Nina machache, Niambie lipi lililokufaa?

STUNTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
13,076
Reaction score
17,247
1-Msichana mwenye ndoto za kuolewa na mtu
mwenye mafanikio wakati yeye anamiliki lipstiki
& wanja tu anahitaji maombi
2-
Bora kupendwa na mtu mwenye tabia za
kimalaya, ukimfumania unamtema kama ugoro
wa bibi...kuliko kupendwa na mtu mwenye roho
mbaya, ukimwambia umelazwa ICU anakujibu SAWA
3-
Big up wale wasichana wanaowazungusha
wanaume pale wanapowatongoza .
Ila poleni kwani siku mkiingia line na kitambi
hakichelewi....
4-
Hupaswi kuhuzunika kwa jambo au kitu ambacho
hukuja nacho duniani iwe ni shida utajiri ipo siku
utaondoka na utaviacha...
5-
Mwanamke haulizwi umri.
Mwanaume haulizwi unafanya kazi gani...
6-
Kama akili yako imezidi utimamu na unataka
kuupunguza, jaribu kumpenda mtu asiejipenda
mwenyewe Kama hajajitambua bila shaka atakusumbua tu. Watoto waachie watoto
wenzao. Cheza na size yako
7-
Ukitumia akili na nguvu nyingi kutafuta
wasichana pesa itakukimbia...ila ukitumia akili na
nguvu nyingi kutafuta pesa wasichana
watakukimbilia...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…