Nina mashaka na malaria test kit, ni bora mafundi maabara watumie hadubini kama zamani

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
3,315
Reaction score
5,058
Zaidi ya mara nne naenda kupima naambiawa hakuna malaria.

Nikiangalia mwili wangu upo hoi na hauna nguvu, watu wa hospital Hai wanapima kwa kutumia Malaria test Kit. Mbona hawatumii darubini kama zamani? Maana matokeo yanazingua jamani, mtu unaumwa alafu unaambiwa hauumwi.
 
Kiukweli hiki kifaa kinapingwa na wengi sana hasa katika kutoa majibu sahihi ya malaria.

Nadhani kinatumika sana kutokana na urahisi wake wa utoaji majibu..kupima watu wengi na kupata majibu kwa muda mfupi.

Ila kwa maoni yangu nadhani microscope kama sijakosea ni kifaa kizuri zaidi katika upimaji wa malaria.
 
Leo nimemwambia Dk lazima anipe Dawa. Lasivyo ningekufa maana hakuna uhalisia.
 

1. Kwanza Sio kila homa ni Malaria,mwii kukosa nguvu sio dalili ya Malaria pekee
2.Ubora wa kipimo husika unategemea vitu vingi, expiring date,joto sehemu ya kuhifadhia na sehemu ya upimaji.
2.Ubora wa kipimo,je kimethibitishwa na TBS.

Ushauri wangu kama umepima kweli hizo mara tatu, it's likely huna Malaria,fanya vipimo vingine zaidi,using'ang'anie dawa za Malaria.

Asante
 
Self diagnostic unaipata boss?
 
Kumbe unajua kabisa mwili wako unaweza kutambua kuwa una malaria bila hata kupima?
Unatumia vibaya neno self diagnosis,kuna baadhi ya shida za mwili ni rahisi kuzijua bila hata kufanya kipimo chochote,ila kwa Malaria tunasema kuna clinical Malaria symptoms ambazo hizi daktari anaangalia tu dalili bila kupima anakuambia una malaria kwakuwa kuna criteria zinakuwa zimefikiwa,ila kwa upande wako ndugu,dalili moja haiwezi kuthibitisha kwamba una malaria!
 
Dalili mmoja hutegemea na mtu pia. Nina jamaa yangu yeye akipata malaria koo huwasha. Apime asipime koo humuwasha kisha mafua na dalili zingine. Mimi huwa general body malaise.
 
Mkuu,pole Sana,Ila sio kila uchovu Ni malaria,wewe ulijuaje kuwa Ni malaria na sio UTI au magonjwa mengine,kwanini ukazane malaria tu?

Ok,nakubaliana nawewe kuwa kipimo hicho kina shida kidogo,lakini si kwa kutumia analysis uliyo fanya wewe,Mimi niliwahi kujihisi Nina malaria,nilipopimwa kwa kipimo hicho ulichotumia wewe yaani MRDT,Nilikuwa negative,niliyakataa majibu na kumwambia daktari anipime kwa kutumia kipimo kingine,kwani nilikuwa na Hari mbaya,alipotumia BS,nilikuwa nina malaria.

Lakini pia Kuna muda niliwahi kuwa na dalili za malaria ,nilipopimwa kwa Kipimo Cha BS,niliambiwa Sina malaria,nilimpinga daktari,naye akanishauri nipimwe UTI,nilipopimwa nilikutwa ninayo.

Hivyo usitumie njia moja kuhalalisha uwepo wa ugonjwa,nenda mbali Zaid mkuu,utaathiri afya yako.
 
Dalili mmoja hutegemea na mtu pia. Nina jamaa yangu yeye akipata malaria koo huwasha. Apime asipime koo humuwasha kisha mafua na dalili zingine. Mimi huwa general body malaise.
Sawa mkuu,ila unaonekana umeizoea hiyo dalili kwamba ukiipata inaashiria Malaria kwa upande wako,kuna magonjwa mengi sana yanasababisha general body Malaise,so uwezekano pia wa kuwa na shida nyingine upo that's why nashauri, you need to have other investigations to find out what is really happening to your body!
 
What if unakuwa na general body malaise alafu unafanya investigations zinakupa negative?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…