basi Naheshimu hilo. Najua mlifanya kazi kulifikia hilo.
Hoja yangu ya kwanza inaanzia hapo, mnafanya nini kulilinda hilo?? Mna timu bora uwanjani?? Mnashinda mechi zenu ipasavyo?? Mnaifurahia timu yenu?? Haya maswali matatu ya mwisho yanajibu hoja yangu ya kwanza.
Sambamba na hilo wananchi, nina neno kwa Menejimenti yenu. Kwa sasa mnapaswa kukaa chini, kushughulikia timu yetu. Mnapaswa kuwa na umoja na kutengeneza Yanga imara. Yanga imara uwanjani haiji bila Yanga imara ofisini.
Ni muda ambao, mnapaswa kukaa chini na kutambua malengo yenu kisha myasimamie. Si muda wa kutazama majirani wanafanya nini, wao wanafanikiwa kwasababu kuna muda walikuwa watulivu wakasimamia malengo yao.
Hoja yangu nyingine inaweza kuanzia hapa, Malengo yenu ni yapi hasa?? Kuna malengo ya muda mfupi na malengo ya muda mrefu. Taji la ligi haliji kwa timu iliyoundwa kwa usiku mmoja. Timu ya kutisha Afrika haitengenezwi kwa jioni moja.
Najua mnajua kuwa, ili muunde timu bora uwanjani mnapaswa kutumia pesa. Hoja nyingine inakuja hapa kwamba, hii pesa inatoka wapi?? Kwenye vyanzo vya timu ambavyo hatuvijui?? Mifukoni kwa wanachama?? Au mfukoni kwa mwekezaji kama walivofanya majirani??
Nadhani ili la mwisho ni rahisi zaidi. Mruhusuni mtu mmoja mwenye pesa awekeze. Nafikiri hilo ni rahisi zaidi na maamuzi yatafikiwa kirahisi zaidi kuliko kinachofanyika sasa.
Mwisho kabisa, msiwaaminishe mashabiki ambacho mnajua kabisa hakiwezekani. Shusheni presha ya mashabiki kwa kuwafahamisha kwamba, sasa mpo kwenye mchakato fulani. Wa kusuka timu pamoja na wa kusimamia mchakato wa uendeshaji. Mashabiki wakitulia, mtapata nafasi ya kufanya kazi kwa utulivu zaidi.
Naomba kuwasilisha wananchi[emoji120]
.
[emoji871]@deo_mwanasoka