Nina laki 9, nifanye biashara gani?

planexboi

Member
Joined
Aug 5, 2021
Posts
45
Reaction score
229
Natumaini mko poa

Nina miaka 24 sasa.nilitoka nyumbani nikiwa ni miaka 22 na kuamua kujitegemea ,niliondoka nyumbani nikiwa na elfu 50 mfukoni nikaenda geita kutafuta maisha.

Sikuwa na ndugu yeyote ,sikuwa na kazi maalum ya kufanya kwa hyo kiasi nilichokuwa napata kiliishia tu kwenye chakula,

Baada ya ugumu wa maisha kuzidi niliamua kuingia machimboni eneo la rwamgasa-KATORO,nimekaa huko pesa nilizokuwa napata ilikuw kidogo sana ,

Sasa mwezi uliopita nimebahatisha kupata millioni 1 na laki 2 baada ya kuuza dhahabu,nimelipa lipa madeni ya watu nimebakiwa na laki 9 nimeziweka MPESA, huku machimboni kugumu sana hasa kama hauna mtaji wa kutosha.

Nimeamua nitoke ili hata hiki nilichokipata kisitekee chote.naombeni ushauri nimefika leo nipo katoro mjini ,nifanye biashara gani ambayo ntakuwa napata elfu 15 kwa siku.


Nahitaji michango yenu ya mawazo wakuu.
 
Tulia sana mzee, labda ufanye matching guy(machinga) maana naonaga watu wana 10m wana muuliza fred vunja bei wafanye nini.
 

Kijana kwanza hongera kwa mapambano hayo. Ningekushauri ufanye hili kama utapenda inaweza kukusaidia sana.
Nenda Mwanza, panga chumba miezi 3 cha elfu 15 kwa mwezi, chukua godoro la 50elfu. Hapo utakuwa umetumia laki moja.

Pesa iliyobakia nenda kisiwani, ulizia kisiwa cha Bwiro, nenda kule unakuwa unanua samaki wabichi kisha unawabanika, kuna wamama wanafanya kazi hiyo ya kubanika unawalipa kidogo sana.

Samaki wakavu utakuwa unawaleta Mwanza mjini kisha unawauza kwa bei ya JUMLA na kisha unarudi tena kisiwani kuchukua mzigo. Mtaji wa laki tano unatosha kabisa kufanya biashara hii na utapiga faida sana.

Unaweza pia kuwa unawabanika samaki kisha unawapeleka migodini Geita kule utawauzia mama Ntilie kwa faida nzuri sana.

Kama hii biashara utaiona ngumu unaweza kusema hapa kisha nitakushauri biashara nyingine.

Mungu akutangulie.
 
Uza visheti shule ya msingi
 
Fanya hii biashara
 
Pita na hii thread usiache page hata 1,fanya kama unasoma story book hakikisha umesoma kitabu kizima ukishakimaliza naamini kichwani mwako hautokua kama kabla hujapitia na hii thread....👇

 
Ukisoma hii thread ukitoka haujapata kitu,itabidi tuelekezane kanisa la kwenda tukaombe pamoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…