Nina imani ndogo sasa kwa hawa utumishi!

Nina imani ndogo sasa kwa hawa utumishi!

Ndikwega

R I P
Joined
Feb 1, 2012
Posts
5,979
Reaction score
5,527
Wana wa nchi hususa tunaosaka ajira, nilikuwa na imani kiasi kwa hawa utumishi na ajira zao ila sasa imetoweka. Wao wanadai ukifanya usaili wa mahojiano na ukapata wastani wa alama 50 tayari unafaa kuwa mtumishi wa umma hivyo unawekwa kwenye kanzidata yao.Swali:kwanini watangaze nafasi za ajira watu waombe wakati waliyoko kwenye kanzidata hawajapangiwa vituo? Binafsi najua nimo kwenye kanzidata yao na nina imani kuwa alama zaidi ya hizo wanazozitaka (50), na kuna wenzangu pia kama 8 hivi wote tulifanya mtihani wa mahojiano toka mwezi Agosti kimya mpaka sasa.

Nimeleta uzi huu humu maana wao kuna jambo niliwauliza walinijibu kihuni huni tu ko naona wanachezea ufahamu wa watafuta kazi haw. Ninyi mnasemaje Waungwna?
 
Waulize taratibu za kuanza kazi zipo Vipi?,na huwa mara nyingi nafasi zinatangazwa baada ya mahitaji na nafasi kubainishwa.
Vile vile huwa inaenda sambamba na bajeti na pesa kutengwa kwa ajili ya waliopata ajira husika.
sasa kuna jambo ambalo linaendelea!
[1].Waombaji na wahitaji ni wengi kila kukicha.
[2].Serikalini kuna uvuvi wa kupekua mambo ya nyuma,watu wanaanza na habari ya leo
[3].Taasisi inayohitaji hizo nafasi haijakumbushia kuletewa watu kujaza hizo nafasi
[4].Kwa sasa Serikali haina fedha,inapumulia mashine.!!!
[5].Hata "know who" inawezekana{uchakachuaji unawezekana pia}

Ushauri:
[1].Omba UFAHAMISHWE taratibu zinakamilikaje mpaka mtu kuanza kazi
[2].Endelea kuomba kazi kwa taasisi na nafasi mbalimbali kwa kadiri utakavyokuwa unakutana na matangazo.!!
 
Back
Top Bottom