Nina kadi tano za vyama vya siasa.

Nina kadi tano za vyama vya siasa.

Wa kusoma

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2011
Posts
3,454
Reaction score
2,975
Nimeona nijitokeze hadharani kuelezea idadi ya kadi za vyama vya siasa ninazomiliki ili kama kuna sheria inayokataza mtu kuwa na kadi zaidi ya moja za vyama vya siasa nisifungwe bure.
1. Kadi ya NCCR, UDP na TLP nilizipata mwaka 2005 wakati wa uchaguzi mkuu. Wakati huo niko shuleni wakati wa kampeni wanasiasa wa vyama mbalimbali walikuwa wanatufuata wenyewe wanatupatia kadi hizo bure bila kuomba.
2. Kadi ya CCM na CHADEMA nimezipata 2010 bila kuziomba kama hii ya CDM alipewa jamaa fulani akaniletea nyumbani wakati mm ndio nimetoka chuo.
Tangu nichukue hizi kadi sijawahi kuona mtu yeyote akinifuata nizilipie na sijalipia hata kadi moja.

Naomba kufahamishwa kama nina kosa kisheria ili nizichome moto zote,au mnichagulie nibaki na kadi gani.

Asanteni naomba kuwasilisha.
 
Jinsia yako na tabia yako uliyofanya vinaendana.Ila kwa mwanaume sio sawa
 
ile uliyopokea kwa mara ya mwisho ndiyo inatambulika kisheria
 
Mimi pia nazo Kadi tano zote za CCM! Mbili ni za umoja wa vijana na tatu ni za CCM nilipewa kati ya mwaka 1990 na 1995 na wagombea mbalimbali wa CCM, kuanzia wajumbe wa baraza la UVCCM, wenyeviti wa mitaa, madiwani na wabunge katika maeneo tofauti!
 
Ya cdm ndio yako ile ya mwisho zingine unaweza kutunza au kuchoma moto. Kuna muda zilikuwa zikichomwa motoinaoekana kama kuwadhalilisha ccm, sijui imekwaje tena nape anajua
 
Back
Top Bottom