Nina mashaka hapo baadae na music life ya Alikiba

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Oii mamb vp wadau, mimi sipo team yoyote ila napenda mafanikio ya msanii iwe diamond ama alikiba ama msanii yoyote anaepata mafanikio kupitia music industry.

Sasa nirud kwenye mada kuu, nasema nina wasiwasi kwa alikiba sababu ya deal lake la SONY, nasema hivo sababu sasa hivi namuona DAVIDO alivo na stress za kukaa mda mrefu bila "kuruhusiwa" kuachia ngoma, imepelekea ameonesha hisiaa zake wazi katika mitandao ya kijamii mbalimbali ikiwemo, SNAPCHAT, hana raha, mashabiki wake hawana raha, wapenda mziki wake alikozaliwa nigeria hawana raha, na daily nikifuatilia naona wasanii kibao ngoma zinatoka na wengine wapya wanakuja na moto mkali,

Sasa ALIKIBA mtanzania mwenzetu na mashabiki wake kwa ujumla na mashabiki wanaopenda mziki tunawasiwasi ndugu yetu kama kuna uwezekano wa ku terminate contract bas fanya hivo ama kaa na management mshauriane msiangalia jina tu sababu ni SONY ama msiangalie hela tu, angalia reputation kwanza,

Mtu kama DAVIDO alikua na uwezo wa kuanzisha lebo yake ama studio kama diamond alivofanya(WCB), sasa sjui ndo sony wanavofanya kazi ama vipi mana miezi 9 unakaa bila ngoma aise na ulizoea kutoa ngoma na zina hit stress yake sio mchezo. Pole sana davido.

ALI KIBA WATCH OUT. Ni advice tu.
 
naona makala za ushuri kwa alikiba zimekuwa nyingi
 
Kufikiria ku-terminate mkataba ni mapema sana kufikiria hilo suala! Angalau mwaka mmoja ingekuwa umepita ndipo angalau mtu angeweza kufikiria hilo jambo!! I know, SONY wana matatizo sana but still it's too early to judge ingawaje ni ukweli pia hivi sasa hana tena ile freedom ya kufanya atakacho hususani suala la kwamba atoe ngoma wakati gani!!!

Hatari kubwa ninayoiona upande wake ni ile operation flow iliyopo Sony na studio zingine kubwa kama Sony! By work flow I mean, Ali Kiba asiye wa Sony alikuwa na uwezo wa kuandika wimbo mwenyewe, akapanga melody mwenyewe na aka-suggest hata midundo! Lakini hata kama mojawapo ya kazi hizo ingefanywa na mtu mwingine bado ingefanyika at low cost!

Kinyume chake, Kiba wa Sony akithubutu melody kutengenezwa na proffesional wa Sony ahesabu maumivu; mashairi yakiandikwa na professional wa Sony ahesabu maumivu! Yaani kila kitakachofanywa na Sony kwa niaba ya Kiba kitakuwa very expensive for Kiba manake hata mauzo yakifanyika, atakuta % fulani imeenda kwa mtengeneza melody, % hii imeenda kwa aliyetengeneza storyline ya video n.k na at the end of the day, unakuta mwenyewe umebakiwa na kiasi kidogo sana!!

Tukija suala la kuvunja mkataba... hakuna kitu kama hicho!!! As I said, bado ni mapema mno lakini ikitokea kwamba hata Kiba mwenyewe ame-fed up, basi awe anakesha akisali kuomba Sony wenyewe ndo wavunje mkataba lakini sio yeye... hataweza!!
 
Duh mkuu kaz ipo. Kama davido msanii mkubwa afrika ana stress saivi, ali atafanyaje...hivi kutengeneza lebo yako na ukajiamini unachofanya ni kazi sana??
 
Hakuwa na watu wenye utaalamu wa kumshauri kabla hajamwaga wino na SONY?

Au ndo yale ya kumwaga wino ili amkomoe Domo?
Hapa ndo unaona umuhimu wa kua na management iliyo makini zaidi sijui kama walikaa chini wakatafakari kwa kina.
 
1.Timu hizi ndo zina haribu wasanii, na ubaya wengi(si wote) walioko kwenye tim Kiba wana mchukia Domo kwanza kabla ya kumpenda Kiba, yaani wengi wako kwa Kiba kwa sababu tu hawampendi Domo sasa chuki hazijengi
2.Ali Kiba hana menejment nzuri
*mawazo yangu tu hayo lakin
 
Aisee,ile wiki ya kiba ndio ametia saini kwenye mitandao kulichafukwa si kitoto,kila aliyesema kinyume cha sherehe yao alikuwa ni hater kwao. Ok hayo hebu tuyapotezee maana kama ni ushauri umeshatolewa wa kutosha.Sasa ni wakati wa kutupa shida kule na kusonga mbele,HEBU TUMUONE MWENYE MUZIKI WAKE WA BONGO FLEVA MAPOKEZI ALIYOPATA JANA HUKO MOMBASA.

 
Wana mu overhype sanaaa, ni mwana muziki mzuri ila hawezi wekwa level za mondi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…